Mo afafanua ununuzi wake kwa Simba

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,227

Na Saleh Ally
MFANYABIASHARA bilionea kijana Mohammed Dewji maarufu kama Mo, ametangaza kuwekeza katika Klabu ya Simba kwa kutoa Sh bilioni 20 ili amiliki hisa kwa asilimia 51, jambo ambalo limezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wanachama wa Simba.
Lakini limekuwa gumzo hata kwa wapenda michezo wengi kuhusiana na namna ambavyo suala hilo linakwenda, kwamba je, Simba wanapaswa kuingia kwenye mabadiliko au la?

Mashabiki na wanachama wengi wa Simba, wanaonekana wazi wanachotaka ni mabadiliko na kwa asilimia kubwa wameanza kuushinikiza uongozi wa timu hiyo kuhakikisha unaingia kwenye mabadiliko hayo kwenda kwenye kampuni na baadaye mfumo wa hisa uanze kutumika.
Baadhi ya wanasiasa, nao wameonekana kuunga mkono ingawa wamekuwa na mawazo tofauti lakini msisitizo kuwa ni wakati mwafaka kwa Simba kuingia kwenye mabadiliko hayo.

SALEHJEMBE:, ilifanya juhudi za kumpata Mo Dewji ili kuzungumza naye kuhusiana na suala hilo ili kujua maoni yake kwa undani zaidi na nia yake hasa.

SALEHJEMBE: Sh bilioni 20 si fedha kidogo, nini hasa kitakufaidisha wewe kama mfanyabiashara kuingiza fedha hizo ndani ya Simba?

Mo: Niseme ni suala la kujiuliza lakini jibu la kwanza nitakuambia ni mapenzi yangu kwa Simba. Lakini ninaamini nitakaposhirikiana na wanachama na mashabiki wa Simba, tutakwenda kwenye mabadiliko na kuifanya Simba kuwa klabu bora ambayo ina uwezo wa kushindana barani Afrika na mwisho mafanikio yatapatikana.

SALEHJEMBE: Unaamini kinachosababisha hivi sasa kuyumba kwa Simba ni fedha peke yake?

Mo: Lazima uwekeze fedha ndiyo ufanikiwe. Lakini lazima uwekeze mfumo kwa ajili ya kuziendesha kwa mwendo sahihi hizo fedha. Simba haiwezi kushindana tena na Yanga na Azam FC kwa kuwa haina fedha. Wao wanafanya mambo mazuri, wanasajili kwa uhakika, kambi bora, huwezi kuwashindanisha na Simba.

SALEHJEMBE:Umesema unatoa Sh bilioni 20, halafu unapenda kuweka bond na baada ya hapo Simba itatumia faida ya hiyo bond kujiendesha. Sasa fedha unayotumia inakuwa ni ile uliyonunulia, huoni hapo unapata faida mara mbili?

Mo: Fedha hiyo ni ile ya Simba, bado inaweza kutumika kwenye maendeleo. Mimi pia ninaweza kuwekeza zaidi. Pia kumbuka fedha hiyo ya Simba itakuwa salama itakapokuwa kwenye ‘treasury bond’. Usipoiweka kule italiwa na mwisho itakuwa Simba ndiyo imepoteza.

SALEHJEMBE: Umepanga kutoa Sh bilioni 20 upate asilimia 51, una uhakika fedha hizo ni sawa na thamani hiyo kwa Simba ambayo ina majengo, viwanja na hata thamani ya nembo yake?

Mo: Nikuambie ukweli, Sh bilioni 20 ni fedha nyingi sana kwa anayeelewa biashara. Ningeweza kununua benki au ningeweza kununua klabu ya daraja la pili barani Ulaya, mfano kwa nchi kama Ureno. Lakini mapenzi ndiyo yamenisukuma kwenda Simba.

SALEHJEMBE: Nirudie kuhusiana na majengo, huoni yana thamani kubwa na huenda ungepaswa kuongeza?

Mo: Majengo yale pale Msimbazi thamani yake kupitia utafiti wao Simba ni Sh bilioni 3.5. Wewe utaangalia vingine vinavyobaki ni kiasi gani.

SALEHJEMBE: Kama unaona Simba thamani yake ni chini, vipi utoe fedha nyingi zaidi?

Mo: Unapotaka kununua biashara kuna mifumo miwili, mmoja ni Valuation to Earn Ration. Unamuuliza mtu anaingiza kiasi gani kwa mwezi, labda anasema ni milioni 100. Halafu wewe unamlipa kwa miezi kumi ambayo ni Sh bilioni moja. Simba imekuwa ikiingiza hasara tu, ningesema niangalie hilo, huenda ningelipa kidogo sana lakini nia yangu ni kuendeleza na kuing’oa ilipo. Inatakiwa fedha nyingi zaidi kuliko ilivyo.

SALEHJEMBE: Umesema kuna mifumo miwili?

Mo: Yaa, mfumo wa pili ni Asset Valuation. Hapa unaangalia thamani ya mali ya unachotaka kukinunua, kwa Simba ukiangalia hilo bado ni chini sana. Hata kama ungeangalia ile nembo, nayo haiingizi faida. Mimi Mo naweza kuwa nauza maji kwa nembo ya Mo lakini hakuna faida kama siuzi, hivyo siwezi kusema eti lazima niuze kwa fedha ya juu maana mtu ananunua hasara.

SALEHJEMBE: Uongozi wa Simba ulikubali kwenda kwenye mabadiliko, ilionekana ni shinikizo la wanachama. Lakini hawakusema wataufanya kwa muda gani, nini ushauri wako hapa?

Mo: Katika barua yangu niliyowaandikia, nimewaomba angalau mchakato uchukue miezi mitatu ili tuingie na kuanza kazi.

SALEHJEMBE:Ulisema utakuwa tayari kusaidia usajili, vipi utawapa kiasi gani?

Mo: Pia niliomba kukutana na viongozi na kamati ya utendaji. Usajili nitasaidia, mimi ni mwanachama wa Simba. Viongozi wengine hapo akiwemo Aveva, tulishirikiana pamoja kuisaidia Simba kuivua ubingwa Zamalek ikiwa timu bora Afrika mwaka 2003, hivyo wanajua kazi yangu na ninavyoweza kushirikiana na wengine. Kuhusu kiasi, inategemea tutakavyozungumza.

SALEHJEMBE: Umesema kuna viongozi hawataki mabadiliko, kina nani hasa?

Mo: Nilisema wanaongozwa na Evans (Aveva), lakini wengi tunafahamiana. Tena ni wachache tu na mmoja nimemwandikia ujumbe kumueleza nashukuru sana kuona ananipinga na hataki mabadiliko.

SALEHJEMBE: Kama mabadiliko yatafanyika, wewe ukaingia, unafikiri ndiyo kila kitu kwa Simba kwa maana ya mafanikio?

Mo: Simba ni klabu kubwa sana, nguvu yake ni watu, fedha ni chagizo la maendeleo. Mfumo bora ni chachu ya kusukuma na kuleta maendeleo. Nikiingia bado nitaendelea kuwa karibu na mashabiki na wanachama wa Simba ili tushirikiane kuingia kwenye mabadiliko ili kutafuta mafanikio.

SALEHJEMBE: Mwisho, unaona mafanikio ya matajiri kama Bakhresa upande wa Azam na Manji upande wa Yanga ndiyo yamekuvuta?

Mo: Labda umesahau, mimi nilikuwa Simba mwaka 2003, kipindi hicho wote hawakuwa wameingia kwenye mpira.

SALEHJEMBE: Vipi ni lazima uwe na asilimia 51 yaani majority share holder, shida nini hasa ukiwa chini ya asilimia 50?

Mo: Nikiwa chini ya asilimia 50 sina changu, kwanza kumbuka ninawekeza fedha Sh bilioni 20, si kitu kidogo ndugu yangu. Halafu kama nitakuwa sina uwezo wa uamuzi wa mwisho, itafikia siku mimi nataka fedha tupeleke kwenye vijana, wengine hawataki na sina nguvu, mambo yakiharibika, watu wataniuliza mimi. Hivyo ni lazima niwe nina uamuzi wa kufanya mambo kukimbilia kwenye mabadiliko na mafanikio.

SALEHJEMBE: Shukrani kwa ushirikiano.

Mo: Ahsante, karibuni wakati wowote
 
"Nikiwa chini ya 51% sina changu"... Mo mjanja sana

Of course yuko sahihi ...ila kuna swali moja ameuliza Saleh Zuri sana na MO ameshindwa kulijibu

Mimi nina maswali wadau mnisaidie:-

1. Simba ni ya nani? Nani anaiuza? Na atapata faida kiasi gani kwenye huo mchakato?

2. (Hili linaendana na nilo la 1), ikishatolewa hiyo 20bil, hela za kuiendesha timu zitatoka humo humo au hizo zinakuwa ni za manunuzi tu, hivyo mmiliki atakuja na hela nyingine ya kuendeshea timu?

3. Tumeambiwa 20bil ni kwa asilimia 51, je hiyo 49% inayobaki nani atamiliki? Atatoa hela equivalent au hizo share zitakazobaki zitakuwa na thamani tofauti?

4. (Hili linaendana na nilo la 3), ikitokea wanunuzi wakakosekana hisa zitakazobaki zitaenda wapi? Na mmiliki atabaki Mo peke yake?
 
Maswali mazuri sana........Nilichojifunza kwenye mchakato huu Mo anataka kukimbiza mambo kwa spidi ili kuwaingiza kingi simba

Hili zoezi inatakiwa samba ndio wawe on top of the game na sio MO........

Maswali yako ni ya Msingi sana...Na ndio maana katika transaction hii kuna umuhimu wa Simba kwenda taratibu sana

Kwa msingi wa kuhakikisha hii long living brand inabaki na thamani yake.....MO ni business man...anavutia upande wake wa faida za kipindi kijacho...sio miaka mitano ijayo...miaka mingi

Hivyo basi nikiwa naunga mkono transformation hii lakini please smart people wawe makini Simba I control hii process na sio MO

CC sembo grafani11 mkolaj Amavubi
 
Mo alisema hiyo 20bil ataikopeshea serikali baada ya miaka kadhaa watavuna return ya hela ambayo itakayo tumika kujenga timu ikiwa pamoja na kujenga kiwanja etc...

Hizo hisa 49% zilizo baki ni za mashabiki na wapenzi wa simba hata wew unaweza kwenda kununua hzo hisa kama una hela!!
 
Mo alisema hiyo 20bil ataikopeshea serikali baada ya miaka kadhaa watavuna return ya hela ambayo itakayo tumika kujenga timu ikiwa pamoja na kujenga kiwanja etc...

Raimundo ameuliza swali zuri hapa

1. Simba ni ya nani? Nani anaiuza? Na atapata faida kiasi gani kwenye huo mchakato?

Na katika swali hili la mkuu...naomba kukuza mjadala kama hivi....MO akipewa 51% anakuwa na Control ya Kampuni ya Simba.Investment kwenye TBond itafanywa na kampuni ya Simba. Return from Investment ya Bond itaingia kwenye kampuni ya simba ambayo MO ndiye mmiliki....Hauoni hapo kuwa hakuna SALE transaction? Kwa sababu mwenye kampuni MO atakuwa tu anatumia hela yake aliyoiweka kule BOT/Hazina kwenye TBond.

Ndio maana mi naona kuna umuhimu wa kuajiri Proffesional law firm ili kushauri muundo sahihi
 
Mkuu hili kuyumba kwa uchumi wa vilabu ni wimbi la dunia nzima si Simba tu.

Yanga wanasahau mapema hata Manji alishawahi kudokeza hili la Yanga Kampuni na Katiba yao ilipitishwa kwa nusu saa tu pale Police Mess ambapo Maniji alitaka 75% na 25% awanunulie Yanga hizo hisa

Kama tunafuatilia kwa makini, hamasa ya soka imeshuka duniani kote kutokana na mdororo wa kiuchumi na pengine njia mbadala kwa vilabu vingi kwa sasa ni kutegemea zaidi wazalishaji wa bidhaa za ndani kuwadhamini.

Roy Miller kutoka kitengo cha biashara ya michezo katika chuo kikuu cha Liverpool anasema kuwa hali kama hiyo haijawahi kuonekana kwa muda mrefu na ni ishara ya kwamba uchumi uko katika hali mbaya.

Wachambuzi wanaamini hata hivyo kuwa vilabu vikubwa kama vile mabingwa wa Uingereza Manchester United, Real Madrid na kadhalika siku zote zitaendelea kuwavutia wafadhili na washabiki wengi, lakini kwa vilabu vidogo hali ni tofauti.

Ligi kuu ya Uingereza ndiyo ligi yenye kuingiza fedha nyingi kabisa ambapo mwaka jana mapato yake yalifikia kiasi cha paundi billioni 1.5.Lakini ni vilabu vinane tu kati ya 20 vya ligi hiyo vinavyojiendesha kwa faida.

Maswali yameibuka juu ya majaaliwa ya udhamini wa kampuni ya kimarekani ya AIG kwa timu ya Manchester United wa dhamani ya paundi millioni 56.5 ambayo ni rekodi nchini Uingereza.Kampuni hiyo ya kimarekani imelazimika kuokolewa na serikali iliyonunua hisa kubwa za asilimia 80 baada ya kuwa katika hali mbaya ya kuelekea kuwa mufilisi.

Timu nyingine ya ligi kuu ya Uingereza ya West Ham Unitd hivi sasa haina udhamini katika jezi zao baada ya kampuni iliyokuwa ikiidhamini ya XL Leasure Group kufilisika.Nayo West Bromwich Albion iliyopanda daraja imeshindwa kupata ufadhili kufuatia kujiondoa kwa aliyokuwa mfadhili wake kampuni ya simu ya Ujerumani ya T-Mobile.

Newcastle United nayo ilikaribia kuwa katika hali hiyo baada ya mfadhili wake benki ya Northen Rock kuokolewa na serikali ya Uingereza kufilisika ambapo huko Italia timu ya Lazio kwa sasa inacheza bila ya kuwa mfadhili .

Hata hivyo kwa mujibu wa wachambuzi na watalaam wa masuala ya ufadhili katika michezo, timu kama Manchester Uinted haitopata shida kupata ufadhili mwengine iwapo serikali ya Marekani itaamua kuondoa ufadhili wake baada ya kuwa imechukua hisa kubwa katika kampuni ya AIG. Pippa Collet ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayohusika na ufadhili kwenye sekta ya michezo anasema kuwa udhamini katika kandanda kwa muda mrefu umekuwa ukipewa thamani kubwa kuliko inavyostahili, na kwamba hivi sasa kunafanyika marekebisho katika soko la udhamini.

Tanzania haipo kwenye kisiwa, unaona hata mfadhili wa hivi karibuni wa simba kwa kiasi kikubwa HZP amenza kuchoka kutumia fedha zake kusajili, ilihali hata idadi ya watazamaji imepungua sana, na mzalishanji wa bidhaa anayejitutumua kwa sasa ni Azam pekee kupitia udhamini wa TV yake

hakuna namna

nitaurid nikupe udadavuzi wa HISA ZA MO
 
Kuna hicho kipande nime-quote inanipa picha kwamba jamaa siyo kwamba anataka kuinunua Simba bali anataka kuwekeza na aweze ku-control matumizi ya hela anayoinvest!

Kwa sababu kama ni kununua ilitakiwa hiyo hela wapewe wauzaji, yeye akishakuja aje na hela yake ya kuendeshea timu ile aliyonunulia asiitegemee tena, inakuwa kama unanunua nyumba halafu hela hiyo hiyo ndo unaitumia kwenye ukarabati.
 
Mkuu hili kuyumba kwa uchumi wa vilabu ni wimbi la dunia nzima si Simba tu.

Yanga wanasahau mapema hata Manji alishawahi kudokeza hili la Yanga Kampuni na Katiba yao ilipitishwa kwa nusu saa tu pale Polisi Mes ambapo Maniji alitaka 75% na 25% awanunulie Yanga hizo hisa

Mkuu mmiliki halali wa simba alikuwa ni mwanachama wa simba na ndio maana kwa mujibu wa katiba ya simba hapo nyuma ilikuwa hakiwezi kufanyika kikao chochote cha timu hadi ifikie idadi fulani ya namba ya wanachama kwa sababu wao ndio wenye maamuzi zaidi kwenye timu yao.
 
So, hiyo hela ikitolewa watapata chochote?

Maana wao watakuwa ndo wameuza timu siyo?
 
Hapa napasubiria mkuu!

mfumo mzima wa hisa na kuwa mmiliki wa hisa, mathalani mtu anapomiliki asilimia 51 au 20 ya 30, kwa upande wa soko la hisa, kwanza ni la pili la mitaji na kwenye soko la hisa mfumo wake ni kwamba linaruhusu bei ya hisa moja liweze kugundulika kutokana na nguvu za soko.

Hisa ikishaorodheshwa kwenye soko inaorodheshwa siku ya kwanza kutokana na bei ya mauzo ya kwanza kwa umma na kutathmini thamani ya kampuni kwamba ni Sh 500 kwa hisa moja, wananchi wananunua halafu zinaorodheshwa kwenye soko la hisa.

Baada ya hapo anakuja mwekezaji, mfano sasa akija Mo Dewji, cha kwanza Simba lazima iorodheshwe kwenye soko la hisa kama kampuni inayomilikiwa na umma kwa njia ya hisa na kwamba imebadilishwa mfumo kisheria, ikaorodheshwa ikauza hisa ikazalisha mtaji ikaorodheshwa na anapokuja Mo, anaangalia ni asilimia ngapi ya hisa za kampuni hiyo zimeorodheshwa kwenye soko la Dar es Salaam.

kigezo kikubwa kinachotumiwa na wana hisa ni kama wewe ni kampuni ambayo unaingia kwenye soko kuu, unatakiwa kutoa asilimia 25 kiwango cha chini au kampuni ambayo inajaribu kuitumia kibiashara wao kiwango cha chini ni asilimia 20 ya hisa zako na inamaanisha mnunuzi ambaye anataka kufanya uwekezaji wowote, inakuwa rahisi kuutathmini thamani yake kuliko yeye akisema anataka kutoa bilioni 20.

Simba wanaweza wakaenda DSE ili waweze kujua na kutathmini thamani ya mwekezaji anayotaka kutoa isije kuwa tofauti na ambayo mtu (Mo) anasema, yaani bilioni 20

Kampuni ya kawaida yenye mfumo wa hisa ni asilimia 51, chini ya asilimia 50 unakuwa hauna mamlaka nayo na hata kwenye kupiga kura, una kuwa na nguvu zaidi ya wengine.

Hata hivyo wanahisa ni wanahisa, kama kila mtu anamiliki hisa za kawaida, inamaanisha kwamba mimi ni mwana hisa na wewe ni mwana hisa, hata kama wewe una asilimia 51, mimi 10, wote tunahesabika ni wamiliki, tunapata haki sawa sawa, hasa katika kupiga kura. Lakini kwa sababu wewe una asilimia 51, kura yako inakuwa na uzito zaidi, kwa hiyo tofauti ni hiyo. Lakini hakuna vyeo katika umiliki wa hisa.

Hata hao wanaosema atauza kwa Manji akiamua haiko hivyo kabisa kwa sababu yeye ameingiza hisa zake miongoni mwa uwekezaji uliokuwepo tayari, sana anaweza kujiondoa wakati wowote ila sio kujimilikisha
 
sawa sawa
na kwa mfumo wa vilabu wenye dhamana na mali za klabu ni watu wanaoitwa wadhamini ama Trustees kwamba Klabu inaweza kushitakiwa na wao wakawa wahusika wakuu ama hata kushitaki kwa masilahi ya Klabu lakini pia endapo Klabu itavunjika ama kufilisika hao ndio wenye dhamana ya mustakabali wa mali za Klabu
 
Mo anania nzuri na simba
Tuache siasa
Timu nyingi duniani zime nunuliwa na kufanya vizuri
Tuache kuogopa tumpe
 
Mimi tatizo langu ni kwenye kununua au kuwekeza, mfumo ninaouona hapa ni wa kuwekeza ila Mo anatumia lugha ya kununua.

Kwa sababu kununua ni vile unatoa hela watu wanachukua hela wanakukabidhi timu, sasa kwenye kuiendesha inabidi utafute hela nyingine siyo utegemee ile uliyotumia kununulia timu.

Chukulia mfano huu; mimi nina nyumba, nikuuzie upande wa nyumba halafu kwenye ukarabati wa nyumba yote tutumie ile hela uliyonunulia upande wa nyumba, sasa huo ni ununuaji au ni uwekezaji?
 
anachonunua ni hisa na ndio maana tunasema kwa kuwahi huenda amerahisisha mahesabu ya hisa lakini pia ilitakia ifahamike thamani yote ya simba kwa uyakini ndio tujue thamani ya kila hisa kama ni 500 au pungufu au zaidi na ndio maana linaitwa SOKO LA HISA kwa watu kununua hisa kulingana na uwezo wao kwa uelewa wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…