Mo Dewji: Amekuwa akinitukana, nimemsamehe sina kinyongo na Haji Manara

Mo Dewji: Amekuwa akinitukana, nimemsamehe sina kinyongo na Haji Manara

Tatizo ni Waandishi wetu, aina ya Maswali wanayouliza lazima yalete majibu ya UKAKASI na haswa ukichanganya na asili ya lugha ya Kiswahili bila umbeya HAKINOGI.

Nakumbuka wakati SENZO MBATHA akijiuzulu SIMBA , MO DEWJI alielezea kuwa jamaa amepata malisho BORA , huko kwao SOUTH AFRICA na anamtakia kila la kheri na wamefanya kazi naye vzr.

Baada ya kutambua kuwa SENZO kahamia kwa WANANCHI alipofuatwa na waandishi wa hbr majibu yake yalikuwa tofauti.

" Huyu SENZO , ameshindwa kufikia malengo ya klabu ,hivyo alitambua kuwa HATUTAMUONGEZEA kipindi kingine"

Waandishi haohao wakarudi kwa SENZO na kujielezea yote aliyotamka MO. juu yake. Lkn SENZO alichowajibu " kama , kawaambia hivyo, atakuwa HAJASEMA KWELI, mwambieni afungue makabrasha yake awaoneshe kazi nilizotakiwa kufanya na nilizofanya" na alichowaambia siyo taratibu sahihi za kiofisi ( kuharibu sifa za kiutendaji za mtu)

Waandishi hao hao wakarudi mbio kwa MO na kuanza kumuuliza tena suala la SENZO safari hii MO akajiongeza kidogo na kuwaambia wale WAANDISHI hapana sasa huu utakuwa mchezo ,nikiwaambia mnaenda kwa Senzo na kuleta MALUMBANO.

Sasa hapa ligi imebaki kwa WASWAHILI kwa WASWAHILI na lugha yao ya UMBEA !! neno la KAWAIDA tu ,mnaloambiana kila siku lkn siku mkikosana hilohilo neno litaitwa TUSI.

Vibonzo vya kawaida vya soka au ujumbe wowote wa utani wa soka UTASEMA ananilenga mimi, WAANDISHI nao maswali yao ndo YANAPITIA humohumo.

Kauli ya MWISHO ,pale WASAFI FM tajiri MO akiwa na HAJI MANARA , alitamka wazi kuwa HAJI WANAMPENDA na hawana tatizo naye.
Lkn kumbe ulikuwa ni KISWAHILI CHA WASWAHILI haikupita mwezi.
 
MO kuambiwa kwamba aonyeshe account aliyoweka 20B ndiyo kutukanwa? Mbona Kigwangala alimwambia hivyo hivyo lakini hakusema kama alimtumkana why kwa manara tu?
 
Katika hali ya kawaida huwezi mtu kujisifia kwa watu mimi mpole sana, mimi sina hichi wala kile ni kawaida mtu husifiwa na watu waliomzunguka kuwa fulani ni mpole sana, hajui kukasirika...... ndio maana hata sisi waislamu hatujawahi kuambiwa kuwa mtume wetu Mohammed(SAW) aliwahi kujisifia japo alikuwa mkamilifu kwa imani zetu ila sisi tunamsifia mpaka leo. Ogopa binadamu anayejisifia tabia na kwa bahati mbaya Mo anatabia hizo na hata Hajji ana tabia hizo ujuwe wote ni fake. Kwa hili Mo kwa level yake ni bora angekaa kimya halafu angeongea positive tu kuhusu Hajji watu wangempa sifa automatic sio kujisifia mimi sina wivu, mimi sikasiriki, mimi bla bla mimi blala...ujinga tu
 
Manara ni kama mbwa koko, anabweka kweli kweli akiwa kwao au ndani ya fensi.
 
Hivi mbona sijawahi kusikia GSM kwenye media zaidi ya kumuona uwanjani akitabasamu tu?

Huyu Mo ni tajiri gani mswahili mswahili hivi?

Hivi Billionaire Mo mtu wa kumjadiri chizi kama Manara kweli?
 
Manara ni kama mbwa koko, anabweka kweli kweli akiwa kwao au ndani ya fensi.
Lakini siyo sahihi kwa Billionaire kama Mo kumjibu au kumjadiri Manara, hayo ni majukumu ya Chawa, kina Mwijaku wana kazi gani? Hao ndio level moja na Manara.
 
Kuwa mkubwa ni jalala, leading by example. Yeye kama mkubwa kiumri, kipesa na kimadaraka anapaswa kuonesha njia
Manara hafugiki,anaweza kumwita then yeye akakimbilia kwenye media.
Ogopa sana mtu anayependa kuonewa huruma na kuonekana anaonewa,wanajua sana kutengeneza matukio ili wajikweze
 
Hivi mbona sijawahi kusikia GSM kwenye media zaidi ya kumuona uwanjani akitabasamu tu?

Huyu Mo ni tajiri gani mswahili mswahili hivi?

Hivi Billionaire Mo mtu wa kumjadiri chizi kama Manara kweli?
Ameulizwa swali na mwashishi,je angekaa kimya ?
Swala la GSM kutokosikika kwenye media ni mapenzi yake
Bakhresa umemuona uwanjani mara ngapi ?
 
Hivi mbona sijawahi kusikia GSM kwenye media zaidi ya kumuona uwanjani akitabasamu tu?
Unawapangia watu style ya maisha? Elon Musk ni tajiri wa kutupwa, namba mbili duniani, lakini yupo sana kwenye nitandao ya kijamii, naye ni mswahili? GSM amechagua kutotokea huko, yawezekana kwa kupenda au kutopenda, wengi hatujui wala hatuna haja ya kumchagulia cha kufanya. Kuna mwanasiasa mmoja alisingiziwa kuandika kitu twitter, akasema hana akaunti wala hajui kutumia twitter. haya mambo yapo sana, unaweza ukaona mtu haonekani kule kumbe hajui kutumia
 
Back
Top Bottom