Tatizo la MO ni moja tu..
Yaani utafikiri sio billionaire, ana tabia, lugha za kienyeji sana au sijui nisemeje, yaani anatafuta very cheap popularity or publicity utafikiri celebrity wa mitaani, yaani tabia ya kimaskini kabisa anayo wakati ni tajiri..
Matajiri hawana tabia kama ya MO, yaani MO anaweza bishana na Manara au Baba Levo au hata Mwijaku au watu wanaotafuta umaarufu wa kijinga tu, hiki ndio kitu anakosea MO.
Matajiri hawana tabia hizo kabisa, mara aseme katumia bilioni 85 Simba, mara bil 50, hizi hela atumie MO? Nyie jamaa muongo sana huyu, hata Simba yenyewe hajatoa hata senti ila kachukua 51% shares bure bure, hatajoa hata senti, uongo mtupu, mara aseme Simba ni hasara sana kwake, uongo mtupu, hivi bidhaa zake kwenye jezi ya Simba angeamua kutangaza angetoa shilingi ngapi kwa miaka yote?
Unaweza ona MO ni tajiri kifedha ila maskini kabisa kitabia na maisha halisi ni maskini.
Mo anasema, eti hajamuona Mayele kwenye mechi? Hata Yanga na Simba wakicheza hajamuona Mayele akicheza? MO muongo sana huyu jamaa, tabia za kienyeji sana hizi.