MO ashambuliwa mitandaoni na Wanasimba baada ya kumpigia Kampeni "Zungu" na Magufuli Simba Day

Tumsamehe alisema kiutani utani tu hata mimi ninaweza kumuombea kura bwana mkubwa lakini akigeuza tu lile komwe namng'ong'a tena ile kung'ong'a ya kutoa ulimi wote nje huku nikisindikiza na mikono
 
Wanachama wa Simba ni maskini watupu hawana uwezo wa kuendesha timu ndio maana hisa zao 49% wamemuuzia Mo.

Hisa 51% zinazobaki ni mali ya CCM usisahau hilo bwashee!
 
Simba mna control-iwa sana na jamaa. Mnachokijadili hapa kwake ni mafanikio. Bado kununuliwa tu na nyie kwa bei ya hasara. Wakti utazungumza.
 

Kuna mtu kwenye Simba day alikuwa ametumia kilevi
 
Nimeshangaa watu humu ni wanachama wa vilabu lakini hawaelewi hata thamani yake inapatikanaje. Alichokifanya Mo ni kurasimisha njia za mapato ya klabu tu, baada ya mfumo wa awali kuwa na tobo kubwa na hivyo kushindwa kudhibiti mapato. Hili ndilo tatizo hata kwenye timu ya Yanga pia. Lakini ni kutokuelewa kusema kwamba timu hizi ni maskini kiasi kwamba haziwezi kulipa mishahara. Yaani kuna watu wanaamini mishahara inatoka mfukoni mwa Mo? Basi kama ndivyo Mo na GSM si wafanya biashara kamwe.
 
Umetoa sh ngapi we mwanachama ?.

Yanga imewashinda na uanachama mnateseka na GSM, tuachieni MO wetu aongee anacho taka simba next level.
 
Kanjibai jana kichwa ilikua moto sana, bila shaka alitumia vitu vya ziada tumchukulie vile vile alivokua kwa wakati ule.
 
Tumsamehe alisema kiutani utani tu hata mimi ninaweza kumuombea kura bwana mkubwa lakini akigeuza tu lile komwe namng'ong'a tena ile kung'ong'a ya kutoa ulimi wote nje huku nikisindikiza na mikono
Weka picha ama katuni, tuone jinsi inavyokuwa ili tucheke sana!
 
Kwa nini uanze na point kwamba wewe ni mwanachama wa Simba?

Andika tu maoni yako bila kutaja hivyo, utaeleweka.

Maana najua kama ni swala la uanachama huna sifa hizo, labda useme wewe ni mshabiki wa Simba.
Hua siku zote mtu akishaanza sema mimi ni fulani ila..... hua simuamini kabisa
 
Huyo Mo pamoja na Haji wajirekebishe kutaka kuingiza serikali katika michezo na kuanza kupiga debe mtu mwenye akili timamu hawezi kumwombea kura Nzungu kwa kusema huyu ni mwenzetu hivi anafikiri Zungu anaweza kushinda kwa kura za simba tu yeye aweke b20 sio kupoteza lengo
 
Mshamba sana jamaa kaharibu maana nzima ya simba day
 
Huyu Mo kashindwa kujaza uwanja wa pili kama alivyotuaminisha sasa amebaki kumpigia debe Zungu asipoangalia atamharibia shauri huyu mwenzetu Gabachori ni Gabachori tu yeye anafaidi sana Simba kuliko Simba inavyofaidi kutoka kwake kwa kusajili wachezaji wazee halafu ujifananishe na Al Ahly
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…