Mo afafanua ununuzi wake kwa Simba

Mo afafanua ununuzi wake kwa Simba

Kweli mkuu nakubaliana na mabadiliko kwa timu ya simba lakini kwa njia anazozitumia mo kutaka kujimilikisha simba sio nzuri na sikubaliani nazo kwasababu anaforce mambo yaende fasta wakati wapenzi na wanachama wa simba awajapata elimu ya kutosha kuhusiana uwekezaji mkuu
Anaforce vipi akat kasema ametoa muda wa miezi mitatu? ulitaka atoe mwaka mzima?
 
Mwandishi kasahau swali moja la msingi. Nalo lingeulizwa hiviii.

" Mo unaonaje kama mwana simba na unaeipenda simba ungepeleka ombi kwa uongozi watathmini thamani ya klabu kisha waje na jibu klabu ina thamani gani na baadaye watangaze kuuza hisa katika soko huria ili wenye uwezo muingie kwenye mchakato wa kumpata mshindi ambaye ndo atakuwa mmiliki wa timu. Badala yake unataka wewe upewe direct timu pasipo kushindanishwa na wengine.?"
Iki kipindi cha miezi mitatu iliyopewa simba ifanye iyo tathmini ya thamani ya klabu af watamwambia kama wamekubali pendekezo lake la 20biln, ye mwenye kasema yale majengo ya simba uongozi umemwambia yanao thamani ya 3.5 biln. haya tuambie ww kipi kingne chakuongezea ambacho inacho simba kitazidi 40bln kama thamani ya klabu nzima? Manake 20biln ni 51%.
Af hisa za klabu haziez wekwa kwenye soko huria zikagombaniwa sabab mnunua hisa lazma awe mwanachama na mpenz wa simba kwaio kama yuko mwanachama mwingne anayeona nusu ya thamani ya simba ni zaidi ya 20biln na yeye aje na hela zake ashindane na Mo lakini sio kuja kupinga tu na maneno matupu.
 
MO ametumia chance kwakuwa wanachama wako desperate kutokana na matokeo mabovu miaka ya karibuni,Nafikiri MO alipaswa kusisitiza kubadili mfumo wa uendeshaji ambao ungempa kila mwanachama nafasi lakini kitendo cha yeye ku-propose apewe 51% ndio kinatia shaka na kitendo cha kuwatia pressure viongozi kuwa mchakato ufanyike ndani ya miezi 3
Mo ndo kawaamsha watu usingizini kaja na io proposal mwanachama gan mwingne alkua na ilo wazo? Kwaio ww unataka timu iachwe bila hela na matokeo mabovu kama saiv
 
.....wewe ndugu ndio ninakuelewa sasa!, kumbe wewe ni miongoni mwa kina Aveva mnaotaka simba iendelee kubaki hapa ilipo!, sijui mnafaidika na nini?!

Yaani yote "MO" aliyozungumza mnaona hana anachofanya!, hii ndio roho typical ya mswahili!, mfukoni masikini hana kitu, lakini full mdomo, maneno mengiiii, mipango mingiii...!!!

Hili zoezi Simba wanatakiwa wawe on top of the game for what?!, hawana pesa za usajili, mishahara ya wachezaji shida (mnaila na njaa zenu!), uwanja wa mazoezi, everything ni shida!, halafu eti mtu anapayuka tu, hili zoezi linatakiwa liende taratibu!

Hiyo brand ya Simba imekuwepo miaka na miaka hapo, mmeifanyia nini zaidi ya kujinufaisha binafsi?!, hivi nikiwauliza maendeleo ya uwanja wa Bunju unaweza kunijibu!, siku zote biashara ni faida, hakuna asiejua. Bora uwe na mfanyabiashara anaejulikana wazi, kuliko kuwa na nyie "wafanyabiashara uchwara" mnaoitegemea klabu kujinufaisha!

Hata km hilo zoezi likienda kwa mwendo wa konokono unaoutaka ndio itakuwaje?, kwamba ipo siku mtapata pesa za usajili?, au mnataka kutuchelewesha tu muendelee kupiga dili!, huku timu ikiendelea kufanya vibaya km kawaida?!

Lazima mbadilike kulingana na wakati, msilazimishe mambo yabaki km yalivyo siku zote wakati maendeleo ya klabu ni mabovu, nahisi KUNA KITU UTAKUWA ULIKUWA UNAKITAFUTA SIMBA, HUU UJIO WA MO UMEKUHARIBIA DILI, katege sehemu nyingine!
Umeongea ukwel mkuu wote wanaompinga MO wanajua atawazibia mianya yao ya kuiibia club hela
 
Mimi nina maswali wadau mnisaidie:-

1. Simba ni ya nani? Nani anaiuza? Na atapata faida kiasi gani kwenye huo mchakato?

2. (Hili linaendana na nilo la 1), ikishatolewa hiyo 20bil, hela za kuiendesha timu zitatoka humo humo au hizo zinakuwa ni za manunuzi tu, hivyo mmiliki atakuja na hela nyingine ya kuendeshea timu?

3. Tumeambiwa 20bil ni kwa asilimia 51, je hiyo 49% inayobaki nani atamiliki? Atatoa hela equivalent au hizo share zitakazobaki zitakuwa na thamani tofauti?

4. (Hili linaendana na nilo la 3), ikitokea wanunuzi wakakosekana hisa zitakazobaki zitaenda wapi? Na mmiliki atabaki Mo peke yake?
Ntamsaidia kujibu no. 3...
Mo anasema yeye atamiliki 51% ya hisa, na Wanachama wa Simba watamiliki 49, alisema kila mwanachama wa Simba atamnunulia hisa ambapo jumla ya umiliki wao ni utakua 49%..

My take:
Mimi naona wanachama wengi wakawaida wanataka timu auziwe Mo! Coz wao wanachotaka ni team ifanye vizuri wawe na furaha ili wawatambie Yanga, hicho ndo mwanachama wa kawaida anataka, na wengi hawajui kuwa Mo atawanunulia hisa ili wawe Wamiliki, wao wanataka team ishinde.....tatizo lipo kwenye Viongozi, kama team ikiuzwa Hawatapata cha juu toka kwenye usajiri, Makomandoo hawatapata pesa za milangoni n.k, Hawa ndo wananufaika na Simba.....naona Simba iuzwe tu coz ikianza kujiendesha kwa faida, wanachama watapata pesa kadri ya umiliki wao wa Hisa, kwani sasa wanapata nini? Hawana umiliki wa Hisa means hawaingizi chochote na wengi sasa wana magonjwa ya moyo kwa kufungwa na Yanga!
 
Hapana mkuu, leta ufafanuzi ndugu.
Asikutishe, eti "biashara za vilabu" biashara ni biashara, muuzaji anasepa na hela yake.

Hata Al Fayed alipoiuza Fulham, kachukua mkwanja wake wote. Hata yule nani, alieiuza Everton kwa mthailand, alichukua chake, akasepa.

Tuambieni. Kwa nini Mo ananunua Simba na bado anapanga matumizi ya pesa ambayo sio yake!
 
Iki kipindi cha miezi mitatu iliyopewa simba ifanye iyo tathmini ya thamani ya klabu af watamwambia kama wamekubali pendekezo lake la 20biln, ye mwenye kasema yale majengo ya simba uongozi umemwambia yanao thamani ya 3.5 biln. haya tuambie ww kipi kingne chakuongezea ambacho inacho simba kitazidi 40bln kama thamani ya klabu nzima? Manake 20biln ni 51%.

Mimi nafahamu industry ya real estate vizuri sana...Value ya hiyo Property ya Kariakoo is way above 10 Bn

Kuna Accounting for goodwill ya club ya simba...Argument ya MO ni kuwa Simba ni Loss earning entity kwa hio hata Goodwill valuation haitakuwa na significant amount....sawa it makes sense lakini sio kwa nature ya hizi timu simba na yanga...That would make sense kama angekuwa ananunua kampuni ya aina nyingine

Pia uongozi wamesema jingo lina thamani ya 3.5 Bn wametumia basis gani.....Ingekuwa busara wakawapa kazi hii Knight &Frank wakawafanyia valuation na hii isigharamiwe na MO.

My take:
Mimi naona wanachama wengi wakawaida wanataka timu auziwe Mo! Coz wao wanachotaka ni team ifanye vizuri wawe na furaha ili wawatambie Yanga, hicho ndo mwanachama wa kawaida anataka, na wengi hawajui kuwa Mo atawanunulia hisa ili wawe Wamiliki

Hapa sasa ndio maana kuna umuhimu wa wanachama kuelimishwa hadi waelewe decision wanayoifanya.......Ku exploit ignorance yao na Desperation yao kwa sasa sio busara........Mimi nimekutana na wanachama wengi tu...Ukiwauliza swali...Hivi itakuwaje endapo MO atakuja kushindwa kuiendesha timu ,tutafanyaje? Wanachama wengi watakujibu TUTAMNYANG'ANYA HISA Tulizompa........sasa watu wanaimba HISA HISA hawaelewi inamaanisha nini.......

Mimi na support sana hii process inayoendelea ....Lakini ningependa ifanyike pasipo upande wowote kujinufaisha na ujinga wa mwenzake
 
Unabadilisha mfumo halafu ndio unakaribisha watu wa kununua hisa au timu kamili.

Wanachama wa simba wamekubali kuibadili katiba yao ambayo ndiyo inasimamia muundo wa sasa wa uendeshaji kwenda kwenye Mfumo/muundo mwingine wa Kampuni....Ikishakuwa kampuni....then hizi transaction zingine zitaendelea.....lakini ikumbukwe ni process moja.

Wenye pesa wananunua mfumo au "business model" na si timu pekee- mfumo ni pamoja na mapato ya uwanjani yaani viingilio, mauzo ya jezi na vifaa au "merchandise", mauzo na manunuzi ya wachezaji na mapato yanayotokana na majengo au jengo

Haya unayoyasema yatafanyiwa tathimini ili kuweza ku ascertain price ya simba...Itabidi ifanyike hivyo

Kwa kuwa yupo mtaalam bwana Hans Pope

Huyo Hanspope sio Mtaalamu...tena huyu ndiye fisadi aliyeigharimu sana timu.......
 
Mo ndo kawaamsha watu usingizini kaja na io proposal mwanachama gan mwingne alkua na ilo wazo? Kwaio ww unataka timu iachwe bila hela na matokeo mabovu kama saiv

MO kaja ni hii proposal baada ya kuona timu inafanya vibaya na mashabiki/wapenzi/wanachama wameuchoka uongozi wa wa kina Aveva.MO alishakuwa mfadhili wa Simba enzi hizo na timu ilifanya vizuri wakati huo hakuleta hiyo proposal na hata angeileta wanachama wangekataa kwa sasa hawana ujanja kutokana na kunyanyaswa kwa muda mrefu na watani zao
 
Lakini mkuu pamoja na ukweli huo....Mfumo wa sasa wa vilabu vyetu hivi umeshachoka.....Tunakoelekea ni sahihi...cha msingi utaratibu ufuatwe
 
Lakini mkuu pamoja na ukweli huo....Mfumo wa sasa wa vilabu vyetu hivi umeshachoka.....Tunakoelekea ni sahihi...cha msingi utaratibu ufuatwe

Sijakataa hilo but mimi sio muumini wa timu kumilikiwa na watu wachache,mabadiliko ya mfumo yalikuwa kuwashirikisha wanachama/wapenzi/mashabiki wengi zaidi kuliko ilivyo sasa.Hivi unajua hata wanachama waliohudhuria hicho kikao cha maamuzi hawakufika hata 3000 ?
Na sikubaliani kabisa na yeye kupewa hisa 51% nafikiri umeona hata maoni ya Zitto amesema limit ya mwanachama kumiliki hisa isizidi 40%

Hapa Dar tu Simba/Yanga zingeweza kuwa na wanachama zaidi ya 100,000 na idea ya MO haina dalili ya kuongeza ushiriki wa wanachama yeye anataka process iende haraka ili apewe timu
 
Dah! Mwanangu ww mgumu kuelewa, hayo mambo yahisa nimambo yakitaalam hakuna kutapeliana huko
 
Sijakataa hilo but mimi sio muumini wa timu kumilikiwa na watu wachache,mabadiliko ya mfumo yalikuwa kuwashirikisha wanachama/wapenzi/mashabiki wengi zaidi kuliko ilivyo sasa.Hivi unajua hata wanachama waliohudhuria hicho kikao cha maamuzi hawakufika hata 3000 ?

Mkuu...sasa kila mkutano ili uweze kuendelea si unahitaji Quorum kutimia....Na kadri ya katiba ya Simba quorum ilitimia na kikao kikaendelea...

Kitu ambacho hujui hii timu ina mashabiki wengi na wanachama ni wachache...Jiulize why hata wewe sio mwanachama?

Kikao kilikuwa na mamlaka ya kupitisha maamuzi then

Pia nikuulize umetaja 3000,Je simba ina wanachama wangapi?

Na sikubaliani kabisa na yeye kupewa hisa 51% nafikiri umeona hata maoni ya Zitto amesema limit ya mwanachama kumiliki hisa isizidi 40%

Then toa argument zako kwanini hukubaliani na 51%...kwamba zito naye kasema....eeeeeeeeh....mkuu...Kwani zito ni Mungu...hayo ni maoni yake....make your own argument.

Hapa Dar tu Simba/Yanga zingeweza kuwa na wanachama zaidi ya 100,000 na idea ya MO haina dalili ya kuongeza ushiriki wa wanachama yeye anataka process iende haraka ili apewe timu

Ongea fact sio hisia.......Simba kama imeshindwa kwa miaka 80 kuwa na idadi hiyo itaweza lini na kwa miujiza gani?

Tuwe realistic.....Mfumo unaoutaka wewe wa kumilikiwa na watu weeengi unafaa sana kwenye timu za ndondo...za mchangani...Ila kwa Mpira wa sasa wa wa kibiashara unahitaji kuwa serious on business kama zifanyavyo timu nyingi

A good ccase ni TP mazembe....ilikuwa inamilikiwa na wanachama na haikuwa na kipya...baada ya kuchukuliwa na Moise...it is one of the best teams in Africa and world
 
Hatari ya kumpa mtu mmoja 51% ya shares ni hii hapa:

Hebu fikiria huyo mtu kama MO akaaga dunia (tena muda mfupi tu baada ya kumiliki 51%, siombei hayo yatokee lakini yanaweza kutokea kwa mwanadamu yeyote) na next of kin wake akarithi hiyo 51%, mrithi huyo akawa hana njozi za mpira kama mtangulizi wake hivyo akaamua kuuza hisa hizo kwa mtu yeyote mwenye pesa kama Manji, akaimiliki Simba kwa 51% na hivyo kuwa na say ya mwisho, naye Manji akaamua kuwaweka wachezaji pale Coco Beach wafanye beach soccer tu, wanachama wa Simba watakuwa na nini katika klabu yao? Hii ina apply pia kwa klabu yangu pendwa ya Yanga.

Sijatoa mawazo haya ku-discourage mabadiliko ndani ya Simba bali umakini mkubwa uwepo kuelekea kwenye mabadiliko hayo.
 
Anza wewe kujibu Mo amesemaje .... Auziwe timu
hivi vijana wa leo mkoje? MTU anapouliza sio kuwa hakumsikia mtu akisema ila hajaelewa! mimi nilichouliza hakiusian na Mo moja kwa moja nimeuliza ili kupata ufahamu in general, sasa sifahamu kwann umenijibu kifedhuri namna hiyo! sio kila MTU anajua haya mambo ya share holder ndugu yangu kama ungeoikua una akili timamu wala usingejisumbua kunijibu kama MTU uliyekurupushwa unajisaidia kichakani! TUHESHIMIANE
 
Ntamsaidia kujibu no. 3...
Mo anasema yeye atamiliki 51% ya hisa, na Wanachama wa Simba watamiliki 49, alisema kila mwanachama wa Simba atamnunulia hisa ambapo jumla ya umiliki wao ni utakua 49%..

My take:
Mimi naona wanachama wengi wakawaida wanataka timu auziwe Mo! Coz wao wanachotaka ni team ifanye vizuri wawe na furaha ili wawatambie Yanga, hicho ndo mwanachama wa kawaida anataka, na wengi hawajui kuwa Mo atawanunulia hisa ili wawe Wamiliki, wao wanataka team ishinde.....tatizo lipo kwenye Viongozi, kama team ikiuzwa Hawatapata cha juu toka kwenye usajiri, Makomandoo hawatapata pesa za milangoni n.k, Hawa ndo wananufaika na Simba.....naona Simba iuzwe tu coz ikianza kujiendesha kwa faida, wanachama watapata pesa kadri ya umiliki wao wa Hisa, kwani sasa wanapata nini? Hawana umiliki wa Hisa means hawaingizi chochote na wengi sasa wana magonjwa ya moyo kwa kufungwa na Yanga!

Hakika, pamoja sana mkuu.

Kilio chetu ni matokeo mazuri, na bila kuwa na hela hakuna siku tutakimbizana na Yanga au Azam kwa mpira wa sasa.
 
Hebu tuwekane sawa tofauti ya kuuza na Ku share holding !! maana tusije kutoka mishipa ya shingo ilihali hatujui tofauti ya maneno haya mawili au msambamba wake

Hicho ni kitu kimoja mkuu.
 
Mkuu una akili mno.

Jamaa hela kaizungusha inarudi mfukoni mwake kama 51%.

Kununua ni kama kawalipa waliokua wameshika hiyo 51% earlier akafanya buyout,hao watu wakashika mshiko wao 20Bil wakasepa,then akaanza kuwekeza kwenye timu afresh.

Jamaa hajanunua kitu,kapewa timu bure 51%,halafu hiyo 20B ni ya kuendeshea timu.

Infact naweza hisi Simba haikua na mmiliki,ilikua kama NGO/Association tu,nadhani Trustees walikua wanashika madaraka kwa niaba ya washika kadi.

Aisee jamaaa ana-close business of the century,kapewa timu bureeee!

Exactly my point, anachukua 51% ya umiliki bure, halafu ndo analeta hiyo 20bil ya kuendeshea timu, na wakati huo huo ana maamuzi juu ya matumizi ya hiyo fedha.
 
Back
Top Bottom