Mo afafanua ununuzi wake kwa Simba

katika zile milioni 400 za usajili wa wachezaji...hao wanachama wamechangia sh.ngapi?
 
katika zile milioni 400 za usajili wa wachezaji...hao wanachama wamechangia sh.ngapi?

Viongozi hawawashirikishi wanachama kuendesha klabu kama wangeshirikishwa wangechangia hata kama,ni kifogo.

Hivi unafahamu kuwa hela za mauzo ya Okwi ($300,000) zilifika mwaka huu ?


Unafikiri hizo mil 400 ndio zitamaliza matatizo ya Simba ?
Aveva amesema Simba inadaiwa karibu mil 800
 
kama viongozi wameshasema timu inadaiwa milion 800 kwa nini wanachama wasichange? Wanasubiri nini?
 
kama viongozi wameshasema timu inadaiwa milion 800 kwa nini wanachama wasichange? Wanasubiri nini?

Wachange bila kuambiwa ?
Kwa uongozi uliopo hata wanachama wakichanga zitaliwa tu,I hope umesikia sababu ya Aveva kukamatwa na Takukuru
 
amesahau au aliacha kwa makusudi kumuuliza kwanini aliiuza afrikan lyon, jibu ni rahisi afrikan lyon haikuwa na wapenzi hivyo alikuwa anapata hasara.ukishajua hilo ndio utajua kuwa mo kinachomsukuma sio mapenzi bali ni fursa ya kufanya biashara zake.
anasema yeye aliingia kwenya mpira kabla ya bakhresa na manji mwandishi kaonyesha ukilaza wake kwani miaka ya mwanzoni ya 80 bakhresa alikuwa anaifadhili simba na kuwapa ajira wachezaji wa simba ila yeye alikuwa hajitangazi kama mo hizo biliono 20 ni ndogo sana kwa hisa 51 zinaweza kuwa chini ya hisa kumi kama tathimini ikifanywa ya uhakika
 
Huyo mtu wa kununua Simba na kuifannya iwe Beach atakua mwendawazimu, mpira ni biashara Mzee!
 
Hivi unafahamu kuwa hela za mauzo ya Okwi ($300,000) zilifika mwaka huu ?

Mkuu hizo hela zimekuja na kina hanspope na aveva ...wamezikula...soma magazeti ya leo

Hizo pesa hazijaenda kulipa madeni.....otherwise watathibitisha mahakamani

Kimsingi....huu mfumo unaouona ni bora tumekuwa nao kwa miaka 80..ina maana miaka yote hiyo hakukuwa na kiongozi mshirikishaji?

Jibu ni rahisi...mfumo wa sasa unawanufaisha viongozi na kuwapa Room ya kutuibia full stop

Bora timu iwe kampuni imilikiwe kama duka la mtu
 
Huyo mtu wa kununua Simba na kuifannya iwe Beach atakua mwendawazimu, mpira ni biashara Mzee!
Hizo ndizo akili za mashabiki wa Yanga mkuu ..wala usiwashangae

Makoye Matale yeye hapo anadhani manji anaipendaaa saaaana yanga kuliko anavyopenda Pesa yake
 
Well said Mkuu! Na ndo maana Viongozi hawataki team iuzwe, ili waendelee kula, ntamshangaa shabiki wa kawaida wa Simba ambaye naye anapiga kelele team isiuzwe wakati hapati kitu, bora team iuzwe nao wawe Wamiliki kwa hizo hisa 49%, team ikianza kuingiza faida nao watapata chochote, kuliko sasa hupati kitu na team inafanya vibaya, maumivu Mara mbili! Huku viongozi wakijipoza kwa pesa kama za Okwi na Samatta!
 
Mwachieni muhindi timu.unajifanya una mapenzi sana na Simba hata kadi hulipii.mawazo ya kimaskini.timu kununuliwa na Mo wewe unapungukiwa na nini.kwani wewe unafaidika na nini unapoizimia sana Chelsea?mbona inamilikiwa
 
Mo mpaka sasa bado hajakabidhiwa simba, atakabidhiwa pale tu simba itakapo fanya marekebisho ya kwenda kwenye public company na hisa zikauzwa na yeye kasema hisa za simba zikiuzwa atakuwa tayari kutoa billioni 20 kwa ajili ya kununua hisa za asilimia 51 ili apate ile final say.Then hiyo 20 blns anaikopesha serikala after a while return itakayopatikana itasaidia kujengea vitega uchumi vya simba
 
SIMBA NA YANGA Tuachane kabisa na Matajiri hawa wenye mrengo wa CCM Au hata wa Vyama vingine vya Siasa... wote ni wapenzi na washabiki wa kutupwa wa CCM ..Tuachane kabisa kuuza timu au kukodisha hizi timu ambazo zinaunganisha Watanzania wote bila ya kujali tofauti za Kisiasa au Dini Kuna Hatari zake.
Nitakupeni Mfano wa wazi.
Kabla Ya Uchaguzi wa Kwanza wa Vyama vingi Kule Zanzibar Football ilipanda Juu sana. Timu za Zamani kama
Malindi
Miembeni
Vikokotoni
Kikwajuni
KMKM
Jamhuri

na zile Mpya kama
Small Simba
Black Fighters
Annur
Shangani nk


zilikua katika hali ya kiwango cha Juu na kuweza kutoa wachezaji wengi wazuri kwenye timu Ya Taifa Stars...
Malindi mwaka 1994 ilikua chini ya Mohammed Raza Na Naushad, Mwana CCM kINDAKI NDAKI...iliweza kusajili wchezaji wazuri na makocha wa nje. Ilifanikiwa Kuingia Fainali ya FA la Africa...
Baadhi ya Timu Hizi zimewahi kuchukua Ubigwa wa Tanzania Wakati ule Ligi ni Moja
Small Simba nayo ilikuwa chini ya Raza mdogo
nazo Timu za Shangani , Annur zilipata Ufadhili wa Matajiri wa CCM...Zote zilikuja Juu.
Ukaja Uchaguzi 1995 Na majimbo haya ambayo timu hizo zipo kwa bahati nzuri yaka chukuliwa na CUF.... Hawa wafadhili wakapata pressure na hatimae wakkaacha kufadhili hizi timu...Hatua Hii haikutarajiwa kabisa na hizi timu waliwaachia hawa wafadhili kila kitu ...hizi Timu zikafa kabisa na kushuka Daraja.. Hili likaleta athari kubwa ya Football Zanzibar. ..Kila Mtu atakubali kuwa hali ya Football zanzibar iko chini sana , imeanguka kweli kweli...Sasa hivi hakuna Small Simba wala Malindi wala Miembeni....Sasa hivi Mpira Zanzibar Unachezwa hivo hivo na Timu za Majeshi. Kuna
Mafunzo
Kmkm
JKU
Na Timu ya CCM Valantia au Green Guards....nao hawachezi mpira ..wanajitoa majasho tu kusukuma siku.

Hivyo Tusifanye Makosa hatua hizi zinaweza kuja angusha kabisa Mpira wa Tanzania. Siasa zetu bado sio zile zilizokomaa sana..
Tujifunze na Kusoma Ilikuwaje Simba..Ikagombana na Hatimae Ikagawanyika na Kuundwa RED STARS
Na ilikuwaje Yanga Ikavurugika na kugawanyika na Kuzaliwa PAN AFRICAN......
Pia someni Historia ya Cosmopolitan. Cosmo Ilikua Timu moja Kongwe zaidi na ilokuwa na ushawishi zaidi ya Simba na Yanga Miaka Ya nyuma. Ilikua na Uhusiano Maalum na Timu Kongwe ya Vikokotoni Zanzibar..Hizi Timu zote zilikua zikiongozwa na Ndugu wawili wa Kizanzibari Mansour Magram alikua Cosmo na Said Magram alikua Kocha wa Vikokotoni. Wakati huo huo Mzanzibari mwengine Abdalla Khalifa Salim ( Kinara) ndie alikua Rais wa Cosmo
Cosmo iliporomoka....Karume hakua anaipenda Vikokotoni Akaziwezesha Simba na Yanga....Cosmo Ikabaki kwenye vitabu vya historia.
Pia tusome Kisa na uhusiano wa Mwalimu na Tabu Mangara ..mara baada ya Ile Mechi Maarufu ya Yanga na Simba Kule Nyamagana Mwanza
Moja ya sababu ya migongano hiii ilikua ni Siasa......

HISTORIA NI MWALIMU MZURI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…