MO Dewji atembelea Klabu ya FC Porto kuangalia namna ya kushirikiana na Simba SC

MO Dewji atembelea Klabu ya FC Porto kuangalia namna ya kushirikiana na Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mfanyabiashara Maarufu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji MO, ameitembelea Klabu ya FC Porto ya Portugal kuangalia namna ya kushirikiana na Simba SC kujua fursa mbalimbali.

"Jana nilipata nafasi nzuri ya kujifunza nilipotembelea FC Porto ambapo niliweza kujua fursa za ushirikiano kwa kukuzia vipaji cha Simba SC huko mbeleni.

Tuna mengi ya kujifunza na kupata kutokana na uzoefu wa FC Porto. Natarajia kuimarisha mazungumzo yetu hivi karibuni".

Ameandika MO kwenye ukurasa wake wa Twitter.
IMG_20190430_233001.jpeg
IMG_20190430_232954.jpeg
 
Tatizo vyuraa fc wakati Manji anashughulikiwa na anaeutaka u waziri wa michezo, hamku mtetea Manji wenu .

Sisi MO hatukupua hadi akaokotwa jirani na anakokaa jiwe. tehetehee tehetehee
 
MO anaitumia simba kwenye PR.
Simba nayo inamtumia....kama mwekezaji.
 
Alishatembelea hadi juventus ,sijui iliishia wapi

Mo ni kanjanja tu, kama manji, kamwe ataondoka simba hata alivyosema atafanya , 50% hajatimiza
 
Haya mambo anayoyafanya MO ndio yanayotakiwa kwenye ulimwengu wa soka la kisasa.
Na sio kuwa ambia wachezaji kukwepa mlango wa kuingilia uwanjani.
Na kuishia kutozwa faini kila kukicha.
 
Mfanyabiashara Maarufu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Klabu ya Simba SC, Mohammed Dewji MO, ameitembelea Klabu ya FC Porto ya Portugal kuangalia namna ya kushirikiana na Simba SC kujua fursa mbalimbali.

"Jana nilipata nafasi nzuri ya kujifunza nilipotembelea FC Porto ambapo niliweza kujua fursa za ushirikiano kwa kukuzia vipaji cha Simba SC huko mbeleni.

Tuna mengi ya kujifunza na kupata kutokana na uzoefu wa FC Porto. Natarajia kuimarisha mazungumzo yetu hivi karibuni".

Ameandika MO kwenye ukurasa wake wa Twitter.View attachment 1085228View attachment 1085229
Aiseee chalii yangu rudisha avatar Picha ya malema kwenye profile yako ile aliyovaa kofia ya EFF
 
mwambieni porto hawahongi marefa
Kila lugha mtaongea, aliwalea sana yule jamaa sasa kwisha shughuli yenu...sisi habari nyingine Vyura nyie[emoji196][emoji23][emoji196][emoji23]
 
Alishatembelea hadi juventus ,sijui iliishia wapi

Mo ni kanjanja tu, kama manji, kamwe ataondoka simba hata alivyosema atafanya , 50% hajatimiza
Wewe ulishatembelea timu ipi na ipi hata hapa bongo ili tukuone ww si kanjanja??
Tatizo mnaongea sana
 
Mbona wakina Shafii wanatembelea mpaka wembley,bernabeu ,nk .Mimi sioni cha ajabu hapo hiyo kama ziara tu
 
Vyura watapinga na hili?
MO ameshajua anafanya kazi na Mbumbumbu kwaiyo anazidi kuwachota akili na Mi Mbumbumbu isivyo jitambua inakenua na kucheka.FC Porto watafanya mipango gani na Simba? Simba awana uwanja wa mazoezi, awana timu za vijana, yeye MO kawekeza Billion 20 kwa miaka 5 ivi mnawaona Porto timu ya Mchangani.

Yaani wafanye Mipango ya maendeleo ya Soka na mwekezaji ambae uwekezaji wake haufikii ata pesa ya ukarabati wa viti katika uwanja wao.
Timu haina ata kituo cha kulea vijana!! Porto wakisema waifuatilie Simba wataikuta ina wachezaji wenye wastani wa miaka 32 kitu ambacho kwa soka la ulaya aina iyo ya wachezaji wengi wanafikiria kustaafu.
Kwa ujumla MO alikwenda kufanya utalii na kupiga picha, kama mtanzania yoyote anaweza kwenda na kufanya ivyo kwakua wenzetu vilabu vyao ni sehemu ya utalii hasa club kubwakubwa zenye historia ndefu. Kwa ujumla Mbumbumbu mnazidi kuonyesha kwanamna gani mna akili za kushikiwa.
 
Mbona wakina Shafii wanatembelea mpaka wembley,bernabeu ,nk .Mimi sioni cha ajabu hapo hiyo kama ziara tu
Hao watu wako wakitembelea wanasema wameanda kufanya mipango ipi...?

Kuna kutembelea kama kutalii na kutembelea pamoja kutaka kufanya ushirikiano..Mbona ameeleza hapo MO lengo inakuwaje msielewe?
 
Back
Top Bottom