Mo Dewji kumiliki hisa za klabu ya Simba baada ya kuwa muwekezaji pekee aliejitokeza

Mo Dewji kumiliki hisa za klabu ya Simba baada ya kuwa muwekezaji pekee aliejitokeza

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Bilionea Mohammed Dewji, amepita katika mchakato wa uwekezaji wa klabu ya Simba na ofa yake ya Sh bilioni 20.

Dewji amejitokeza na kuwa muwekezaji pekee ambaye aliweka dau la Sh bilioni 20 kupata hisa asilimia 51.

Hata hivyo, baada ya mchakato huo makubaliano yalikuwa ni hisa 49 anazoruhusiwa kuchukua kwa kitita hicho cha Sh bilioni 20.

Mwenyekiti wa kamati ya mchakato huo zabuni, Jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema, Mo Dewji amepita na kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa leo.

“Mohammed Dewji ndiye mshindi, maana katika kamati yetu. Hivyo yeye ndiye amekuwa mshindi wa kuwania kuwekeza katika klabu ya Simba. Baada ya mkutano huu kutakuwa na majadiliano,” alisema.

Mkutano huo wa wanachama bado unaendelea Katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.

Kwa hisani ya Saleh Jembe
=======

Wanachama wanazidi kumiminika. Mabadiliko makubwa kutokea

Kaimu rais wa Simba Sports Club Salum Abdallah anawahutubia wanachama waliohudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo unaoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa J.K Nyerere, Dar es Salaam.

Updates

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya kumtafuta mwekezaji Jaji Mstaafu Thomas Mihayo anazungumzia mchakato mzima uliowezesha kumpata mwekezaji katika klabu ya Simba katika Mkutano Mkuu Maalum unaoendelea hivi sasa.

Simba App iko LIVE, unaweza kuangalia kwa ku-Update Simba App yako na moja kwa moja utaweza kufuatailia mkutano huu kupitia simu yako ya mkononi.

24293901_884164975075852_4796277506856014989_n.jpg
 
Apewe tu hamna namna nyingine. Wajanja Wamekula sana pesa yake.

BUT mark my words. Baada ya mwaka au kabla, ataiuza kwa hela ndefu.

Wale wenye timu yao akina Makofia watabakia kupiga kelele tu.
Unaujua mkataba wake na kanuni za TFF kuhusu kuuza timu? Unajua ananunua shea asilimia ngapi na uwezo wake kufanya maamuzi utakuweje
 
Eti ni first club East and Central Afrika kuwa na mfumo huu.
Dah, kazi kweli kweli!
 
View attachment 642938

Wanachama wanazidi kumiminika. Mabadiliko makubwa kutokea

Kaimu rais wa Simba Sports Club Salum Abdallah anawahutubia wanachama waliohudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa klabu hiyo unaoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa J.K Nyerere, Dar es Salaam.

Simba App iko LIVE, unaweza kuangalia kwa ku-Update Simba App yako na moja kwa moja utaweza kufuatailia mkutano huu kupitia simu yako ya mkononi.
Title yako Imeendana vizuri na kilichojiri
 
Back
Top Bottom