Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

Huu msemo unatumika sana, lakini binafsi huwa siuelewi yani unamnyonga mtu halafu unampaje haki yake.

Naona kama msemo wa kinafiki. Wataalam hebu nisaidieni.


Wahenga waliotunga hiyo methali walikuwa wamekunywa pombe nyingi ndipo wakatunga, ni moja ya methali isiyoingia akilini.

Ni sawa na methali inayosema; "Mpe mchawi alee mwanao", yaani mtu mbaya ndiye umkabidhi akutunzie hazina yako!!! 🤣
 
Misemo Haisomwi Kama gazeti
Mnyonge mnyogeni haki yake mpeni maana yake kila mtu ana madhaifu na uimara wake, au mabaya na mazuri yake
Hivyo usiseme mabaya tupu sema na uzuri wake
 
Back
Top Bottom