Mo aweka 500milion Simba akishinda ingawa hata yeye anajua tu haiwezekani

Mo aweka 500milion Simba akishinda ingawa hata yeye anajua tu haiwezekani

Ukiwaaminisha watu kwamba una pesa, hata Kama Ni vijisenti vya michongo utapata heshima Sana mtaani.
Ngoja nisiongee Sana maana Bei ya mawakili iko juu Sana.
Kwamba Kuna umchongo [emoji23]
 
Habari wakuu

Rais wa heshima na Mwekezaji wa klabu ya Simba SC Mohammed Dewji Maarufu ‘MO’ ameweka ahadi nono kwa wachezaji na benchi la ufundi endapo wataweza kufuzu kwenda hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu 2023-20 24.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’amesema motisha imetolewa ni kubwa hivyo ni jukumu la wachezaji kujituma na kupata matokeo katika mchezo huo.

Je tajiri anatuzuga...au yupo serious....???
Au Kwa vile anajua hili ni impossible [emoji23][emoji23] Kwa makolo kushinda View attachment 2953408
500m kwa Mo kuipa Simba siyo tatizo kabisa, ila sasa mpokeaji ndiye hajulikani vizuri.
 
Huyo Mo naye mzinguaji sana. Kwenye usajili anasajili washambuliaji wa bei rahisi wa milioni 100 halafu huku kwenda nusu fainali anajua kabisa hao wachezaji wa bei rahisi hawawezi vuka labda utokee muujiza kama wa ngamia kupita kwenye tundu ya sindano anajitia kutoa ahadi ya milioni 500 kama sio uhuni ni nini hiyo. Mo aambiwe ukweli aache hizo ahadi hewa aweke pesa kwenye usajili wa maana ili izalishe pesa mbele ya safari.

Wapenzi, mashabiki na wanachama wa Simba safari hii wasimuache kabisa huyo Mo. Hiyo milioni 500 aliyotoa ahadi ikitokea timu haijafuzu kwenda nusu fainali basi alazimishwe amkabidhi kocha Benchika alete mwenyewe mshambuliaji wa milioni 500 anayemfaa fullstop. Hili likifanyika basi huu utapeli tapeli kwenye mpira na kucheza na akili za watu wazima na kuwageuza watoto utaisha kabisa.
 
hamasa muhimu na ya maana sana hii [emoji205]
Kila la kheri Simba huko Cairo
Simba kuingia kwa MO waliingia choo cha kike. Huyu mtapeli ana uhakika Simba kafika mwisho ndio anatoa ahadi kuwalaghai wajinga. Nadhani wanaSimba wameshashtuka. Kufuzu hatua ya makundi hakuahidi wala hakutoa zawadi yoyote. Kuingia robo fainali hakuahidi wala kutoa chochote. Kuchukua Ngao ya Jamii au Hisani hakuahidi wala kutoa zawadi yoyote. Bado ni mfadhili? Badala yake anafadhili posts kwenye social media kumpiga vita Mwenyekiti aliyechaguliwa na wanachama Bwana Mangungu
 
Back
Top Bottom