Mo Dewji amshauri Kocha Omog aachie ngazi, Simba yavunja naye Mkataba

Mo Dewji amshauri Kocha Omog aachie ngazi, Simba yavunja naye Mkataba

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
FB_IMG_1514037210356.jpg


Naungana na Mo Dewji,huyu kocha hawezi kuwa na kipya tena
---------

Baada ya SAA kadhaa kupita..

Klabu ya Simba na Kocha wake Mkuu Joseph Omog wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili

> Uongozi wa Simba SC umesema unamshukuru kocha Omog na kumtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba..
 
Inatakiwa mkae mezani mjadiliane sio kukimbilia mitandaoni tu.
Kujiuzuru ni kuvunja mkataba ina maana inakula kwake. Bosi Mo ampe stahiki zake ili ajiondokee awaachie litimu lenu butu mlilosajili kwa majina bila weredi.
 
Simba ni timu ya kelele bila weledi. Hangaikeni na hali zenu
 
Inawezekana Omog akawa in tatizo Simba, lakini nnachokiona Mimi tofauti sana.
Kama washabiki tumeamua kumtwisha zigo la ' Mavi ' kocha tu.
Mosi, Nafikiri ulifanyika usajili wa majina tu pale Simba kuliko kuangalia uhalisia. Mfano, unamuachaje Janvier Besala Bokungu kwaajili ya Ally Shomari au mchezaji ' majeruhi ' Kapombe?
Pili, wachezaji was Simba naona wanaamini kuwa wao ni ' wakubwa ' kuliko timu. Sioni timu ikiwa na spirit ya ushindi uwanjani, kifupi wachezaji ' hawajitumi ' kabisa. Most of them ni mizigo tu.
Faida ya kuwa na wachezaji wanaoitwa ' wazoefu ' ni ipi kama wanashindwa kusoma mbinu za timu ndogo kama ile ya Jana?
Ni ujinga na uwendawazimu kuendelea kumtupia lawama kocha pekee.
Nafikiri ' reform ' inahitajika hata kwa wachezaji wa Simba ambao ' tunaaminishwa ' eti wa mabilioni ya pesa.
Nawasilisha..!
 
Inatosha aisee! Hana mbinu mpya kwa wachezaji waliopo. Anapanga kwa kukariri. Zidane amebeba makombe matano lakini atatolewa mkuku. Omog hana hata kikombe cha kahawa alaf avumiliwe! Utakuwa uzwazwa huo.
Kwahiyo, Omog asepe Tu. Kwasababu ya matokeo ya Jana au kuna kingine?

Viongozi nao wanachangia
 
c2895081d5df660e391e37410a250191.jpg

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
*_____________________________________*
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.
Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.

Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho,na kupumzika siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara,ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo.

Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu. *Mwisho*
klabu inawatakia nyote Sikukuu njema ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.
IMETOLEWA NA.... *Haji S MANARA*
Mkuu wa Habari Simba Sc

*SIMBA NGUVU MOJA*
 
Back
Top Bottom