Mo Dewji atema tena cheche, atawataja wanao mkwamisha ndani ya Simba

Mo Dewji atema tena cheche, atawataja wanao mkwamisha ndani ya Simba

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
"Huu ni Mwaka wa Tano na mchakato wa mabadiliko haujaisha na Bahati mbaya kuna watu ndani ya Simba wanakwamisha huu mchakato, angekuwa mwekezaji mwingine ambaye hana mapenzi na Simba siku nyingi ameondoka"

“Lakini kutokana na historia yangu na klabu na navyoipenda hiyo klabu, leo usipojua hatma yako nani ataendelea kuwekeza lakini kila mwaka (Year in, Year Out) naendelea kuwekeza,”

"Nimefanya nao mkutano nimewaambia kuwa wale ambao wanakwamisha hili jambo nawajua, kwahiyo wakiendelea nitatoka hadharani nitawataja kwa majina na hatma yangu mimi na wao itabaki mikononi mwa Wanasimba"

“Kuwekeza kwenye vijana ni Long Term Goals, mimi nimeingia Simba tukiwa na Bajeti ya Bil. 2, leo bajeti yetu mwaka huu 2023/24 inaweza kufika Bil. 20 kwa hivyo Bajeti imezidi mara 10 kwenye miaka mitano na hii ni Great Achievement.

“Lakini kuna watu wanasema hapana tuwekeze kununua wachezaji ambayo ni Short Term ambayo utapata mafanikio mara nyingine utafeli,”

1679981099312.jpg

Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba SC, MOHAMMED DEWJI.
Source: Futball planet
 
Ya SIMBA yafaa kujadiliwa na wana SIMBA wenyewe.. Wengine nje ya hapo ni wachawi tuuu
"Nimefanya nao mkutano nimewaambia kuwa wale ambao wanakwamisha hili jambo nawajua, kwahiyo wakiendelea nitatoka hadharani nitawataja kwa majina na hatma yangu mimi na wao itabaki mikononi mwa Wanasimba" mo dewji, 2023
 
Hivi mnaoshabikia mpira wa hapa kwetu huwa mna roho za namna gani?

Mimi ni mpenzi wa mchezo wa mpira wa miguu,ninaangalia ikiwa unachezwa na rika lolote,timu yoyote,lkn kuweka ushabiki na mapenzi kwenye timu zetu hapa kwetu,hiyo ni ngumu.
 
Ni mtazamo wake kwa kile anachokijua sijaona shida hapo
 
Hivi mnaoshabikia mpira wa hapa kwetu huwa mna roho za namna gani?

Mimi ni mpenzi wa mchezo wa mpira wa miguu,ninaangalia ikiwa unachezwa na rika lolote,timu yoyote,lkn kuweka ushabiki na mapenzi kwenye timu zetu hapa kwetu,hiyo ni ngumu.
Lazima tuthamini vya kwetu mkuu
 
Back
Top Bottom