Hatari ya kumpa mtu mmoja 51% ya shares ni hii hapa:
Hebu fikiria huyo mtu kama MO akaaga dunia (tena muda mfupi tu baada ya kumiliki 51%, siombei hayo yatokee lakini yanaweza kutokea kwa mwanadamu yeyote) na next of kin wake akarithi hiyo 51%, mrithi huyo akawa hana njozi za mpira kama mtangulizi wake hivyo akaamua kuuza hisa hizo kwa mtu yeyote mwenye pesa kama Manji, akaimiliki Simba kwa 51% na hivyo kuwa na say ya mwisho, naye Manji akaamua kuwaweka wachezaji pale Coco Beach wafanye beach soccer tu, wanachama wa Simba watakuwa na nini katika klabu yao? Hii ina apply pia kwa klabu yangu pendwa ya Yanga.
Sijatoa mawazo haya ku-discourage mabadiliko ndani ya Simba bali umakini mkubwa uwepo kuelekea kwenye mabadiliko hayo.