MO Dewji akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa FIFA Gianni Infantino, amkabidhi jezi ya Simba SC

MO Dewji akutana na kufanya mazungumzo na Rais wa FIFA Gianni Infantino, amkabidhi jezi ya Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC Mohammed Dewji 'MO' amekutana na kuzungumza na Rais wa Shirikisho la Soka duniani FIFA Gianni Infantino kuhusu masuala ya maendeleo ya mpira wa miguu hususan barani Afrika.

Baada ya mazungumzo hayo MO Dewji amemkabidhi jezi ya Simba SC ambayo imeandikwa jina la Rais huyo wa FIFA Infantino.

"Leo nimekutana na Gianni Infantino Rais wa FIFA katika makao makuu, kwa kweli nimefurahishwa sana, kwa dira na shauku ya kuendeleza mpira wa ushindani na wa kuvutia Afrika.

Nia yao ni kuboresha maendeleo ya mpira, na najua chini ya uongozi wa Gianni mpira wa miguu kwenye bara letu utaenda Next Level". MO Dewji.

IMG_20200128_142708_581.jpeg
FB_IMG_1580210607252.jpeg
FB_IMG_1580210619404.jpeg

 
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.. hatimaye jezi ya Mnyama Mkali yamfikia mwenye mpira wake huku huku aliko.

Huu ni uthibitisho wa ubora na thamani ya klabu yetu ya Simba SC.
Ndio mwenye mpira wake anapokea jezi ya timu yoyote ile bila kujali ni timu ya kiwango gani. Je tutegemea simba kufaidika na vitu gani baada ya ziara hiyo Mo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
jizi hilo lililo taka kumhonga kabwili IST, limeisha inunua simba na wanachama + washabiki wootee na 'kuwatia' mfukoni mwake, mikia woote kwisha habari yenu
 
Kwahivyo alikataa IST, lakini alikubali hongo la Kagere?

jizi hilo lililo taka kumhonga kabwili IST, limeisha inunua simba na wanachama + washabiki wootee na 'kuwatia' mfukoni mwake, mikia woote kwisha habari yenu
 
Back
Top Bottom