Mkuu hili kuyumba kwa uchumi wa vilabu ni wimbi la dunia nzima si Simba tu.
Yanga wanasahau mapema hata Manji alishawahi kudokeza hili la Yanga Kampuni na Katiba yao ilipitishwa kwa nusu saa tu pale Police Mess ambapo Maniji alitaka 75% na 25% awanunulie Yanga hizo hisa
Kama tunafuatilia kwa makini, hamasa ya soka imeshuka duniani kote kutokana na mdororo wa kiuchumi na pengine njia mbadala kwa vilabu vingi kwa sasa ni kutegemea zaidi wazalishaji wa bidhaa za ndani kuwadhamini.
Roy Miller kutoka kitengo cha biashara ya michezo katika chuo kikuu cha Liverpool anasema kuwa hali kama hiyo haijawahi kuonekana kwa muda mrefu na ni ishara ya kwamba uchumi uko katika hali mbaya.
Wachambuzi wanaamini hata hivyo kuwa vilabu vikubwa kama vile mabingwa wa Uingereza Manchester United, Real Madrid na kadhalika siku zote zitaendelea kuwavutia wafadhili na washabiki wengi, lakini kwa vilabu vidogo hali ni tofauti.
Ligi kuu ya Uingereza ndiyo ligi yenye kuingiza fedha nyingi kabisa ambapo mwaka jana mapato yake yalifikia kiasi cha paundi billioni 1.5.Lakini ni vilabu vinane tu kati ya 20 vya ligi hiyo vinavyojiendesha kwa faida.
Maswali yameibuka juu ya majaaliwa ya udhamini wa kampuni ya kimarekani ya AIG kwa timu ya Manchester United wa dhamani ya paundi millioni 56.5 ambayo ni rekodi nchini Uingereza.Kampuni hiyo ya kimarekani imelazimika kuokolewa na serikali iliyonunua hisa kubwa za asilimia 80 baada ya kuwa katika hali mbaya ya kuelekea kuwa mufilisi.
Timu nyingine ya ligi kuu ya Uingereza ya West Ham Unitd hivi sasa haina udhamini katika jezi zao baada ya kampuni iliyokuwa ikiidhamini ya XL Leasure Group kufilisika.Nayo West Bromwich Albion iliyopanda daraja imeshindwa kupata ufadhili kufuatia kujiondoa kwa aliyokuwa mfadhili wake kampuni ya simu ya Ujerumani ya T-Mobile.
Newcastle United nayo ilikaribia kuwa katika hali hiyo baada ya mfadhili wake benki ya Northen Rock kuokolewa na serikali ya Uingereza kufilisika ambapo huko Italia timu ya Lazio kwa sasa inacheza bila ya kuwa mfadhili .
Hata hivyo kwa mujibu wa wachambuzi na watalaam wa masuala ya ufadhili katika michezo, timu kama Manchester Uinted haitopata shida kupata ufadhili mwengine iwapo serikali ya Marekani itaamua kuondoa ufadhili wake baada ya kuwa imechukua hisa kubwa katika kampuni ya AIG. Pippa Collet ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni inayohusika na ufadhili kwenye sekta ya michezo anasema kuwa udhamini katika kandanda kwa muda mrefu umekuwa ukipewa thamani kubwa kuliko inavyostahili, na kwamba hivi sasa kunafanyika marekebisho katika soko la udhamini.
Tanzania haipo kwenye kisiwa, unaona hata mfadhili wa hivi karibuni wa simba kwa kiasi kikubwa HZP amenza kuchoka kutumia fedha zake kusajili, ilihali hata idadi ya watazamaji imepungua sana, na mzalishanji wa bidhaa anayejitutumua kwa sasa ni Azam pekee kupitia udhamini wa TV yake
hakuna namna
nitaurid nikupe udadavuzi wa HISA ZA MO