Mh. Dewji,
Ninakubaliana na hoja yako, lakini isiishie kusaka umaarufu huku kwenye forums na kwenye blogs. Wewe ni Mwakilishi wetu Bungeni una platform ya kutoa mawazo/maoni na kuihoji serikali kuhusiana na swala zima la tatizo la umeme nchini.
Ombi langu kwako ni moja, chukua hatua ya kushawishi wabunge wenzako ili kuishinikiza serikali ya CCM iachane na hii biashara ya kushughulikia tatizo la umeme kwa njia ya dharura, matokeo yake tunaendelea kuliwa kila siku. Tatizo la umeme lilishakuwa ni mradi wa watu kula tangu ilipoanza IPTL na mwendelezo wa makampuni mengineyo mpaka kwa marehemu Richmond aliyerithiwa na Dowans.
Kwa kuwa wewe ni Mbunge wa CCM basi ni rahisi sana wabunge wenzako wa CCM wakakuelewa kwamba una nia njema, na siyo kile kisingizio kwamba hoja ikitolewa na wapinzani basi inakuwa na lengo la kutafuta umaarufu na siyo kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme.
Nikiangalia umeshuka point za muhimu sana kwenye kuelezea tatizo la umeme Afrika. Hebu jaribu kuandaa hoja binafsi itakayokuwa inaongelea tatizo la umeme Tanzania na jinsi ambavyo nchi imekuwa ikiliwa kuanzia tulipoanza kushughulikia tatizo la umeme kwa njia ya dharura kuanzia enzi za IPTL mpaka zama za marehemu Richmond na mrithi wake Dowans. Onyesha hasara ambazo zinajitokeza kwa kutokuwa na umeme wa kuaminika, onyesha jinsi tunavyoingia mikataba ya ajabu ajabu kwa dharura hizo na hatimaye elezea umuhimu wa umeme ambao reliable kwa ajili ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje, then finally toa mapendekezo ya nini kifanyike ikiwemo hiyo ya kushirikiana na nchi nyingine ama kuangalia uwezekano wa kupata funds kutoka kwa wafadhili ama kuomba mikopo yenye riba nafuu ili tuweze kuwekeza kwenye mradi mmoja mkubwa na tutakuwa tumeagana na tatizo la umeme moja kwa moja.
Kwa njia hiyo utakuwa umetusaidia sana watanzania na utakuwa umechangia pakubwa sana. Haya mambo huwa yanaanza kidogo kidogo na then serikali inaamka toka usingizini na hasa kama ikiona kuna msukumo mkubwa kutoka Bungeni na hasa kama wanaoisukuma ni wabunge wa chama chake, lazima itaona kwamba kuna mahali hapako sawa.
Bado hatujachelewa sana kuna vyanzo vingi sana vya maji ambavyo vinaweza kutumika kuzalisha umeme. Kama swala la ni gharama, bado kuna opportunity ya kushirikiana na nchi za jirani na ikiwezekana kuomba mikopo kutoka kwa wafadhili. Once tukiwa na chanzo cha umeme cha kuaminika, tatizo la umeme litabaki kuwa historia na hakutakuwa na ulaji mwingine wa umeme wa upepo ama sijui akina Dowans hawawezi kuja tena.