MO Dewji atembelea Klabu ya FC Porto kuangalia namna ya kushirikiana na Simba SC

Ila kwa hali hii Mtani inaonekana mliteseka sana kule nyuma. Maana kila habari kwenu mmeigeuza habari ili mradi tu. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Sisi lengo letu ni kukuza brand tu na hilo mtani tumefanikiwa. Jina letu hata miamba ya soka barani Africa kwa sasa wakilisikikia najua kihofu lazima kiwaingie
 
washabiki wengi wa yanga wanasubiri uongozi mpya ndio waanze kuchanga,subir baada ya uchaguz uone mikakati ya yanga, MO Dewji ni tapeli tu ndio maana African Lyon ilimshinda
 
Mbona wakina Shafii wanatembelea mpaka wembley,bernabeu ,nk .Mimi sioni cha ajabu hapo hiyo kama ziara tu
Kwani shaffi ni nani , kwanini asipewe udhamini yanga kwakuwa yeye ni mzoefu kwenda ghaibuni
 
Kea mtazamo huh..tutaikuza na kunyanyuwa kiwango Cha mpira nchini haswa wachezaji nao waShirikishwe ili waondowe hofu na woga !!
 
Simba Inatakiwa Wafanye Mipango Na Gor Mahia Ndio Saizi Yao Sio Porto
 
Mkuu umesoma maelezo ya MO au unajifurahisha tu ifike wakati utumie akili yako kuandika vitu vya maana vinginevyo tutakuana una wivu wa kike
 
Sasa mkuu simba hawana vyote hivyo ulivyovitaja na ndio maana huenda Mo ameenda kujifunza ili kuweza kuanzisha vitu hivyo kwenye club yake? Ningeshangaa sana endapo FC Porto wangekuja kujifunza kwa simba, lakini kwa Mo kwenda kujifunza kwa Porto nadhani ni sahihi kabisa.

Kubali kataa, hatuwezi kutoboa kwenye soka letu bila kujifunza kwa waliotuzidi
 
Mbona wakina Shafii wanatembelea mpaka wembley, bernabeu ,nk .Mimi sioni cha ajabu hapo hiyo kama ziara tu
Wembley na Bernabeu ni viwanja, Porto ni klabu. Sasa sijui inakuwaje unalinganisha mtu aliyetembelea uongozi wa kiwanja na aliyetembelea uongozi wa klabu
 
Bora huyu kuliko MANJI aliyekuwa anasafirisha sembe
 
Hao watu wako wakitembelea wanasema wameanda kufanya mipango ipi...?
Kuna kutembelea kama kutalii na kutembelea pamoja kutaka kufanya ushirikiano..Mbona ameeleza hapo MO lengo inakuwaje msielewe?
Mimi naona kama utalii tu coz kuna mwaka ilikuwa kama hivyo ushirikiano na Klabu ya sunderland ya uingereza mpaka leo sijaona matunda yeyote ya huo ushirikiano ndio maana naona kama siasa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…