Mo Dewji kujiuzulu kabla ya tarehe 16 Sept ameona nini?

Mo Dewji kujiuzulu kabla ya tarehe 16 Sept ameona nini?

Kumbe Utajiri wa ukanjanja tu🤣🤣🤣
Mo amechonganisha wananchi na serikali ya CCM hukoooo kwenye mashamba. Wananchi wanaikataa CCM kwasababu yake. Kapewa mashamba na viwanda vya chai huko milimani yeye akaviweka rehani akakopea mabilioni ya fedha ambayo hajayaelekeza kwenye mashamba na viwanda. Tapeli huyu sijui kwanini JPM alimuona Manji tu akamuacha huyu.
 
Dereva ndiye mtu wa kwanza kufahamu kama gari imefeli breki, mtu wa pili ni kondakta na watatu ni abiria ambao mara nyingi ndio wanakuwa wahanga wa gari kufeli breki.

Baada ya dereva (Fadlu) kutokuwa na imani n kikosi chake msimu huu alimtonya kondakta (Mo) kuwa kikosi chetu ni dhaifu sana dhidi ya kikosi cha wale mabwana by far kutokana na kuwakisa wachezaji wengi sana niliowataka. Na isivyokuwa bahati wachezaji hao walichukuliwa na mabwana wale. Hivyo tusije kulaumiana.

Taarifa hii ilimshtua kondakta ambae alitaharuki na kuruka kutoka kwenye gari bila kusubiri kuona nini kitatokea..

Kondakta amegundua kuwa ana umri wa miaka 50 Sasa hataki karaha Wala dhambi tena bali anataka kwenda kwa Mungu kihalali sio kwasababu ya Simba. Maana yake msimu huu hatatoa hela yake kwenda kwa mganga, kuhonga marefa, viongozi wa TFF/bodi ya ligi Wala wachezaji ili kupata matokeo; labda wewe Magori ufanye hivyo wewe msimu huu sio mimi. Yeye anataka kwenda mbinguni akiwa safi, ame confess akatema bungo.
.
Nini hasa kinesababisha ateme bungo, kazi nyingi au kuogopa kipigo?
Yule bwana ni mjanja sana lakini ni kawaida ya wahindi,,sababu aliyoitoa kwamba amebanwa na majukumu aikuniingia akilini kwasababu sio mara ya kwanza kurudi pale kama mwenyekiti wa bodi,,mpaka anarudi alikuwa anajua majukumu yanavyombana kwanini alirudi?
Kwamba amekuja kuona majukumu yanambana baada ya kuwa mwenyekiti kwa mara ya pili?
Wakati anarudi akuwaona wakina magori kuwapa huo uenyekiti wa bodi?
Hapo keshachungulia na kuona atakuja kudhalilika uko mbeleni kaonq isiwe kesi Wacha awabebeshe zigo la misumari wanyamwezi watajua wenyewe yeye kajiweka pembeni litakalotokea aulizwe magori na bodi yake🤣🤣🤣
 
Dancer mzuri ni yule anaejua wakati sahihi wa kushuka jukwaani. Kuna watu walimwambia aige kile cha GSM cha kuwaacha waswahili watukanane wenyewe kama GSM alivyofanya, yeye abakie na jukumu la kutoa tu kama anavyofanya GSM. Bahati mbaya muundo wa Simba ni tofauti na ule wa Yanga kwakuwa pale Yanga hakuna Mangungu.
 
Back
Top Bottom