Mo Dewj asema atazungumza na Wana Simba Instagram ili Wafanye usajili wa kishindo

Mo Dewj asema atazungumza na Wana Simba Instagram ili Wafanye usajili wa kishindo

Mmiliki wa klabu ya Simba ndugu Mohamed Dewji amesema ya kwamba atazungumza na wanasimba instagram live ili wamueleze changamoto za klabu yao ikiwemo wachezaji gani wafukuzwe katika klabu ya Simba..

Pia amewaomba wanasimba waandae majina ya wachezaji wanaoona wanafaa ili awasajili dirisha lijalo la usaji..

Kwako mwana Simba je unapendekeza nani afukuzwe na nani asajiliwe?
Anacheka cheka
 
Sisi tunataka tarehe 20-4-2024 tushinde wengine hatuko Instagram
 
That's not the way uongozi na usimamizi wa club au kampuni unavyofanyika ulimwengu wa corporates. Huyu ni mwehu au anawachezea akili simba fans and members. Mkikubali imekula kwenu.

Mambo ya kiutawala yanaendeshwa kiofisi sio kiholela namna hiyo otherwise angeitisha extra ordinary meeting wayajadili huko sio kuendesha team kwa mitandao.

Je mna uhakika gani hayo maoni yatatokana na simba fans and members wa kweli? Mnaingizwa chaka kweupe msikubalii huu ujinga wa gabachori kama ameshindwa kusimamia team awape wadau wengine.

Otherwise tukutane tarehe 20 ndio mtaamua muendeshe team kwenye mitandao au kiofisi.
 
Nimeangalia "clip" ya MO nimejiridhisha kuwa katika matatizo makubwa iliyonayo Simba basi Mo ni jipu namba moja linalohitaji kutumbuliwa tena haraka sana. Toka lini mashabiki wenye uwezo na uelewa tofauti wakafanya kazi ya kitaalamu ya kusajili na kutimua wachezaji? Je kazi ya benchi la ufundi, kamati ya ufundi, kamati ya usajili, skauti mzungu na bodi ya Simba ni nini juu ya usajili wa wachezaji pale Simba? Vipi kwa wachezaji watakuwa na hali gani watakapokuwa wanadhalilishwa " live" kwenye instragam. Je huko mbele ya safari kuna mchezaji anayejielewa atakubali kuja kuchezea timu inayodhalilisha wachezaji wake mitandaoni.

Aliye karibu na MO amwambie aache huo upuuzi badala yake awape " scout team" pesa ya kusajili wachezaji wa maana. Pia mkumbusheni kuwa ubahili wake wa kutoa pesa kiduchu ndio tatizo la kupata wachezaji wa hovyo kama wakina Babcar Sarr, Freddy na Jobe. Mo asifikiri kuwa watu wote kwenye hii nchi hawana kumbu kumbu kuwa alitajiwa bei ya Shabani Juma, Manzoki, Aucho, Aziz Ki, kwa kuwataja wachache tu akakimbia mbio wenzake wakajitosa na mafanikio yanaonekana. Tena hata Manzoki Yanga walikuwa tayari kulipa TZS 400M alizokuwa anaomba apunguziwe lakini Manzoki mwenyewe akachomoa na nafikiri huko alipo anajuta kuwasilikiza Simba.

Mo aambiwe wazi yeye ndiye aliyemweka Try Again tena kinyume na katiba ya Simba. Tangu amwachie timu Try Again ndio shida ilipoanzia hapo kwani vikombe vyote vimeondoka Simba kuacha ngao ya hisani iliyopatikana kimagumashi kule Tanga. Mo aulizwe kwa nini makocha wakiboronga huwa anawatimua fasta lakini Try Again hajamtimua mpaka sasa? Kuna nini nyuma yake? Kwa nini anapindisha mjadala badala ya kuwa kuwaondoa viongozi walioshindwa kuingoza Simba akiwemo Try Again aliyemweka yeye na kuufanya uelekee kuwalaumu wachezaji na kujifanya atafanya usajili mzuri?

Ni mtizamo tu.
 
Mmiliki wa klabu ya Simba ndugu Mohamed Dewji amesema ya kwamba atazungumza na wanasimba instagram live ili wamueleze changamoto za klabu yao ikiwemo wachezaji gani wafukuzwe katika klabu ya Simba..

Pia amewaomba wanasimba waandae majina ya wachezaji wanaoona wanafaa ili awasajili dirisha lijalo la usaji..

Kwako mwana Simba je unapendekeza nani afukuzwe na nani asajiliwe?
Huyu jamaa ameshaona kuwa akili za Wanasimba ni kama vitenesi tu.
Accounts za Wanasimba ni verified? Mambo ya kuamuliwa na tachnical bench anataka yajadiliwe na kuamuliwa na Mashabiki, au michuano ya Soka sasa hivi matokeo yake hupatikana kwa kupiga kura mitandaoni kama Musics Awards?
Simba hawana platforms za kuweza kujadili mambo yao na kuyafanyia maamuzi mpaka wakafanyia Instagram? Key people wote wa Simba wana Instagram accounts? Hawana uongozi? Hivi anawachukulisje mashabiki wa Simba?
Hawezi kuipa Simba umuhimu inayostahili kwa kuwapa heshima ya kuitisha mkutano hadi aamue kufanyia Instagram?
 
Mmiliki wa klabu ya Simba ndugu Mohamed Dewji amesema ya kwamba atazungumza na wanasimba instagram live ili wamueleze changamoto za klabu yao ikiwemo wachezaji gani wafukuzwe katika klabu ya Simba..

Pia amewaomba wanasimba waandae majina ya wachezaji wanaoona wanafaa ili awasajili dirisha lijalo la usaji..

Kwako mwana Simba je unapendekeza nani afukuzwe na nani asajiliwe?
Ameona wanachama na mashabiki wanamzonga, kawa mpole.
 
Back
Top Bottom