Mo Dewji kafanikiwa pakubwa sana kuishika Simba SC

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Sina muda wakutoa salamu Wala kuwajulia hali, kutokana na namna gani nilivyochafukwa kwa kuona mtani akisimangwa waziwazi na kanjibahi Mo dewji.

Wiki imekua ngumu sana kwa wanasimba kutokana na boss wao janja janja kuropoka kwenye media namna gani simba SC inavyomtia hasara lakini pia hakuishia hapo na kusema kuwa anawajua wote viongozi wa simba wanaoihujumu simba sc na wakiendelea atawataja hadharani.

Kutoka na kauli hizo za kanjibahi Mo dewji, naona kabisa ni nanmna gani anajaribu kucheza na akili za wanasimba hii ni hatari sana kwa maana anajua kabisa pale simba hakuna wakumbabaisha hakika ana amini simba kaishika kwenye koromeo hakuna wakusema chochote mbele ya kanjibahi.

Kuna kiongozi mmoja alishawahi kusema wanasimba ni mbumbumbu, huu msemo inaendelea kuwatafuna wanasimba waziwazi bila yakificho.

Hawajiulizi maswali haya "Kama simba inampa hasara kwa Nini haondoki??
Mo dewji huwa anaibuka kila anapoona simba imefika robo fainal lakini wanasimba wamefumba macho na masikio hakuna atakayehoji haya.

Ndiyoooo, kwani nana asiyejua kuwa mo dewji alimpambania mwenyekiti huyu mpya achukue kiti na alifanikiwa ili aendelee kula ugali wake pale simba bila kubughudhiwa na mtu yoyote??

Nani asiyejua kuwa kanjibahi aliratibu vijana kumpinga hamisi kingwala alipohoji juu ya zile bilioni hewa pale simba??

Babu yangu mzee NGWENA alishawahi kuniambia kuwa "mtu anayefanya kibarua mahali miaka takiribani kumi lakini ukimuuliza mafanikio yake juu ya hiyo kazi anayofanya hawezi kukuambia kweli Kama anapata faida Bali atalalamika tu nakusema hali ngumu tupo tunazuga tu."

Ndiyo kinachotokea kwa kanjibahi, hawezi kuweka wazi mafanikio anayoyapata hapo simba Bali ataendelea kulia Lia ili aonekane mwema na anaipambania sana simba sc.


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Amewamalisa kabisa kawavunja magoti,
Anawamudu mnoo hadi anawatisha kuwa eti ikifika hatua wakaamua kukaa mezani kupiga mahesabu itakutwa amewekeza billion 50 na sio billion 20.
Kiswahili Gani hiki wewe!
 
Bahati nzuri MO waalaa hababaishwi na maneno maneno ya hovyo kama haya yenu! Na wana Simba, hawawezi kuitupa ALMASI waliyonayo mkononi kwa kelele zenu kuwa hiyo si ALMASI bali ni VICHUPA CHUPA!
 
Kwa hizo porojo itakuwa unakula na kulala kwa shemeji Yako huna hata uwezo wa kuchangia mlo mmoja wa wachezaji, endelea kucheza draft kijiweni mpika majungu.
Kweli kabisa hujakosea nipo nacheza draft huku nimempakata dada yako. [emoji41]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Bahati nzuri MO waalaa hababaishwi na maneno maneno ya hovyo kama haya yenu! Na wana Simba, hawawezi kuitupa ALMASI waliyonayo mkononi kwa kelele zenu kuwa hiyo si ALMASI bali ni VICHUPA CHUPA!
Anavyokuja kulia Lia kwenye media si anataka huruma za wadau Kama sisi lazima tuzungumze nakumchana kuwa sisi siyo mbumbumbu Kama hao anaowapiga huko.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wenye Simba yao wala hawajali, cha msingi timu haikosi kucheza mfululizo robo fainali ya CAF club competitions
Siku hizi mafanikio yenu ni kufika robo fainali. Zile story zenu za kusema "muhimu timu inashinda na kuleta makombe" hazipo tena. Maana makombe yote siku hizi yanabebwa na Yanga.
 
wewe mafanikio yako yako wapi, weka wazi yakwako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…