Mo Dewji Bilionea aliyegeuza soka la Africa kuwa Biashara

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
IMG-20240912-WA0040.jpg
IMG-20240912-WA0041.jpg
 
Wabongo kujisifia ujinga na mambo yasiyokuwa na maana tuko vizuri.
Timu kama Al Ahly ambazo zimekuwa zinawalipa mishahara mikubwa wachezaji wake kama wa ulaya na kununua wachezaji kutoka ulaya zitasemaje?
Rais wa klabu, Mohammed Dewji ametajwa na jarida la Face2Face Africa lenye makao makuu yake jijini New York, Marekani kuwa mmoja kati ya mabilionea wawili ambao wamesaidia kukuza biashara ya mpira wa miguu barani Afrika.

Kutajwa kwa Mo kumetokana uwekezaji na mafanikio ambayo Simba imeyapata tangu alipoanza kufanya uwekezaji katika klabu hii kubwa zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
 
Kutajwa si una weza uka lipia ili uonekane ??
Majarida mangapi yana kumbwa na skendo hizo
 
Big no, watu walio fanya mpira wa Africa uonekane biashara, SI mo dewji big nooo.

Total oil, dstv na Azam, hawa wame cheza nafasi kubwa sana kujenga soka hili.

Dstv ali kuwa ana onyesha klabu bingwa.
total oil ali dhamini kwa mkwanja mzuri.
Azam kaja kutu unganisha Wana east Africa kwa kutangaza na kudhamini pia.
 
Kwahiyo hao wote wangeendelea kuonesha huku timu zetu zikiwa bado zinatembeza mabakuli kuchangishana pesa za kulipa wachezaji, kungekua na team gani tz ingefika kwenye michuano ya kibingwa ya Africa katika hali ya ushindani na si kushiriki tu.

Lazima tukubali kwamba Tz mpira ulikua haujapewa thamani kama ambavyo umepewa sasa, na Mudi ndio alikua mtu wa kwanza kuingia front na kuanza kuufanya mpira wa Tanzania uanze kupata nguvu katika level za ushindani na wengine nao ndio wakaingia kuja kuweka pesa kwenye vilabu vingine.

Sasa hivi unaona vilabu vya Tanzania vinagombania wachezaji na vilabu vingine vya kwenye top ten Africa na vinashinda hizo bato.

Kwahiyo jamaa apewe mauwa yake kwamba ameweza kuwafumbua watu macho na kuwafanya waweze kuona fulsa na kuanza kuwekeza kwenye mpira.
 
Rais wa klabu, Mohammed Dewji ametajwa na jarida la Face2Face Africa lenye makao makuu yake jijini New York, Marekani kuwa mmoja kati ya mabilionea wawili ambao wamesaidia kukuza biashara ya mpira wa miguu barani Afrika.

Kutajwa kwa Mo kumetokana uwekezaji na mafanikio ambayo Simba imeyapata tangu alipoanza kufanya uwekezaji katika klabu hii kubwa zaidi kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Simba imechukuwa ubingwa mara ngapi wa Africa?

Moze Katumbi ameiwezesha TP Mazembe kuchukuwa ubingwa wa Africa, sasa asitajwe Katumbi atajwe huyu Gabachori kama siyo uandishi wa bahasha ni nini?

Bakhresa huwa hawaangaiki na hivyo vijarida ambavyo havimuweki kwenye orodha ya matajili lakini ukweli ni kwamba Mo Dewji hamfikii Bakhresa wala Rostam Aziz, hawa hawana mpango na Forbes.
 
Big no, watu walio fanya mpira wa Africa uonekane biashara, SI mo dewji big nooo.

Total oil, dstv na Azam, hawa wame cheza nafasi kubwa sana kujenga soka hili.

Dstv ali kuwa ana onyesha klabu bingwa.
total oil ali dhamini kwa mkwanja mzuri.
Azam kaja kutu unganisha Wana east Africa kwa kutangaza na kudhamini pia.
Hao wote unaowataja wanarusha mpira ambao vilabu vina wawekezaji. Yes wana nafasi kubwa mno na bila wao ligi isingekua kubwa ila uwepo wao haufuti umuhimu wa wawekezaji katika Club husika.
 
Kwahiyo hao wote wangeendelea kuonesha huku timu zetu zikiwa bado zinatembeza mabakuli kuchangishana pesa za kulipa wachezaji, kungekua na team gani tz ingefika kwenye michuano ya kibingwa ya Africa katika hali ya ushindani na si kushiriki tu.

Lazima tukubali kwamba Tz mpira ulikua haujapewa thamani kama ambavyo umepewa sasa, na Mudi ndio alikua mtu wa kwanza kuingia front na kuanza kuufanya mpira wa Tanzania uanze kupata nguvu katika level za ushindani na wengine nao ndio wakaingia kuja kuweka pesa kwenye vilabu vingine.

Sasa hivi unaona vilabu vya Tanzania vinagombania wachezaji na vilabu vingine vya kwenye top ten Africa na vinashinda hizo bato.

Kwahiyo jamaa apewe mauwa yake kwamba ameweza kuwafumbua watu macho na kuwafanya waweze kuona fulsa na kuanza kuwekeza kwenye mpira.
Basi angesema kwa Tanzania au kwa Africa Mashariki na sio kwa Africa. Kwa Africa kuna watu wameanza kabla ya Mo na wamefanya makubwa na kuipa thamani mpira wa Africa.

Hakuna klabu ya Tanzania inayoweza kushindana na Al Ahly, Raja Casablanca, Es Tunis, Mamelodi, Wydad, Zameleki, Petro Luanda, Pyramids, n.k kwenye kugombaniana mchezaji. Bajeti za timu za Tanzania na mishahara hailingani na hao wakubwa. Hizo timu hazijawahi kusajili mchezaji mwenye jina kubwa Africa, Adebayor, Bwalya, Manzoki n.k hawa wote huyo Mo alishindwa kuwaleta Simba kutokana na mfuko wake mdogo.
 
Back
Top Bottom