MO ashambuliwa mitandaoni na Wanasimba baada ya kumpigia Kampeni "Zungu" na Magufuli Simba Day

MO ashambuliwa mitandaoni na Wanasimba baada ya kumpigia Kampeni "Zungu" na Magufuli Simba Day

Tumsamehe alisema kiutani utani tu hata mimi ninaweza kumuombea kura bwana mkubwa lakini akigeuza tu lile komwe namng'ong'a tena ile kung'ong'a ya kutoa ulimi wote nje huku nikisindikiza na mikono
 
Wanasimba walichukizwa saana na kitendo alichokifanya MO jana wakati akimtambulisha mgeni rasmi aliyekuwa Mbunge wa Ilala Zungu kwa kuanza kumuombea kura uchaguzi ujao na baadae akaendelea kwa kusema Magufuli oyeee huku akiomba wananchi waendelee kumuamini Rais na kumpa kura tena mwaka huu.

Ghafla uwanja mzima ukapooza baada ya yeye kuongea huo upuuzi kuanzia jana usiku hadi mida hii kwenye mitandao mbali mbali kila akindika jambo( anapenda saana kupost Twitter & Instragam) amekuwa akishambuliwa sana hasa na mashahabiki kwa upuuzi alioufanya jana.

Funzo:
Anahitaji kuondoa kiburi, majigambo na kujikweza kwani mpaka sasa bado hajatimiza masharti ya kumiliki Club wanachama wanaweza ichukua muda wowote.
Wanachama wa Simba ni maskini watupu hawana uwezo wa kuendesha timu ndio maana hisa zao 49% wamemuuzia Mo.

Hisa 51% zinazobaki ni mali ya CCM usisahau hilo bwashee!
 
Simba mna control-iwa sana na jamaa. Mnachokijadili hapa kwake ni mafanikio. Bado kununuliwa tu na nyie kwa bei ya hasara. Wakti utazungumza.
 
Wanasimba walichukizwa saana na kitendo alichokifanya MO jana wakati akimtambulisha mgeni rasmi aliyekuwa Mbunge wa Ilala Zungu kwa kuanza kumuombea kura uchaguzi ujao na baadae akaendelea kwa kusema Magufuli oyeee huku akiomba wananchi waendelee kumuamini Rais na kumpa kura tena mwaka huu.

Ghafla uwanja mzima ukapooza baada ya yeye kuongea huo upuuzi kuanzia jana usiku hadi mida hii kwenye mitandao mbali mbali kila akindika jambo( anapenda saana kupost Twitter & Instragam) amekuwa akishambuliwa sana hasa na mashahabiki kwa upuuzi alioufanya jana.

Funzo:
Anahitaji kuondoa kiburi, majigambo na kujikweza kwani mpaka sasa bado hajatimiza masharti ya kumiliki Club wanachama wanaweza ichukua muda wowote.

Kuna mtu kwenye Simba day alikuwa ametumia kilevi
 
Nimeshangaa watu humu ni wanachama wa vilabu lakini hawaelewi hata thamani yake inapatikanaje. Alichokifanya Mo ni kurasimisha njia za mapato ya klabu tu, baada ya mfumo wa awali kuwa na tobo kubwa na hivyo kushindwa kudhibiti mapato. Hili ndilo tatizo hata kwenye timu ya Yanga pia. Lakini ni kutokuelewa kusema kwamba timu hizi ni maskini kiasi kwamba haziwezi kulipa mishahara. Yaani kuna watu wanaamini mishahara inatoka mfukoni mwa Mo? Basi kama ndivyo Mo na GSM si wafanya biashara kamwe.
 
Umetoa sh ngapi we mwanachama ?.

Yanga imewashinda na uanachama mnateseka na GSM, tuachieni MO wetu aongee anacho taka simba next level.
 
Tumsamehe alisema kiutani utani tu hata mimi ninaweza kumuombea kura bwana mkubwa lakini akigeuza tu lile komwe namng'ong'a tena ile kung'ong'a ya kutoa ulimi wote nje huku nikisindikiza na mikono
Weka picha ama katuni, tuone jinsi inavyokuwa ili tucheke sana!
 
Watamuua Mo walimwengu. [emoji16]
FB_IMG_1598179664760.jpg
 
Kwa nini uanze na point kwamba wewe ni mwanachama wa Simba?

Andika tu maoni yako bila kutaja hivyo, utaeleweka.

Maana najua kama ni swala la uanachama huna sifa hizo, labda useme wewe ni mshabiki wa Simba.
Hua siku zote mtu akishaanza sema mimi ni fulani ila..... hua simuamini kabisa
 
Huyo Mo pamoja na Haji wajirekebishe kutaka kuingiza serikali katika michezo na kuanza kupiga debe mtu mwenye akili timamu hawezi kumwombea kura Nzungu kwa kusema huyu ni mwenzetu hivi anafikiri Zungu anaweza kushinda kwa kura za simba tu yeye aweke b20 sio kupoteza lengo
 
Huyu Mo kashindwa kujaza uwanja wa pili kama alivyotuaminisha sasa amebaki kumpigia debe Zungu asipoangalia atamharibia shauri huyu mwenzetu Gabachori ni Gabachori tu yeye anafaidi sana Simba kuliko Simba inavyofaidi kutoka kwake kwa kusajili wachezaji wazee halafu ujifananishe na Al Ahly
 
Back
Top Bottom