Mo Dewji na plagiarism kutoka NY Times

Mo Dewji na plagiarism kutoka NY Times

Semilong

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2009
Posts
1,711
Reaction score
220
Juzi juzi mbunge kijana Mohammed Dewji alikuja hapa na article yake juu ya mambo ya umeme. article hiyo inamuonyesha yeye kama amefanya uchunguzi yakinifu kuhusu hili swala la umeme. article hiyo aliitoa kwenye NY times la july 29, 2007 na kui taifsiri kwa kiswahili bila kumnukuu mtengenezaji wa makala hiyo.

Kwakuwa Mo ni kiongozi nimeona ni wajibu kuyaweka haya bayana.

yafuatayo ni artcile ya mohammed dewji kwa kiswahili, article ya michael wines wa NY times kwa kiingereza na link ya hiyo article. unaweza ukaoanisha hizo article mbili kati ya Mo na Michael Wines.
Mambo mengi yamesemwa kuhusu tatizo la umeme nchini Tanzania, mimi nitaanza kwa kugusia mambo machache yanayoonyesha matatizo ya umeme yalivyokuwa makubwa ndani ya bara letu la Afrika:

  • Hatujawekeza ipasavyo kwa miaka 15 hadi 20 katika kitengo cha uzalishaji na usambazaji wa umeme, hayo maneno yalitamkwa na Lawrence Musaba, Meneja wa Southern African Power pool, muungano na mtandao wa nchi kumi na mbili kusini mwa Sahara.
  • Kuanzia Nigeria, Ghana mpaka Luanda hela nyingi inatumika kuzalisha umeme kwa majenereta hali inayofanya uchumi wa nchi nyingi za Afrika kupungua ukuaji kwa asilimia mbili – ripoti ya Benki ya dunia.
  • Ukiitoa nchi ya Afrika Kusini kwenye mambo hayo, nchi zote zilizobaki za kusini mwa jangwa la Sahara lenye watu milioni 700, linapata umeme sawa na wananchi wa Poland ambao ni milioni 38 tu.
  • Eskom, kampuni ya umeme ya Afrika Kusini mwaka 1998 iliambiwa mwaka 2007 itaanza kupata tatizo la mgao wa umeme nchini iwapo isipopanga jinsi ya kuongeza uzalishaji wa nishati, lakini kutokana na matatizo ya fedha na mipango kampuni haikufanyia kazi yale mapendekezo ya wataalamu kwenye ripoti ya mwaka 1998, na kuanzia mwaka 2006 Afrika Kusini imeanza kupata misuko suko ya mgao wa umeme pia.
  • Nigeria, nchi yenye watu wengi kuliko wote Afrika na yenye utajiri wa mafuta ina vituo 79 vya kuzalisha umeme lakini ni vituo 19 vinavyofanya kazi na hivyo kusababisha hasara ya dola za kimarekani bilioni moja kwa mwaka kiuchumi.
Ukienda kuangalia hapo juu ni mifano michache ya matatizo ya umeme barani Afrika, lakini ninachoweza kusema tatizo kubwa linatokana na ukosefu wa mipango. Nishati ya umeme inapatikana kwa njianyingi, kuna umeme wa nguvu za maji, nguvu za jua, kwa njia ya nguvu za upepo, umeme wa majenereta, na njia nyingine nyingi ambazo wataalamu wanaweza wakatuambia zinatufaa.

Ninakaribisha comments wadau na mnakaribishwa kwenye blog yangu

http://www.mohammeddewji.com/blog

MO

"We've had no significant capital injection into generation and transmission, from either the private or public sectors, for 15, maybe 20 years," said Lawrence Musaba, the manager of the Southern African Power Pool, a 12-nation consortium of electricity utilities at the continent's tip.

The implications go beyond candlelight suppers and extra blankets on beds. The lack of reliable power has already begun to hamper the region's development, clipping more than
2 percent off the annual growth rates of the worst-hit African economies, according to the World Bank. Some nations, like Ghana, have tried to deal with their power crises by leasing huge teams of gas generators, producing emergency power at exorbitant rates until power plants can be built.

In Nigeria,
Angola and some other nations, virtually all businesses and many residents run private generators to supplement faltering public service, saddling economies with added costs and worsening pollution.

Excluding South Africa, whose economy and power consumption dwarf other nations', the region's remaining 700 million citizens have access to roughly as much electricity as do the 38 million citizens of Poland.

The government monopoly Eskom, the world's fourth-largest power utility, was advised in a 1998 report that it would run short of power in 2007, but planning and financing problems - not all within the utility's control - stalled upgrades. The forecast was actually optimistic: Eskom began running short in 2006.

Yet South Africa's woes pale beside those of Nigeria, Africa's most populous nation. Only 19 of 79 power plants work, the government said in April. Daily electricity output has plunged 60 percent from its peak, and blackouts cost the economy $1 billion a year, the Council for Renewable Energy in Nigeria says.

http://www.nytimes.com/2007/07/29/world/africa/29power.html?pagewanted=1&_r=1
hii article inapatikana hapa http://www.nytimes.com/2007/07/29/world/africa/29power.html?pagewanted=1&_r=1

plagiarism is a piece of writing that has been copied from someone else and is presented as being your own work (wordnetweb.princeton.edu)
 
Avumaye JF Shy kumbe wengi wapo!...
 
Mkuu mbona utaumiza kichwa chako bure kama issue ni plagiarism, duh! mbona utawapata wengi Tanzania hii?

Kuna mtu yeyote umeshawahi kusikia ameenda jela nchi hii au kapigwa faini kwa sababu ya plagiarism??

I dont support the practise, I surmise you should address as a big problem not pointing MO. kwa sababu tumekua na kulelewa katika hali hiyo kila kitu copying siyo articles tu many things.....

Unaweza kushangaa kabisa watu hawajui plagiarism ni nini mkuu!

I lost 10 marks because of plagiarism in my Msc.degree abroad, kabla ya hapo wakati nasoma degree yangu UDSM sikuwahi kusikia kuwa hili ni tatizo, unakula desa from internet una copy 'onto' na professors wanakupa banda zuri! kabisa.

Start with academician, journalist..... ni janga la kitaifa

It is right time to discuss though
 
Mh Mohammed Dewji tuombe radhi wana JF kwa kutuwekea article hapa bila kusema kuwa umenukuu baadhi ya mambo kutoka kwa mtu mwingine.

Hakika hilo ni kosa kubwa sio kisheria tu bali hata kitaaluma.

Muheshimiwa umetia aibu.
 
Nadhani anachotaka kufanya mwenzetu ni kumtahadharisha mwanachama mwenzetu kuhusu pitfalls za uandishi ili siku nyingine akumbuke ku-cite anakotoa data zake. Lakini ukweli ni kuwa hapa si academia. We are generally more forgiving. Lakini kama ana mawazo ya kujichukulia ka-Ph.D........

Amandla......
 
Msitake kumwonea Dewji. Yeye si wa kwanza na hatakuwa wa mwisho kufanya hivyo. Hapa hatuko chuoni. Si kosa kubwa kama ambavyo unataka kulifanya.

Amandla.......
 
Juzi juzi mbunge kijana mohammed dewji alikuja hapa na article yake juu ya mambo ya umeme. article hiyo inamuonyesha yeye kama amefanya uchunguzi yakinifu kuhusu hili swala la umeme. article hiyo aliitoa kwenye NY times la july 29, 2007 na kui taifsiri kwa kiswahili bila kumnukuu mtengenezaji wa makala hiyo.
kwa ajili Mo ni kiongozi nimeona ni wajibu kuyaweka haya bayana.

yafuatayo ni artcile ya mohammed dewji kwa kiswahili, article ya michael wines wa NY times kwa kiingereza na link ya hiyo article. unaweza ukaoanisha hizo article mbili kati ya mo na michael wines.

hii article inapatikana hapa http://www.nytimes.com/2007/07/29/world/africa/29power.html?pagewanted=1&_r=1

plagiarism is a piece of writing that has been copied from someone else and is presented as being your own work (wordnetweb.princeton.edu)

Thanks Semilong for being a great thinker, you went and do what we all are supposed to be doing, validating sources of info

I just feel bad for Mo kwani sijui alifanya kwa kujisahau au ni kutafuta sifa, usually sisi tunaposimulia kitu tulichosoma sometime tunasahau kutoa source, so i hope Mo will come and say "Yes zile figures nilizitoa kwenye taarifa fulani"

Sasa huyo ni Mo (sijui hata elimu yake), je hao waandishi wa habari ambao baadhi yao sasa wanashinda JF kuchukua taarifa na kuzzita za kichunguzi??
 
Ndugu yangu inawezekana hiyo kazi alimpa mtu amwandalie na kuja kuiweka kwenye mtandao kwa ajili ya kutangaza blogu yake kama sijakosea
 
Ndugu yangu inawezekana hiyo kazi alimpa mtu amwandalie na kuja kuiweka kwenye mtandao kwa ajili ya kutangaza blogu yake kama sijakosea

Shy aisee, hii inawezekana, Duh!!!
 
Thanks Semilong for being a great thinker, you went and do what we all are supposed to be doing, validating sources of info

I just feel bad for Mo kwani sijui alifanya kwa kujisahau au ni kutafuta sifa, usually sisi tunaposimulia kitu tulichosoma sometime tunasahau kutoa source, so i hope Mo will come and say "Yes zile figures nilizitoa kwenye taarifa fulani"

Sasa huyo ni Mo (sijui hata elimu yake), je hao waandishi wa habari ambao baadhi yao sasa wanashinda JF kuchukua taarifa na kuzzita za kichunguzi??

MTM,

Mh. Mo ni msomi mzuri tu,product ya chuo kizuri tu, kwa hiyo asijesema hajui nini maana ya ku-acknowledge sources zake.

Amani.
 
MTM,

Mh. Mo ni msomi mzuri tu,product ya chuo kizuri tu, kwa hiyo asijesema hajui nini maana ya ku-acknowledge sources zake.

Amani.

ndugu bantu kama nilivyosema mimi hapo kabla inawezekana mo alimtumia mwandishi kumwandalia mada hiyo na kuja kuiweka kwa ajili ya kutangaza blogu yake na vitu kama hivyo
 
MTM,

Mh. Mo ni msomi mzuri tu,product ya chuo kizuri tu, kwa hiyo asijesema hajui nini maana ya ku-acknowledge sources zake.

Amani.

Thanks Mkuu, basi nadhani ametuona sie mabwege, ngoja nikarejee ile thread na kuondoa thanks yangu kwanza
 
ndugu bantu kama nilivyosema mimi hapo kabla inawezekana mo alimtumia mwandishi kumwandalia mada hiyo na kuja kuiweka kwa ajili ya kutangaza blogu yake na vitu kama hivyo

Shy,

Kama ndiyo hayo tena basi anakosa umakini katika kazi yake kama kiongozi!, simfundi katika kazi yake bali anapaswa kutambua kwamba alitakiwa afanye uhakiki wa mwisho kabla katibu wake hajaitundika hapa jamvini JF.
 
siamini yaliyopo lakini nakumbuka walianza na Mkewe, mtoto wake, wazazi wake, leo CV, kesho sijui nini

Anyway he is a member and anaweza kuja humu au akawa kama Kikwete na Mbowe - kunyamazia kila kitu

MTN,
Hapa unamzungumzia nani sasa? Mh. Mo ama Mh. dkt Slaa?
 
Hahahaaa, yaani St. George ni pombe kali sana, tena naacha na mirungi kabisaaa

Nimefuka mkuu

Angalia usiende kusaga na wale wasomali mirungi yao ni mikali sana! teh!, teh!, teh!😉
 
Nadhani anachotaka kufanya mwenzetu ni kumtahadharisha mwanachama mwenzetu kuhusu pitfalls za uandishi ili siku nyingine akumbuke ku-cite anakotoa data zake. Lakini ukweli ni kuwa hapa si academia. We are generally more forgiving. Lakini kama ana mawazo ya kujichukulia ka-Ph.D........

Amandla......
sababu ya mimi kuweka hii link sio kumtahadharisha bali ni kumwambia ukweli
ukiisoma ile thread ya mo utazania ni mtu ambaye amefanya uchunguzi wa kutosha kuhusu maswala ya umeme. ukizingatia yeye ni mbunge utajua hizo ni data amezitoa kutoka bungeni.

na alijua akiweka kama vile ilivyo kwa kiingereza watu paste kwenye google na italeta link.

jamaa ametafsiri five paragraph kama zilivyo (verbatim).
 
Back
Top Bottom