Mo Dewji aendelea kukimbiza kwa utajiri nchini

Mo Dewji aendelea kukimbiza kwa utajiri nchini

Wachaga ni kabila pekee lilitoa bilionea na kuingia kwenye orodha za Forbes, hao wengine ni wahindi wabantu
Acha uongo....

Kulikuwepo na muhaya pia...

Hebu fuatilia billionaire Ally mfuruki....alishawahi kuwa top ten pia...ingawa naye alishakufa...
 
Mengi anakuwaje tajiri wakati mali zake zimegawanyishwa kufuatia mirathi yake "will".
 
Waache uongo, ko miaka yote utajiri wao uko palepale uku maviwanda yao yanapiga kazi kila siku
 
Sisi masikini tunachojua ni chuki dhidi ya waliofanikiwa/matajiri.Utakuta mtu anaanzisha mada "Sielewi utajiri wa mo chupri chupri,ni janjajanja tu" ..wakati huo jumapili hii anafua nguo Kisha anaanika kamba ya jirani na vibanio anaiba wakati vinauzwa buku tu.
Saguda47 amelike
 
Habari wakuu,

Mohammed Ghulam Dewji, ameendelea kuwa top kwenye suala zima la utajiri nchini Tanzania. Licha ya bilionea huyo kuchukuliwa poa nchini ila ndio bilionea no.1 kijana barani Afrika na anashikilia no.15 kati ya mabilionea wote Afrika kutokana na taarifa za Forbes na Bloomberg.

Mo Dewji ni tajiri pekee Tanzania aliefikia utajiri wa thamani ya dollar bilioni 1.5 na hakuna Mtanzania yeyote aliewahi kufikia kiwango hicho. Pia ni bilionea pekee wa kitanzania mwenye biography kwenye jarida la Bloomberg, zaidi ya huyo hakuna bilionea mwingine alieongelewa au kutajwa na jarida hilo.

Kwa upande mwingine bilionea Rostam Aziz ameshikilia no.2 kwa mabilionea nchini kwa utajiri wa thamani ya $900M, huku mwakilishi wa wachaga Marehemu Mhe.Reginald Mengi akishika no.3 kwa utajiri wa $680M, Said Salim Bakhresa akifuata kwa kuwa na utajiri wa $600M.
Nitakiwa mtu wa mwisho kabisa duniani, kuamini eti Mohamed Dewji ni tajiri mwenye pesa nyingi zaidi kuliko Rostam Aziz, au Said Salim Bakhresa.
 
Nitakiwa mtu wa mwisho kabisa duniani, kuamini eti Mohamed Dewji ni tajiri mwenye pesa nyingi zaidi kuliko Rostam Aziz, au Said Salim Bakhresa.
We unajulikana, unaweza ukasema gari imetengenezwa kwa mbao na ukasimamia msimamo wako
 
Unafuatilia kweli data za matajiri!!!?? Mara ya mwisho forbes uliingia lini ukaona Mengi hayupo!!?? Kanywe chai urudi uje kuniambia nani amekwambia bilionea akifa anaondolewa kwenye orodha ya matajiri. Maana naona hujanywa chai
Sasa marehemu anakuwa vipi tajiri ikiwa mali zake huku duniani wameshagawana?
 
Back
Top Bottom