Hebu tafakari...
Azam Media wana Mkataba na Yanga wa Billions of TSh kwa MAUDHUI peke yake!!!
Je, unaamini Azam Media hawana akili hadi wawekeze pesa zote hizo kwa ajili ya maudhui peke yake?
Kwavile Yanga na Simba wana almost the same market power, sasa assume Mwamedi angekuwa ndie Mmiliki wa Yanga! Kwamba, anamiliki timu inayokula mkataba wa zaidi Sh 40 Billion (kwa miaka 10) kwa maudhui peke yake!!
Sasa linganisha huo mkataba wa Billion 40 na hiyo Billion 45 inayompa umiliki wa 49% of the club huku bado kila wakati akiendelea kulia lia kwamba anapata hasara!! Hapo hujataja mikataba ya haki za matangazo, uuzaji jezi, mikataba mingine kama ile ya SportsPesa na gharama ambayo angeingia kutangaza bidhaa kama asingekuwa anatumia Brand ya Simba!!