Mo Bamba NBA sasa sio tena Hasheem Thabeet

Na uzuri na mimi nimezungumzia wanamichezo ambao jamii ilikuwa na matarajio makubwa kwao, na baadaye kushindwa kufikia hayo matarajio!

Hasheem Thabit na huyo dogo ni mifano halisi. Wala sina shida binafsi na yeye. Nimewalinganisha tu.
💯
 
Mchezaji gumzo duniani Kwa sasa anaitwa Victor Wembanyama ana asili ya Congo lakini mfaransa...watu wanadai anaenda kuwa star kuliko LeBron mwakani ... NBA ...wanamsubiri Kwa hamu..
Yeah huyo dogo lazima awepo kwenye draft ya mwaka huu. Sema ma scout wanadai weakness yake ni wembamba, dogo hana msuli.
 
Hili suala la kuwasakama wachezaji kucheza na kufanya vizuri uko nje Ajibu alishaliweka vizuri kabisa. Kama kwenda marekani au ulaya ni rahisi basi kupitia shughuli yako iyo iyo nenda wewe. Ulaya kuna wahasibu, madokta, wajasiriamali, madereva, wapishi n.k kama kwenda uko ni rahisi nenda kafanye shunghuli zako wewe sio lazima waende uko wanamichezo tu
 
Comment yako kama ina mashiko kaka, hata pale makongo kipindi icho alikua amateur's sana it was just for fun kwake.
 
Hasheem yuko china Sichuan🏀 blue 🐋

Anazisukumia tango pori papuchi za kishuanshuu!
Helaaaa mzeee watu wanaangalia penye hela sio umaarufu na title hata CR7 kaenda kucheza kule kwa waarabu sababu ya hela, David Beckham nae alienda kucheza ligi ya Marekani sababu ni helaaaa, Thabit anasaka Doe anadunduliza hizo hizo za Shuanhu akirudi hapa anafungua shule ya kikapu ndio utajua alienda kufanya nini China
 
Hasheem kilichomponza ni sketi na kulewa sifa. Over! Angekua mbali sana
 
Tatizo basketball ya bongo ilikuwa ni aidha walikuwa mabishoo wengi warefu lakini hamna kikapu ndio wanacheza, au wale wako serious tatizo walikuwa wafupi, Bahati, Evarist,
Pazi na Vijana wameshakufa siku hizi, na pia wao hawajawahi kushinda chochote nje, wala wakiwa timu ya taifa.
 

Nigeria, Senegal na Angola ndio timu bora za muda wote za kikapu kwa Afrika...
 
Tulikua na dogo patrick nyembela hapo bongo kapigana sana na kikapu cha bongo nafkiri hata hashim thabit kapita kwake na madogo wengi wa kishua wenye ndoto hizo wamepita kwake pale viwanjani tanesco ila hamna aliyetoboa zaidi ya hashim.
Nasemaje watoto wa kishua ndio walikua na mawazo ya kucheza basket,uswazi kwetu daladala camp gereji mchangani ni chandimu na kuwaza kuiba maandazi badae wapige chabo wapi na kupora ndio kipaji akitoboa anakua mpiga debe
 
Yeah huyo dogo lazima awepo kwenye draft ya mwaka huu. Sema ma scout wanadai weakness yake ni wembamba, dogo hana msuli.
sasa huyo mumfananishe na Le Bron James?ni mbingu na ardhi Le bron hajafika hapo alipo kimzahamzaha kapigana sana na hiyo game.
na swala la msuli unatafutwa aanzie huko kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…