Mo Dewji kaitelekeza timu yake African Lyon ataiweza Simba?

Mo Dewji kaitelekeza timu yake African Lyon ataiweza Simba?

Manji anachaguliwa na wanachama.
Je Mor, mmiliki atachaguliwa na nan??
 
Amesema aliiacha africa lyon kwa sababu ilifika muda, mechi inaendelea uwanjani hakuna mashabiki.
Azam angekua na mawazo kama yale asingefika pale,,,yeye angeibrand timu na ingekua na viwango vya akiza azam tu au aungeibadili jina na kuiita Mo F.C,Mo Sports Club na mengineyo,mbona ingefanikiwa tu
 
Tafuteni Business Consultance, Aje awashauri kabla amja fanya maamuzi??
Mor ana Wisdom of the Business that's why anataka anunue club ya simba.
Ushaury. Embu pigeni hesabu mjuwe kila mwanachama atauza club kwa shingap.??
Alafu mpate Akili!!
 
Manji anachaguliwa na wanachama.
Je Mor, mmiliki atachaguliwa na nan??
Naamini unaijua changamoto atakayoikabili Mo huko mbeleni............Kuitoa timu kwa wanachama na kumuuzia mtu si jambo rahisi kama ilivyo kuianzisha timu lyk azam.
Mo atakutana na changamoto toka kwa hao hao the so called wanachama
 
Kwani Abramovich ni sponsor wa Chelsea? Nyie kaeni na sponsor wenu sisi tunataka mmiliki
Siamini kama huku kwenye michezo uwezo wako reasoning ni mdogo hivi....

Tunataka wamiliki wa timu kama Bakhresa, huyu ni kweli ameonesha nia ya dhati ya kuwekeza katika soka, Manji na Dewji hawa ni wajanja tu wa mjini.

Kama si raia wa Dar kuipigia kura nyingi UKAWA leo Manji angekuwa ndio meya wa jiji.
 
mi nawashangaa wanachama njaa na waandishi njaa wanaompigania mo kununua simba kwa bilioni ishirini kwani kabla timu kuuzwa ilitakiwa ijulikane thamani yake halisi kazi ambayo inafanywa na mashirika ya ukagusu wa mahesabu kama price water cooper au kpmg.
Thamani ya timu mbali na mali inazomiliki pia inaangaliwa idadi ya wapenzi wake.
umeuliza swali la msingi huyu mtu aliitelekeza african lyon je baada ya miaka michache hawezi kuuza timu kwa bei kubwa zaidi pengine hata kwa mtu wa yanga maana yye ni mfanyabiashara.
wengi tuliwaamini kina aveva ila ukweli hawana mipango yoyote ya kuiendesha simba kisasa wako pale kibiashara ile timu waliikuta imeanzishwa waiache kama ilivyo
 
Naunga Mkono Simba Kubaki kama ilivo. Kama Dewji ana Talent za uongozi na yeye ni mwanachama wa simba anaruhusiwa kuogombea Uongozi ili afanye maendeleo anayo kusudiwa. Njia Nyengine ni kui sponsor Simba kwa udhamini wa muda mrefu .
Kuuza Simba kwa yeye kuimiliki hilo haliwezekani. Mimi ni mwanachama wa simba na mtu wa kwanza kwenda mahakamani kupinga hatua hii.
Simba ni timu ya wazee wetu wa Dar es salaam ..Pamoja na Yanga na Coastal Union na African Sports zina Historia za kipekee katika siasa za nchi hii tangu enzi za Kugombea Uhuru.
wazee wale waliziongoza timu hizi kwa mafanikio makubwa na ikawa ndio chachu ya maendelo ya Footbal Tanzania.
Simba ni Priceless..huwezi kuithamini kwa fedha kabisa. Ni club ambayo imeweza ku survive zaidi ya Miaka 70 ya dharuba kwa muundo wake huu huu uliopo ambao ni kuwa chini ya wanachama na wapenzi.
How much is share ya Club hii ?'
Na jee nani atakua beneficiary wa hizo share Jee wajukuu wa waanzilishi wa Simba au matapeli kina Hanspope na Aveva ?
Ni wa zi Simba sio Africa Lyon ambayo Dewji ilimshinda kuindesha kwa sababu moja tu..hakua tayari kuwekeza kama alivo ahidi.

Tunamshauri yeye na wote wanaopokea Rushwa waache ndoto zao halitawezekana kabisa hili.....bora simba ife kabisa kuliko kuuziwa mtu mwenye malengo ya kuifanya simba brand ya biashara yaek. Na hakika Tunaomba TAKUKURU Wachunguze wale wote wanaoshabikia hili kwani kuna kila dalili wanapokea rushwa kufanikisha mpango huu haramu
SIMBA NI YA WATANZANIA WAPENZI HAIWEZI KUUZWA NA HAITAUZWA..
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] kelele nyingi afu umeongea pumba tu. Sasa hiv Mpira ni pesa na ili uweze kuendeshee timu ni lazima kuwe na mfumo unaoeleweka kiutendaji pia ishu ya pesa nan atanufaika nazo ni wanachama wa simba na club yao ndiyo watakao nufaika na mfumo huu mpya ambao vilabu vyote dunian wanatumia. MFANO arsenal. Mfumo huu utatupa faida wanachama wa club ya simba kupitia hisa zetu kwa sababu tutaweza kuuza ikitokea mwanachama ameamua tofaut na sasa hiv unamilik likad tu afu hupat faida YOYOTE. Ishu ya hajasema anaenda kubadil historia ya simba jibu hapana anaenda kufanya mageuz ya kimpira ndani ya club ya simba
Kuhusu African Lyon amejibu ni timu ambayo haikuwa na mashabik hivyo na pia ubabaishaji ulikuwa mwingi watu walikuwa wanawaza kupiga dili tu

Ishu ya kudhamin simba kama ni mfuatilij mzur wa soka kumbuka udhamini wa mo kuanzia 2003 ,kurud nyuma alidhamin simba na kwanini aliamua kujitoa jibu ni kwa sababu ya mfumo wa kibabaishaji ya uendeshaji wa club hakuna mfanyabiashara asiyependa faida kupitia udhamini wa club

Wanasimba ni bora tumpatie mo ajaribu kuleta mageuzi wee timu ina 70 lakin hata uwanja mdogo kama ule kituo cha michezo cha jakaya kikwete pale kidongo chekundu hatuna

Kwa mpenda soka YOYOTE yule huu ni muda mwafaka wa kuamua hatma ya club yetu
 
Mtoa mada kaauliza swali zuri hiyo hela anapewa nani?

Yaani unatumbukiza hela kwenye account ya Simba halafu wewe tena unapewa kumiliki Simba kwa hiyo unaenda kumiliki hela zako mwenyewe
yaani umetoa hela mkono wa kushoto na kupeleka wa kulia.
 
....nyie jamaa kila siku mnahangaika kuirudisha simba nyuma, halafu mnajiita wanazi!, poa, endeleeni kusajili "rejects" toka vilabu vingine muendelee kuota kuwa mabingwa!
 
Siamini kama huku kwenye michezo uwezo wako reasoning ni mdogo hivi....

Tunataka wamiliki wa timu kama Bakhresa, huyu ni kweli ameonesha nia ya dhati ya kuwekeza katika soka, Manji na Dewji hawa ni wajanja tu wa mjini.

Kama si raia wa Dar kuipigia kura nyingi UKAWA leo Manji angekuwa ndio meya wa jiji.


Nadhani kati yangu mimi.na wewe mwenye uelewa mdogo amejionyesha dhahiri. Unawezaje kulinganisha uchaguzi wa meya na uchaguzi wa klabu? Kama ni hivyo basI hata Diamond anaweza kuwa Rais maana ana wafuasi kuliko JPM!
 
ukiwa na njaa, hasira ama furaha ilio pita kiasi usijaribu kufanya maamuzi Simba wengi wanahasira ya kuukosa ubingwa mfululizo hii itapelekea kufanya maamuzi ambayo baadae watayajutia yaa sababu wewe huna hela unaona bora familia yako utunziwe na mwanaume mwingine
 
Mo chukua simba bureeeeeeeeeeeee kabisa wala hatukuuuzii kwani hao wazee wa dar na wanachama wa simba ndio kikwazo cha maendeleo ya timu kwani wamekalia uchawi,siasa za mpira ,majungu,fitna na ubabaishaji wa kimazoea pamoja na maslahi binafsi. Tujiulize miaka 70 iliyopita toka simba ianzishwe Ina historian gani barani Africa na duniani kwa ijumla? Uwanja na miundombinu ya clab ilioanzishwa mika 70 iliyopita haieleweki na bado mnang'ang'ania wazee na wanachama waendelee kuiongoza clab? Huu ni MUDa muafaka wa kumuuzia MTU binafsi club kwani si si washabiki hatujaili clab inamilikiwa na nani, tunachotaka ni clab ishinde tufurahi twende makwetu.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mmiliki binafsi ni hatari sana kibongobongo bora ingekua ni kampuni


Pengine hujasikia proposal ikoje. Nashukuru nilichopendekeza humu miezi kadhaa iliyopita ndicho kinachofanyika sasa. Ngoja niutafute ule uzi
 
Mtoa mada hujui ukubwa wa Simba kuizidi hiyo African Lyon?

Kwanza timu zote zenye jina African ni uzao wa Yanga

Toto Africa
African Sports
Pan African
Nyota Africa
African Snakes
African Lyon
Safi.. Vilevile mtoa mada hoja yake ni butu mno.. wala hajiulizi kuwa kwanini hata ulaya huwa wanatafuta timu kubwa ndo wanawekeza.!?
 
Mtoa mada kaauliza swali zuri hiyo hela anapewa nani?

Yaani unatumbukiza hela kwenye account ya Simba halafu wewe tena unapewa kumiliki Simba kwa hiyo unaenda kumiliki hela zako mwenyewe
yaani umetoa hela mkono wa kushoto na kupeleka wa kulia.

Simba ikiuzwa 20b nani mlipwaji?
 
Safi.. Vilevile mtoa mada hoja yake ni butu mno.. wala hajiulizi kuwa kwanini hata ulaya huwa wanatafuta timu kubwa ndo wanawekeza.!?

Sawa mwelewa, tueleweshe hii ni club ya wanachama huyo tajiri akinunua mpunga atamlipa nani? Na wanachama haki zao zipo wapi? Acheni ujanjaujanja.
 
Back
Top Bottom