.....wewe ndugu ndio ninakuelewa sasa!, kumbe wewe ni miongoni mwa kina Aveva mnaotaka simba iendelee kubaki hapa ilipo!, sijui mnafaidika na nini?!
Yaani yote "MO" aliyozungumza mnaona hana anachofanya!, hii ndio roho typical ya mswahili!, mfukoni masikini hana kitu, lakini full mdomo, maneno mengiiii, mipango mingiii...!!!
Hili zoezi Simba wanatakiwa wawe on top of the game for what?!, hawana pesa za usajili, mishahara ya wachezaji shida (mnaila na njaa zenu!), uwanja wa mazoezi, everything ni shida!, halafu eti mtu anapayuka tu, hili zoezi linatakiwa liende taratibu!
Hiyo brand ya Simba imekuwepo miaka na miaka hapo, mmeifanyia nini zaidi ya kujinufaisha binafsi?!, hivi nikiwauliza maendeleo ya uwanja wa Bunju unaweza kunijibu!, siku zote biashara ni faida, hakuna asiejua. Bora uwe na mfanyabiashara anaejulikana wazi, kuliko kuwa na nyie "wafanyabiashara uchwara" mnaoitegemea klabu kujinufaisha!
Hata km hilo zoezi likienda kwa mwendo wa konokono unaoutaka ndio itakuwaje?, kwamba ipo siku mtapata pesa za usajili?, au mnataka kutuchelewesha tu muendelee kupiga dili!, huku timu ikiendelea kufanya vibaya km kawaida?!
Lazima mbadilike kulingana na wakati, msilazimishe mambo yabaki km yalivyo siku zote wakati maendeleo ya klabu ni mabovu, nahisi KUNA KITU UTAKUWA ULIKUWA UNAKITAFUTA SIMBA, HUU UJIO WA MO UMEKUHARIBIA DILI, katege sehemu nyingine!