Mo Dewji amuomba msamaha Kigwangalla kwa kumnyima mkopo baada ya kuhojiwa uenyekiti wake Simba bila kukamilisha uwekezaji

Mo Dewji amuomba msamaha Kigwangalla kwa kumnyima mkopo baada ya kuhojiwa uenyekiti wake Simba bila kukamilisha uwekezaji

Kile chama chakavu hata akiingia malaika atakua mchafu tu.
Mama fwalaa sana naee yulee... yani fisiemu ukoo wa panyaa nilidhani samia na Majaliwa wanajielewa kumbe nao mumbwaaa tu...
 
Chuki ya kunyimwa mkopo inaweza tumika kufitinisha, bado mo naona yupo sawa kuwa watu wajue nyuma ya pazia, unajua simba kuna watu wameitoa mbali, asije mjinga mmoja akaharibu kigwangala ni mtu wa ajabu sana anapenda ligi
Nakubaliana na were. Washabiki wanataka kuona mpira tu. Kama tunavyoona Arsenal na MnaU na kuwashangilia wakati hatujaweka haya sent moja. Kwa Simba kuna wanasheria. Kama hili I hawakuliona huyu HK anajua nini?
 
Yeye Mo sio mkweli..
Anataka geuza Simba kama Mali yake binafsi
Hisa zake ni asilimia 49 Tu na hajalipa hiyo hela.


Watu wenye hisa hisa asilimia 51 wanayo haki ya kuuliza
Hawa wenye hisa 51% wameshalipa kiasi gani hadi sasa?
 
Juzi Kati Kwenye akaunti ya twitter Kigwangala alionekana akiwanadi ng'ombe wake

Kabla ya hapo alionekana jimboni kwake akigawa pikipiki kitu ambacho hajawahi kufanya kwa miaka ya nyuma kabla ya mwaka wa uchaguzi.

Leo kabwatuka kuhusu uteuzi uliofanywa na klabu ya Simba akidai taratibu hazijafuatwa.

Baadaye Mo Dewji anahoji kwanini asimpigie simu? Mwisho anamshauri asichukulie hasira kunyimwa mkopo wa bodaboda


========
Tundu Lissu kawavuruga MATAGA vibaya mnoo!
 
Niko tofauti kidogo Kigwa namkubali sana,na kwa hili la bilioni 20 za uwekezaji,hoja ipo na inatakiwa ijibiwe.Kwangu mpaka sasa Mo anapiga chenga.Haihitaji siasa tunataka mzigo uingie kwa akaunti za klabu.
 
Naona MO aligoma kutoa pikipiki za kuhonga wajumbe,Dewji anakopa Bank kwa kutumia assets zake kama dhamana(Collateral), yeye Kigwa anaomba mkopo kwa MO akiweka Dhamana ya kitu gani?

Kigwangala bana mara nalima maelfu ya ekari za mchele,mara nina ng'ombe maelfu, kila siku anaimba imba ooh vijana hawana ajira sababu they don't think out of the box kumbe yeye mwenyewe ombaomba tu.,mafao yake ya ubunge hataki kuyanunulia Pikipiki za wajumbe ila hela za MO ndio za kufanyia hayo.
Ndio ku think out of the box kwenyewe huko.
 
Vitu alivyohoji lazima tuangalie kilichomsukuma kuhoji, nimapenzi aliyonayo kwa Simba?. Au nikwasababu alinyimwa mkopo?. Baada yahapo tujiulize yeye anadai nimwanachama wasimba, kwa nini asisubiri vikao halali vya Simba ndio akahoji?. Tukishapata hayo majibu ndio tuje kwenye hoja zake.

Kabla yahapo aliuliza elimu ya CEO akaona imeshiba, akaimbia mjadala wa elimu akahamia kuwa ameshawahi kuongoza club yeyote kulinganisha na Senzo, akajibiwa hapana akapewa mifano ya Ma CEO waliotoka katika tasisi mbalimbali kuja kuongoza soka kwa Mara yakwanza na wakafanikiwa mmoja wao akiwa CEO wa Chelsea na CEO wa Liverpool.

Baada yahapo akahamia kwenye bill 20, hili lishazungumzwa sana na MO mwenyewe hata siku moja kabla ya Simba day alilizungumzia kama hakuridhika asubiri vikao halali vya Simba akaulize na atajibiwa.
Hili ndilo jibu...Leo Wasafi wameirudia ile sauti kwenye Interview ya Mo...kifupi Muheshimiwa Waziri amepuyanga...maana kwenye ile sauti Mo alisisitiza kuwa kuna watu chokonozi ndo wanajifanya hawataki kuelewa...halafu mmoja wa watangazaji(jina kapuni asije kutekwa) akasisitizia hiyo kauli ya watu chokonozi ambao wanjifanya hawataki kuelewa kinachoeleweka...Kigwa amejivua nguo..katibu wake kamuokoa
 
Hii nayo kali, huyu waziri sifa zimemjaa ndiyo maana akigombana na naibu waziri kwa tamaa zake na kujifanya wizara ni yake pekee sifa tu
Pamoja na sifa unazodai za Kigwa je Mo anadaiwa au hadaiwi kwa mujibu wa mkataba?
Yanayosemwa mtaani kwamba ni janja janja yaweza kuwa kweli amemhonga klabu PA wake!!!
Midhali timu bado inashinda kishika uchumba kinatosha ila mimba ikipevuka tutauona mtiti na ndipo tutajua yule "Mwenyekiti, Mzee Kilo na yule mama yetu" kwanini walinyamazishwa!!
Yetu macho na Mo Foundation
 
Pamoja na sifa unazodai za Kigwa je Mo anadaiwa au hadaiwi kwa mujibu wa mkataba?
Yanayosemwa mtaani kwamba ni janja janja yaweza kuwa kweli amemhonga klabu PA wake!!!
Midhali timu bado inashinda kishika uchumba kinatosha ila mimba ikipevuka tutauona mtiti na ndipo tutajua yule "Mwenyekiti, Mzee Kilo na yule mama yetu" kwanini walinyamazishwa!!
Yetu macho na Mo Foundation
Kwani wanachama na wapenzi wa Simba sport wanataka nini? I hope wanataka ushindi, mataji ili waweze kuwatambia watani zao. Hiyo ndiyo Big Satisfaction kwa wapenzi wa Simba. Kwani hata leo Simba Ingekuwa na akiba ya Tsh Trilioni 10, je wapenzi wangepata fedha hizo mfukoni mwao? La hasha.

Nani hajui Simba ilivyo STRUGGLE miaka 4 kabla ya Mo Dewji hajakuja Simba? Yanga na Azam ndiyo walikuwa wanabadilishana kwenye ubingwa wa Tanzania.

Mimi personnally naona mawazo ya Mo Dewji ni zaidi ya hizo Tsh 20 Bilion. Kwa kuwa tuna mwaka wa mfulizo na ubingwa wa Tanzania, tulifika robo faunali ya CAF Championship, tayari tuna uwanja wa mazoezi na unatumika Bunju. Tuna sajili wachezaji tunaowataka kutoka popote Afrika na wachezaji wetu wanalipwa bila usumbufu.

Ni MWANACHAMA gani leo ana uwezo wa kuyafanya haya just in case Mo Dewji anaondolewa Simba?
 
Nimefuatilia suala hili kuanzia huko Twitani na hata kwenye vijiwe vya kahawa na ni wazi kuna jambo ambalo halipo sawa kati ya Mo na Kigwa.Kidogo mwanga unaanza kuonekana lakini tuanze kwa kumuangalia Mo.Mo hakuingia Simba kwa mtutu wa bunduki lakini through taratibu za kisheria na mchakato wa muda mrefu.Hili linanipa nguvu ya kuwa maswali ya Kigwa yana evil motive behind kwani kama mtu msomi,waziri na mwanasimba alikuwa na njia nyingi za kulifanikisha hilo kuliko kulianzia twitter.Nimejaribu kuitafuta interview ya Mo alipofanya na Wasafi na kuna kipengele anachosema atawekezaje 20bn kwenye club ambayo rasilimali zake hazizidi 4bn?Hapo watu wenye utaalamu wa biashara watusaidie na pia wanasheria wapitie mkataba uliompa club.
Kigwa alikuwa na nia ya kuanzisha taharuki katika club kwani ni waziri na naamini hata akimuita Mo ofisini kwake angekuja tu.
Jambo hili limenikumbusha Marehemu Reginald Mengi na wafanyabiashara wa kihindi ambapo Mengi aliitisha mkutano na kudai anatishiwa maisha.Kikwete alilizungumza na kwa lugha ya kidiplomasia alimlaumu Mengi na kuuliza kuwa mbona Mengi hakumpigia hata simu wakati ana namba yake?The same kwa Kigwa "kwa nini hukumpigia simu wakati namba yake unayo?".Kigwangwala ana nia aidha ya kubadili mazungumzo (spinning)watu waache kujadili uchaguzi au ana chuki binafsi na Mo.
Napitia tu
 
Back
Top Bottom