Mo Dewji: Kuwekeza Simba ni hasara, nimeshatoa Bilioni 45

Mo Dewji: Kuwekeza Simba ni hasara, nimeshatoa Bilioni 45

Kwahiyo unaamini kabisa anafanya biashara ya hasara?!

Ikiwa African Lyons ambayo alikuwa anaamiliki kwa 100% aliamua kuipiga bei baada ya kuona hakuna anachopata, sasa kipi kinamfanya aendelee kuingia hasara kwa timu ambayo haimiliki kwa 100% tena huku akikumbwa na masimango kibao?

Btw, tangu lini gate collections ikawa ndo biashara kuu ya soccer club?!
Mimi naamini kabisa kwa sasa anafanya kwa hasara, sema ana expectations fulan in future.

But soon or later you will see my friend
 
Acha fix mkuu, ukiangalia PAYE za Simba kwa mwezi huwezi sema hao jamaa wanalipwa mil 10, 15 au hata 7 kwa mwezi. Acha uongo, watu wanadanganyana sana. Labda wasema wanapata hizo pesa kama posho.
Sijaelewa vizuri hoja yako mkuu, hebu iweke sawa tuelimishane
 
Unataka atoe hela zake alafu akae kimya tu ata kama anaona mambo hayaendi vizuri.au unadhani moo pesa yake haimuumi?.Au hivi simba inavyocheza ovyo unadhani aumii.wewe shabiki ni rahisi kuongea maana huna chakupoteza timu ikifanya vibaya ila mwenzako zile ni pesa kaweka sio kelele zakushangilia.Na sidhani kama hao kina hans pope waliwahi kutoa hata bilioni 2.Tumuache moo aongee ukweli na aonee uchungu pesa zake ili timu ifanye vizuri.kelele za moo ni faida kwa timu ili ijitathimini.Hii misimu yote 4 ambayo simba imemsumbua yanga nikwasababu yanga alikua hana mwekezaji wakueleweka na simba ilikua na Moo.Sasa sitakake kurudi tulikotoka kwasababu mashabiki hamtaki kusikia aliyeweka pesa kipindi chote cha timu inafanya vizuri mnashangilia akiziongelea pesa zake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Ndo hoja yangu na mimi hii
Watu wanabeza tu hawajui uchungu wa kutoa pesa
 
Nadhani wote hamjaelewa intention ya Mo dewji katika kueleza mpk sasa amewekeza Bilioni 45 ktk klabu hiyo

Thamani halisi ya klabu ya Simba Sports ni bei gani?, valuation analysis iliyofanyika mwanzo na yy mwenyewe alisema thamani yake ni bilioni 20 na akajitokeza na hundi ya hiyo pesa kwamba tayari ameshadeposit

Ila kiuhalisia thamani ya klabu ya simba ni zaidi ya Bilion 20,na ndio maana kila siku anaeleza mwanzo niliwekeza Bilion 25 na sasa bilioni 20 imekuwa ni 45.

Hili jambo mtakuja kulielewa zaidi wakati valuation analysis ya Yanga ikifanyika na kuonekana ni kubwa zaidi na wawekezaji wakatokea na kuweka mpunga huo ndo itakuja kuonekana maana ya Mo dewji kusema amewekeza simba Bilion 45 badala ya kutaja zile 20 alizodeposit

Hauwezi ukawa unahesabu pesa za ufadhili ktk timu kwamba ni pesa ambayo ulikuwa unawekeza na wala haikuwa kwenye makubaliano ya uwekezaji ila ni ktk fadhila zako tu kwa timu hiyo ni kama baadae GSM aje aanze kuhesabu na pesa ambazo leo hii ana fadhili ktk timu ya Yanga kama alikuwa amewekeza

Hili mtalielewa zaidi baada ya valuation analysis kufanyika ya klabu ya Yanga
 
Sijaelewa vizuri hoja yako mkuu, hebu iweke sawa tuelimishane
Simba hulipa wachezaji wao kila mwezi, na wakati huo wachezaji hao hulipa kodi (PAYE) kila mwezi, ukiangalia PAYE za klabu na SDL yake, utaona wazi hiyo mishahara mnayoisema hapa haipo. Hakuna mtu pale analipwa mil 15 kwa mwezi hayupo.
 
ebu mwambieni alete risiti au 'transactions' kwa hizo extra 25b alizotumia kwa simba sport club ………..
 
Mimi naamini kabisa kwa sasa anafanya kwa hasara, sema ana expectations fulan in future.

But soon or later you will see my friend
Lakini pia usisahau umesema 40 Billion in 10 Years kwa Mo ni pesa ndogo...

Nakubaliana na wewe kwamba ni pesa ndogo sana kwake lakini hapa hatutakiwi kuangalia ikiwa pesa husika ni kubwa au ndogo bali tunatakiwa kuangalia gharama ambazo clubs zinaingia relative na wanachopata ndipo tujiridhishe kwamba Mo ni mwendo wa hasara kwa kwenda mbele!!

Sasa turudi kwenye hiyo Sh 40 Billion...

Tafsiri yake ni kwamba, kwa mwaka ni 4 Billion... ONLY FROM CONTENT RIGHTS!

Na kwavile Simba wanajigamba wao ni zaidi ya Yanga, basi wanaweza kulipwa hata 50 Billion kwa hiyo miaka 10... which means ni takribani 5 Billions kwa mwaka... ONLY FROM CONTENT RIGHTS.

Azam wameingia mkataba wa matangazo wa Sh 225 Bilioni na TFF kwa miaka 10, ambazo ni zaidi ya 22 Billioni kwa mwaka! Na Simba ni Mdau wa TFF, na kwahiyo hapo ana chake kabla hatuzungumzia uwezekano wake wa kushika nafasi moja kati ya 3 za juu ambazo Bingwa anachukua 500M, na mshindi wa 3 anachukua 225 Million.

Simba pia...

Wana mkataba na SportsPesa....

Wana mkataba na ATCL

Wana Mkataba na nani na nani sijui

Wana mkataba wa jezi...

ZOTE HIZO okoteza okoteza kwa mwaka kisha jumlisha pale kwenye 5 Billions za Contents Right ambazo hadi leo hawajasema wanalipwa ngapi!

Kwa hesabu za haraka haraka hizo ni ZAIDI YA 7 BILLION kwa mwaka!

Sasa Mwamedi anataka kutuambia bajeti ya Simba kwa mwaka ni billion ngapi?

Hivi kwa hadhi ya Simba, yale makorokoro ya Mo yaliyojaa kwenye jezi ya Simba yana thamani ya shilingi ngapi kwa mwaka?! Je, anapotaja hizo billions alizotoa, anazingatia na yake makorokoro yake kwenye jezi?

Hivi hizo billions anazotaja taja kila leo anazitoa kama msaada au anazotoa kama gharama ya kujaza kutangaza bidhaa zake kupitia Simba?

Hizo billions anazotaja anazitoa kama msaada au baadae anakuja kulipa kama wakati ule Yanga wanachekelea pesa za Manji na mwisho wa siku anasema anaidai Yanga zaidi ya 11 Billions?
 
Ingekuwa ni hasara si angeacha kuwekeza. Jezi kaweka mikorokoro kibao alafu anasema hasara?

Twende Kwenye Uhalisia, Simba Inashiriki Michuano Mingapi? Kuweka Jezi Mambo Mengi ni Ishara kuwa Utangazaji wake ni mdogo ndio maana Anataka kuuza Bidhaa nyingi Kwa Wakati Mmoja. Mo kwa sasa Anahitaji Kutangaza Biashara zake kimataifa na sio Tanzania. Tanzania Ushindani wa Kibiashara ni mdogo sana Kulingana na Hali ya Maisha. So hata Asipo Tangaza Mo energy ya 500, Mwananchi wa Kawaida ataulizia Tuu Energy Ya Bei ndogo na Ataipata. Ali Kiba Alikuwa Anatangaza Mo Faya Tanzania Iko Wapi? Lakini Mo Faya South Africa Inafanya Vizuri sanaa. Usione matangazo mengi kwenye Jezi Za Simba Ukadhani Wananufaika. Ni mapenzi na Timu.

Kama Mo Dewdji Asinge anzisha Utaratibu wa Uwekezaji kwenye Mpira, Je mpira wa Tanzania Ungekuwa Wapi? Ndio maana Anatumia Pesa nyingi Kuipush Simba Kwenda Kimataifa ili Baadae aje afaidike na Sio Sasa
 
Mkuu, huu ndio ukweli! Nawashangaa wanaodai MO anapata faida kubwa kwa matangazo.
Tumeona GSM alikuwa anatangaziwa na timu 15,lakini akaona hakuna kitu, na kuamua kumwaga manyanga!

Ingekuwa Tanzania Matangazo yanalipa Sahizi Clouds Isingekuwa Pale Ilipo. TBC Isingekuwa Vile Wala ITV.

ITV ndio Kituo cha Television Ambacho, Kianaongoza kwa Kufuatiliwa katila Habari ya Saa Mbili Usiku. Lakini Nani Kaweka Matangazo pale wakati wa Habari ya Kueleweka? Tanzania Hatujafikia Kwenye Advertisment kwasababu Ya Hali ya Uchumi.
 
Hebu tafakari...

Azam Media wana Mkataba na Yanga wa Billions of TSh kwa MAUDHUI peke yake!!!

Je, unaamini Azam Media hawana akili hadi wawekeze pesa zote hizo kwa ajili ya maudhui peke yake?

Kwavile Yanga na Simba wana almost the same market power, sasa assume Mwamedi angekuwa ndie Mmiliki wa Yanga! Kwamba, anamiliki timu inayokula mkataba wa zaidi Sh 40 Billion (kwa miaka 10) kwa maudhui peke yake!!

Sasa linganisha huo mkataba wa Billion 40 na hiyo Billion 45 inayompa umiliki wa 49% of the club huku bado kila wakati akiendelea kulia lia kwamba anapata hasara!! Hapo hujataja mikataba ya haki za matangazo, uuzaji jezi, mikataba mingine kama ile ya SportsPesa na gharama ambayo angeingia kutangaza bidhaa kama asingekuwa anatumia Brand ya Simba!!

Mkuu Unachanganya Mambo.

Mo dewji anauza Sabuni, Azam Media Anauza Kifurushi na King’amuzi.

Azam Akisema Kuwa Kipindi fulani cha Yanga Kukiona Lazima Ulipie Kifurushi Cha Elfu 10 anategemea Mashabiki wa Yanga na Wapinzani Wake watalipia Onsport ndio maana Faida yake kwake itakuwa kubwa Kuliko Mo Dewji Ambaye Mtumiaji wa Bidhaa Ana uwezo wa Kuchagua Biadhaa nyingi zenye kufanana na Yeye.

Lets Say Sahizi huja Kinga’muzi Cha Azam Utaona Taarifa za Yanga? Ndio maana Azam Alitumia Akili kusema kuwa Hela hizi nitazilipa kila Mwaka. Akiwa na Uhakika wa ku monitor biashara yake.

Mo Dewji kaweka Billioni 20 onsport bila kujua Return yake Itakuwaje. What If Simba Ikashushwa Daraja Sahizi kwasababu Yoyote ile? Ataendelea kupata Faida.

Uwekezaji Wa Azam Media na Mo dewji ni Tofauti kabisa
 
Hujajibu swali la jamaa hapo juu halafu liko wazi kabsa ila naona unalikwepa kwa maksudi. Jamaa kauliza hivi leo hii akitokea mtu anataka kuweka 40B, Mo atakubali kuiachia kwakua anasema anapata hasara kuindesha Simba SC?!

Kwenye Jicho La Kibiashara Anaweza kuichia, unawekaje Billioni 40 kwa Timu Ya Tanzania Utegemee Faida? Mo aliweka billioni 20 bila installment ameiweka kwa Mara moja paaaah

Tofautisha na Muwekezaji ambaye kila Mwaka Atakupa Billioni 3 kwa Miaka 7
 
Bilioni 20 hazijatolewa cash.
Zimetolewa kama faida ya hatifungani, so probably 3-3.5 bil a year kuanzia mwaka huu.
Jumla ni 29bil so far zimeenda kwenye operations ( kiuhalisia).
Simba ingemiliki tu media zake vizuri, ingeweza kuingiza hela hizo katika miaka minne. msipende kujipa unyonge hizi timu zinaweza kuleta faida zikisimamiwa vizuri.
Hata wanachama laki mbili wa Simba wakilipa 30,000 kwa mwaka au 2500/- kwa mwezi wanaipiku hiyo hela.

Watanzania Ambao Maisha Magumu? Wataingia Uwanjani mashabiki elfu 60 lakini wanao Lipia Kadi Utaona ni 100 wenye Uwezo.

Mpira unalipa lakini kwa Tanzania Bado
 
Kama vipi Moo atoke tu ili GSM achukue nafasi ya udhamini.
 
Hii habari umeiona mkuu?? OKW BOBAN SUNZU nakushtua isikupite, najua inauma ila ukweli mchungu.
Mkuu niumie kwa vipi. mimi ni mchumi na mhasibu,nauelewa mkubwa sana kuhusu biashara. Mwekezaji kaeleza changamoto za biashara na kwamba haijaanza kulipa. Lakini ameonyesha nia ya kuendelea kuwekeza angalau kufikia break even point. Kwa nini iwe tatizo
 
Back
Top Bottom