Ukweli hata mimi naona mabadiliko makubwa katika utendaji wa jeshi la polisi toka wakati wa kurejea kwa Tundu Lissu. Wamejitahidi kutoingilia shughuli za kisiasa kwa kuwatanya wanasiasa na shughuli zao.
Ila kasoro moja bado ipo ya kuwa kamata watu na kuwaweka ndani kwa muda mrefu bila kuwafungulia mashitaka au kuwapa dhamana bado haijaisha. Hili halina tija wala masilahi kwao na taifa. Mfano hivi wale vijana wa CHADEMA bado wanashikiliwa kwasababu gani mpaka sasa kutokana na kile polisi walicho ita kuogezea maneno kwenye wimbo wa taifa kitu ambacho hata vijana wa CCM walifanya lakini hakuna aliye kamatwa. Kwanini bado wanamshikilia aliye changia uzi wa Mange badala ya kumpa dhamana au kumpeleka mahakamani?
Wakati mwingine ni kama jeshi linajua kabisa hakuna mashitaka ila lina amua kutoa adhabu kwa kuwashikilia ambapo hicho ni sawa na kifungo ambacho hakijatolewa na mahakama. Sirro aangalie hili jambo ukweli lina kera. Kumnyima mtu uhuru kwa kisingizio chote chote kile hakukubaliki. Hivi hao vijana wanashikiliwa kwa uchunguzi gani wanaouchunguza. Mbona nyimbo zipo hadharani wana chunguza nini? Common jeshi la polisi change now! However you are currently doing a good job!