Mo Dewji: Kuwekeza Simba ni hasara, nimeshatoa Bilioni 45

Hakuna mfanyabiashara yeyote mwenye akili anyewekeza mahala anapopata hasara!!! Mo anawafanya mashabiki wa Simba hamnazo; mtakuja kukumbuka maneno ya Kingwangalla!
Mo kaajiriwa Simba SC au yeye Mo ndiye mfadhiri wa Simba SC?
 
Bilioni 20 hazijatolewa cash.
Zimetolewa kama faida ya hatifungani, so probably 3-3.5 bil a year kuanzia mwaka huu.
Jumla ni 29bil so far zimeenda kwenye operations ( kiuhalisia).
Simba ingemiliki tu media zake vizuri, ingeweza kuingiza hela hizo katika miaka minne. msipende kujipa unyonge hizi timu zinaweza kuleta faida zikisimamiwa vizuri.
Hata wanachama laki mbili wa Simba wakilipa 30,000 kwa mwaka au 2500/- kwa mwezi wanaipiku hiyo hela.
 
Mkuu mbona unamkejeli doni wetu
Yule ni muhindi mswahili akinyenyekewa sana atatubuluza yule.kutwa kucha kulalamika anapata hasara na bado yumo sasa hapo anatengeneza picha gani kwa wanasimba?

Marehemu Hans Pope na madoni wengine walikua wakitoa fedha zao za mfukoni kutengeneza mambo pale Simba lakini awakuwai kulalama kama huyu muhindi.
 
Tutamkumbuka sana Hans
 
Moo kwa wenye akili tunajua ilivyovigumu kuwekeza kwenye hizi timu zetu ila mzee endelea kutuvumilia maana kuna mashabiki wa timu flani wanataka ujiondoe ili simba ipitishe bakuli kama wao kipindi kile cha manji alivyoondoka.wasifikiri tumesahau.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Biashara zake si anafanya tanzania au
 
Unataka atoe hela zake alafu akae kimya tu ata kama anaona mambo hayaendi vizuri.au unadhani moo pesa yake haimuumi?.Au hivi simba inavyocheza ovyo unadhani aumii.wewe shabiki ni rahisi kuongea maana huna chakupoteza timu ikifanya vibaya ila mwenzako zile ni pesa kaweka sio kelele zakushangilia.Na sidhani kama hao kina hans pope waliwahi kutoa hata bilioni 2.Tumuache moo aongee ukweli na aonee uchungu pesa zake ili timu ifanye vizuri.kelele za moo ni faida kwa timu ili ijitathimini.Hii misimu yote 4 ambayo simba imemsumbua yanga nikwasababu yanga alikua hana mwekezaji wakueleweka na simba ilikua na Moo.Sasa sitakake kurudi tulikotoka kwasababu mashabiki hamtaki kusikia aliyeweka pesa kipindi chote cha timu inafanya vizuri mnashangilia akiziongelea pesa zake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nyie mvurugeni tu Mo akibwaga manyanga ndo mtaona mtakavosuasua kuendesha timu. Wawekezaji popote pale duniani wanabembelezwa, nyie kutwa kumnanga Mo wakati anatumia hela yake kuendesha timu.

Kwa taarifa yako Bil 40 kwa miaka 10 ni hela kiduchu sana kwa Mo. Kwa kina sie ndo tunaona hela ya maana.

Akisema ukweli mnamnanga, sasa sijui mnataka adanganye ndo mfurahie.

Unaambiwa Gate collection za simba za mwezi mzima hazitoshi kulipa mishahara ya wachezaji. Hali ni hiyo hiyo kwa yanga.

Sasa nyie badala ya kuwabembeleza wawekezaji, kutwa nzima kuwasimanga na hesabu zenu za kinadharia
 
Kwahiyo unaamini kabisa anafanya biashara ya hasara?!

Ikiwa African Lyons ambayo alikuwa anaamiliki kwa 100% aliamua kuipiga bei baada ya kuona hakuna anachopata, sasa kipi kinamfanya aendelee kuingia hasara kwa timu ambayo haimiliki kwa 100% tena huku akikumbwa na masimango kibao?

Btw, tangu lini gate collections ikawa ndo biashara kuu ya soccer club?!
 
Acha fix mkuu, ukiangalia PAYE za Simba kwa mwezi huwezi sema hao jamaa wanalipwa mil 10, 15 au hata 7 kwa mwezi. Acha uongo, watu wanadanganyana sana. Labda wasema wanapata hizo pesa kama posho.
 
Acha tu nikuache kwasababu hujijui kama hujui na yaliyomo ndani ya Simba pia hujui.
hata nikikujuza hapa ntawapa faida Utopolo mahasimu wa Simba wapate pa kuanza zengwe kwa Simba yangu.

Basi yameisha mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…