Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asubiri wamvunjie mkataba ajijazie mihelaHaji Manara alicho post jana sicho kizuri kwa kocha na tazama na kwa hili la Mo sijui Omog yupo kwenye hali gani sasa
Mkuu nimecheka sanaifike kipindi wachezaji wawe wanafukuzwa
mfano Benzema
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]Wamchukue kocha wa hao wajeda ndo afundishe simba
Sure mkuu. Pale Simba tuna ' mizigo ' tu.ifike kipindi wachezaji wawe wanafukuzwa
mfano Benzema
Timu za kiswahili,pia huendeshwa kiswahili swahili.Haji Manara alicho post jana sicho kizuri kwa kocha na tazama na kwa hili la Mo sijui Omog yupo kwenye hali gani sasa
![]()
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI*
*_____________________________________*
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.
Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.
Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho,na kupumzika siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara,ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo.
Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu. *Mwisho*
klabu inawatakia nyote Sikukuu njema ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.
IMETOLEWA NA.... *Haji S MANARA*
Mkuu wa Habari Simba Sc
*SIMBA NGUVU MOJA*