Mo Dewji ateua wajumbe wapya Bodi ya Simba SC

Nitajaribu kuitafuta hiyo sheria niisome vizuri na huo mkataba wa mabadiliko ndani ya Simba.

Sidhani kama Mo anapigiwa magoti na mtu, ni kwamba yeye ndiyo ameweza kuonyesha utashi wa kuwekeza na mabadiliko haya yanayoendelea kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu ya utashi wake, hivi hivi yangebaki maneno tu.

Siku za mbele Simba watapata wawekezaji bora zaidi, huu ni mwanzo tu na mwanzo ni mgumu.
 

katika suala la mabadiliko pesa yake ndo imeongea. Akijichomoa tu siku moja hata uko caf tutakuwa zaidi ya vichekesho.

kupata wawekezaji kwa nchi yetu sidhani kama ni rahisi ndio maana yanga iligeuka ombaomba.
Kama ingekuwa rahisi kupata wawekezaji basi zile 49% zinazotolewa kwa ajili yao zingegombaniwa lakini haipo hivyo.
hivyo inabidi hawa waliopo tuwapigie goti ili wasiondoke.
Ndio maana mashabiki wanaolijua hilo hawataki hata kuulizia bil.20 ziliko.
 
Ni kweli kwa uchumi wetu huu hakuna wawekezaji wengi wanaoweza kuwekeza kwenye mpira. Hata wale waliopo hawawezi kuingia huku mpaka mazingira ya ufanyaji kazi yaboreshwe katika ngazi zote.

Yanga wangeweza kuwa wa kwanza kwenye kujiendesha kisasa ila mpaka leo wanasumbuliwa na uswahili na siasa za ccm.

Ila bado nahisi hilo suala la 49% haujalielewa. Hisa za Simba zikitangazwa kuuzwa wazi zitauzika sana tu. Sidhani kama mpaka sasa mwanachama mmoja mmoja au mshabiki anaweza kujinunulia hisa za club.
 
Samahani kwa wanaojua mtusaidie, kateua kwa mamlaka yapi aliyonayo?

Wale wenye 51% wanawakilishwa na akina nani kwenye hiyo bodi?

Maana nimeona pia kamteua mwenyekiti wa bodi, sijui nafasi ya wale wenye 51% ni ipi so far
Bado hata mimi nafikiria nguvu ya kuteua wajumbe wa bodi ameitolea wapi.
 
Bodi ina wajumbe 16? Pengine taratibu zimebadilika ama kuna kitu nimesahau.

Bodi inakuwa na member wasiopungua watano na wasiozidi kumi.
 

kwa kifupi mo alitaka 51% (majority)
sheria ikambana ikasema 51% za club 49% wawekezaji wa tatu wagawane.
nadhani ili kuziba huo mwanya mo akamweka dada yake fatma dewji na kaka yake kassim dewji. Kama ingekuwa inawezekana kununua hizo 51% sidhani kama angeshindwa.
 
Ungekua ww Ungeweka hizo billion 20
Kwa lipi la maana kiasi cha kuhatatisha pesa yote hiyo
Hizo ni pesa ndogo kwenye mpira
Mo akiuza jezi milion 3 kwa faida ya elfu 20 anakuwa na bilioni 60 bdani ya mwezi mmoja fikiria kwa upana huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…