Mo Dewji kawadanganya tena mashabiki wa Simba?

Mo Dewji kawadanganya tena mashabiki wa Simba?

Watanzania kweli tunapenda sana kusikia habari za kupikwa kutoka mataifa mengine kuliko za makanjanja wa nchini kwetu.! Huo ushahidi wa ole moshi unatofauti gani na habari za ndani za kina privaldinho hizo si blog tu za kawaida na wao wameandika timu tajiri??? Sasa kama caf hawajaandika anpataje mamlaka ya kushutumu kuwa watanzania wana iQ ndogo kuliko. Mbona yeye kaweka ushahidi wa mablogers wa south.ambao pia ni makanjanja.?????
 
Na Thadei Ole Mushi.

Watanzania ni wepesi sana wa Kudanganywa. Jana niliandika kuhusu IQ zetu kuwa chini leo tena tumedanganyika.

Kupitia Ukurasa wa Mfadhili wa Simba Mo Dewji ameweka Poster inayoonyesha Simba kuwa moja ya Club 10 kwa Utajiri Afrika.

Nimezunguka kila Pembe ya Mitandao ya Africa ikiwemo CAF yenyewe kuona taarifa hiyo sikuona Popote.

Fuata link kuona alichokipost Mo Dewji.



Kote nilikopita wametaja Club 10 Tajiri kwa Africa kama ifuatavyo..

1. Al Ahaly
2. Kaizer Chiefs
3. Pyramids
4. Club African
5. Zamalek
6. Orlando Pirates
7. Whydad Casablanca
8. TP Mazembe
9. L' Esperance
10. Mc Alger.

Hii ni list ya 2022... fuata link zifuatazo kuona.

1. Mtandao wa Wikisouthafrica


2. Mtandao wa Newshub 360


3.Mtandao wa Briefly Richest football clubs in Africa: Which club is the wealthiest?

4. Mtandao wa Sport Briefy


Mo anaitaja Simba Kama Club Tajiri kutoka Source ipi? Tunatamani kweli kuwa na Timu Tajiri ila sio Utajiri wa Michongo.

Kinachonishangaza mashabiki wa Simba wanapongezana sasa hivi kwenye ulanzi. Kwa nn tunakuwa wepesi hivi kudanganyika?

Hata List ya Timu 10 tajiri 2021 Simba haipo na Hata kiuhalisia Simba haiwezi kuipita hata Azam kwa Utajiri hapa nchini achilia mbali huko Africa.

Cha kushangaza Mashabiki wote wa Simba wana akili za kufanana. Na sijui kwa nn IQ zao zinalingana hata graduate anashindwa kupata data Rahisi kama hizi kwenye Source Mbalimbali.

Ole Mushi
071702602
[3/2, 12:49] +255 717 158 181: Africa's Top 20 most valuable clubs
Al Ahly (Egypt) - €30.75m
Mamelodi Sundowns (South Africa) €21.3m (R382 million)
Zamalek (Egypt) - €20.55m
Pyramids FC (Egypt) - €19.43m
Orlando Pirates (South Africa) €18.15m (R325.9 million)
Esperance Tunis (Tunisia) - €17.63
Kaizer Chiefs (South Africa) - €14.63m (R262 million)
Wydad Casablanca (Morocco) - €13.21m
Etoile Sportive du Sahel (Tunisia) - €13m
CR Belouiszdad (Algeria) - €12.05m
Raja Club Athletic Casablanca (Morocco) - €10.35m
USM Alger (Algeria) - €10.05m
AmaZulu (South Africa) - €9.68m (R173 million)
Paradou AC (Algeria) €9.53m
SuperSport United (South Africa) - €9.48m (R170 million)
ES Setif (Algeria) - €9.2m
Cape Town City FC (South Africa) - €8.88m (R159 million)
Club Sportif Sfaxien (Tunisia) - €8.85m
MC Algiers (Algeria) - €8.83m
US Monastir (Tunisia) – €8.8m

😂😂😂
Hata Kaduguda amedanganyika?
 
Back
Top Bottom