Mo Dewji ateua wajumbe wapya Bodi ya Simba SC

Samahani kwa wanaojua mtusaidie, kateua kwa mamlaka yapi aliyonayo?

Wale wenye 51% wanawakilishwa na akina nani kwenye hiyo bodi?

Maana nimeona pia kamteua mwenyekiti wa bodi, sijui nafasi ya wale wenye 51% ni ipi so far
Mamlaka ya Katiba ya Simba company Sports club
ambayo inataka kutakuwa na bodi ya wakuregenzi 16
8 kutoka upande wa timu ambao walipigiwa kura hiv karibuni
na 8 wengjne kutoka kwa mwekezaji (Mo)

wale 51% wanawakilishwa na wale kina mangungu na wenzake waliochaguliwa mwezi uliopita
 
Kwani wakati wanaweka kwenye account hewa walikuja Magwepande?,si walikuwa huko huko na sisi habari tulizipata sasa kwa nini mpaka leo haijulikani ni Bank gani waliweka?

Ila Tz pamoja na utajiri wa mali nyingi basi pia tumebarikiwa na ushabiki wa hovyo sana.
Nyie mwanachama huo mpunga 51% uko wapi?zikusanyeni kwanza ndipo atawaonyesha zilipo ili mchanganye!!na kweli Tz kuna mashabiki wa hovyo wao wanataka kuona timu inashinda tu bila kuisaidia kwenye kujiendesha,utasikia tu bora utuachie timu yetu!!!
 
Nadhani hizo 51% zitapelekwa kwenye soko la hisa na watu watanunulia huko.

Kimsingi Mo hashindwi kumpanga mtu wake anunue hisa za 2%, kwa hiyo ukichanganya na ile aliyonayo sasa, majority ownership waliyomnyima ataipata tu kwa njia hiyo.
 
Mkuu masuala ya Hisa hayafanyiki hivyo. Wale watakaonunua 51% watabaki huku huku kwa 51%. Mo anabaki na za kwake 49%
 
Naelewa vizuri. Ninachosema anampanga tu mtu anunue 2% kwa jina la huyo mtu (au watu 4 wenye 0.5%) halafu kwenye maamuzi yanayohitaji kupigiwa kura wanakuwa wanaungana pamoja.
 
Samahani kwa wanaojua mtusaidie, kateua kwa mamlaka yapi aliyonayo?

Wale wenye 51% wanawakilishwa na akina nani kwenye hiyo bodi?

Maana nimeona pia kamteua mwenyekiti wa bodi, sijui nafasi ya wale wenye 51% ni ipi so far
Hukuona uchaguzi uliofanyika wajumbe wa bodi waliochaguliwa ?
 
Labda hiyo, yawezekana Mkuu.
Niliwahi kuhudhuria mkutano wa wanahisa wa CRDB. Nilikuwa bwa mdogo tu ila tayari nikikuwa navielewa hivi tuvitu kiasi. Kuna mpuuzi alikuwa ana hisa za majority alikuwa kila hoja inayoletwa, anasimama anaipangua kwa kusema yeye anawazidi wote kwa hisa. Yaani ilikuwa hadi kero.
 
Naelewa vizuri. Ninachosema anampanga tu mtu anunue 2% kwa jina la huyo mtu (au watu 4 wenye 0.5%) halafu kwenye maamuzi yanayohitaji kupigiwa kura wanakuwa wanaungana pamoja.

sidhani kama inawezekana kwa sababu hiyo 51% ni ya mashabiki haigawanyiki.
Investor yoyote itabidi aende kwa mo wagawane zile 49%.
ingekuwa inawezekana basi mo angechukua hata 100%.
 
Hiyo 51% inaweza kuwa hisa milioni 400 kwa mfano. Wanaweza kuamua waweke akiba hisa milioni 250 halafu zilizobaki hisa milioni 150 zikaingizwa sokoni. Kwa hiyo watu wanaenda kwenye soko na kununua kwa jinsi ya uwezo wao.

Kwa hiyo mwingine anaweza akanunua hisa 500, mwingine hisa 20,000. Kwa hiyo inawezekana kabisa hilo kufanyika ingawa hata hizo 0.5% si pesa ndogo itakayohitajika kuzinunua.

Ila pia nadhani utaratibu utakuwepo wa mwekezaji kwenda moja kwa moja kwa Mo na kununua baadhi au hisa zake zote.
 
kwa kidogo nijuavyo mo alitaka kuchukua 100% ila baadaye ikatungwa sheria iliyolimit investor kumiliki 49%(minority). Kama kuna mtu atataka ku invest ndani ya simba itabidi amfuate mo wagawane hizo 49%. Hizo 51% ni za timu hazigusiki.
 
Nakuelewa na kukubaliana na wewe hadi hapo unaposema 51% hazigusiki. Nadhani huo utaratibu ni wa muda tu ila baadae naamini BAADHI ya hizo hisa zitawekwa katika soko la mitaji ili ziweze kununulika na kuuzwa kwa uhuru zaidi.

Pia Simba wanaweza kukusanya pesa nyingi sana kwa kuziingiza hizo hisa katika soko maana si tu watu binafsi watakaonunua ila pia makampuni na taasisi mbalimbali za fedha na uwekezaji.

Kwa hiyo faida itakuwa kwa pande zote mbili, club na wanachama pia.
 
unaposema kuuza hisa maana yake moja kwa moja timu unaiweka kwenye private sector/investors kitu ambacho sheria ya umiliki iliyotungwa kipindi mo anataka kuinunua simba ilikataa.
ukishauza hizo hisa maana yake hao wawekezaji watafanya wanachotaka wao shabiki hahusiki. Nadhani ni kwa vile tu taifa letu halina wawekezaji wengi ndo maana mo anapigiwa magoti pale simba. Siku akiamka vibaya akaamua kujitoa tutatembeza bakuli kama yanga.
 
Back
Top Bottom