SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Nitajaribu kuitafuta hiyo sheria niisome vizuri na huo mkataba wa mabadiliko ndani ya Simba.unaposema kuuza hisa maana yake moja kwa moja timu unaiweka kwenye private sector/investors kitu ambacho sheria ya umiliki iliyotungwa kipindi mo anataka kuinunua simba ilikataa.
ukishauza hizo hisa maana yake hao wawekezaji watafanya wanachotaka wao shabiki hahusiki. Nadhani ni kwa vile tu taifa letu halina wawekezaji wengi ndo maana mo anapigiwa magoti pale simba. Siku akiamka vibaya akaamua kujitoa tutatembeza bakuli kama yanga.
Sidhani kama Mo anapigiwa magoti na mtu, ni kwamba yeye ndiyo ameweza kuonyesha utashi wa kuwekeza na mabadiliko haya yanayoendelea kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu ya utashi wake, hivi hivi yangebaki maneno tu.
Siku za mbele Simba watapata wawekezaji bora zaidi, huu ni mwanzo tu na mwanzo ni mgumu.