Mnyoosho unaendelea: Diamond ashinda tuzo African Achivers Awards usiku huu

mkuu mi naona ilitokea bahati mbaya tu kama binadamu ila sababu inayonifanya nizisambaze ni baadhi ya mashabiki wa daimond kubisha kwamba hawezi fanya hivyo labda afande sele ndo maana nawawekea kila ninapo waona

Mbona tunazifahamu? Huyo anayesema Diamond hawezi kufanya hivyo labda ameanza kumfatilia Diamond jana.
 
Hivi diamond hizo pesa za nauli mara south afrika mara nigeria nani anampa? nakumbuka swaiba yangu Juma Nature alichaguliwa kugombea tuzo Sweden nauli ya kwenda huko alikuwa hana ,, ilibidi tufanye harambee tumchangie nauli.
Diamond ni brand... mtu ukishakuwa brand vitu kama hivyo ni vidogo sana coz' huwa zinatokea kampuni za kudhamini hayo mambo... kwa mfano, kwenye MTV, Fast Jet walimsafirisha yeye na team yake kwenda na kurudi!!
 
vituzo maandazi lakin jukwaani hana kitu huyu domo, mziki hajui kuimba zero,tuzo za kununua nyambafu
 
jukwaani zero kichwani o. na tungo zero,tuzo ya kununuaaa

Mwisho wa siku western and south Africa mtu wanaemjua kama nembo ya taifa (Tanzania) kwenye sanaa ni Diamond. AY amejitahidi ila hajafika level ya jamaa.
 
Mwisho wa siku western and south Africa mtu wanaemjua kama nembo ya taifa (Tanzania) kwenye sanaa ni Diamond. AY amejitahidi ila hajafika level ya jamaa.

wote hawa ndomo na AY hawajafika level ya KING
 
Labda nisaidie kuemwaelezea wale wanaosema hizi tuzo za kununua au si za maana kwasababu hakushindanishwa na baadhi ya wasanii wengine wa Afrika, ukirejea ile barua iliyowahi kutolewa na uongozi wake ilionesha katika kipengele alichokuwa Diamond kulikuwa na wasanii wengine wengi tu na mchujo ulifanyika hatimaye Diamond akafanikiwa kuingia fainali, halafu ni tuzo ambayo unapewa kutokana na impact ya kitu unachofanya, yaan wewe kama mwanamuziki je jamii yako imenufaika vipi na kwa kiasi gani kipaji chako ukiacha mbali kuburudisha, sasa majaji wanaangalia vyote hivyo siyo unaimba tu na kupata tuzo nyingi ila jamii inayokuzunguka haifaidiki na hicho kipaji ulichopewa na Mungu. Wito wasanii wetu wafanye kazi na kuhudumia jamii zinazowazunguka pia wajaribu kusambaza kazi zao za kijamii ili wasanii wengi zaidi wapate tuzo za aina hii, umaarufu wa jina lako tu ukiutumia vizuri basi jamii zetu zitafaidika zaidi na kuipunguzua Serikali yetu mzigo
 

pelekeni uko taarabu zenu
 
kwa stayle hii madai ya q chief ni kweli 100%

Nadhani unasahau kuwa maisha ni safari yenye changamoto na mabadiliko mengi. Pia unasahau kuwa ili kuweza kufanikiwa jambo fulani kuna wakati inabidi ujitoe muhanga. Bila kujitoa muhanga Diamond asingefika hapa alipo sasa. Afrika isingemjua. Wala Amerika isingemjua.
 
Bahati mbaya au nzuri siko africa
Hakuna aliyekuuliza upo wapi na issue yenyewe wala haitegemei upo wapi ili uweze kuafahamu kuhusu awards tajwa!
na if like ningependa kukupa elimu kiduchu kuh hao nigerians ambao wana create hizo vitu inshort ni matapeli tu wa kawaida even u ni kiasi cha kusetle nao tu ili ushinde thats why unaona daily huyo daimond yupo huko lagos,
Yaani ndo elimu hii? Uliona wapi legitimacy ya kitu inapimwa kwa kuangalia citizenship ya wahusika? Kama issue ni u-Nigeria, kwahiyo unataka kusema hata Dangote anayewekeza kule Mtwara nae ni tapeli? Badala ya kuangalia team inayounda taasisi husika na profile zao wewe unazungumzia citizenship!!!!
ifike muda wa tz muamke kidogo
Kabisa, sema ondoa hiyo "m" kisha i-replace na "t"... au sio mwenzetu ndugu? Manake Kiswahili chako kimenyooka ile mbaya!!! Duh! Kumbe ndo maana Maboso ameniambia natumia rungu kuua inzi!! Manake we mwenzetu inaelekea hufahamu hata waliotumbuiza hivi majuzi kwenye Road to MAMA achilia mbali waliotumbuiza kwenye tuzo za CAF January 2015 mjini Lagos!! Mara oh, sipo Africa as if umeulizwa lakini bado hauna access to information!!! Nilidhani Africa ndo bara la mwisho kabisa duniani kwa barriers to information!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…