MO Dewji: Nataka kuwekeza bilioni 20 Simba

Queen V

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Posts
775
Reaction score
1,332
Mfanyabiashara kijana na mwenye mafanikio makubwa nchini, Mohammed Dewji amesema angependa kuwekeza Simba ili kubadili mfumo.

Dewji maarufu kama “MO”, amewaambia waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo jijini DAr es Salaam kwamba bajeti ya Yanga na ile ya Azam FC ni mara mbili ya ile ya Simba, jambo linaloifanya klabu hiyo kuendelea kubaki kuwa msindikizaji.

Tayari Mo amesema yuko tayari kutoa Sh bilioni 20 ili kununua hisa asilimia 51 na kuwekeza ndani ya Simba.

“Kama unataka mafanikio kwenye mpira, hakuna zaidi ya fedha. Simba haiwezi kuwa na miaka 80 leo haina hata uwanja wa mazoezi.

“Unajua kama nikiwekeza fedha hizo, tunaweza kuzipeleka kwenye mkopo na kuikopesha serikali. Baada ya hapo tutapata faida ya dola bilioni 7.5 ambazo tutaziingiza kwenye maendeleo.

“Mimi ninaamini Simba haiwezi kubadilika kwa kuwekeza kwenye bajeti ya Sh milioni 500 kwa mwaka. Haitawezekana, ndiyo maana nimekuwa nikisisitiza, kwanza Simba inahitaji muwekezaji na si mdhamini.

“Nisisitize hili,mimi ni mwanachama wa Simba, ninaumia kuona timu hii inakwenda hivi. Ndiyo maana ninaingia nikiamini nitaweza kubadilisha mambo kwa kushirikiana na wanachama wa Simba ili kuleta mabadiliko katika klabu yetu.”
 
Maslahi ya wakomandoo wahakikishie tu Mo mbona wanakubali tu,hapo kina washinda maslahi yao yatakuwa wapi?
 
Yupo sahihi, maana simba imekuwa kama chapati mpka uigeuze upande wa pili ndyo iwe tayari kuliwa

Karb mo, ila ujue fedha ni hoja moja masilahi ya tim ni hoja ya pili, fanya kama alivyo fanya manji, ukijifunza kwake utafanikiwa...
 
Eti ni "kama chapati mpaka uigeuze upande wa pili ndo iwe tayari kuliwa"[emoji23] [emoji23] [emoji23] yaani watu mna maneno nyie. Mimi imenibidi nihame hilo chama kangu sasa ivi ni mshabiki wa Panone fc[emoji5] [emoji5]
 
Simba ni club ambayo ni association ambayo ni mali ya wanachama na sii kampuni mtu ajitokeze kununua hisa. Ila ndani ya klabu inaweza kuanzisha a subsidiary public company ya SSCC isajiliwe kama Public Company ifanye IPO ya 51% stake ya hiyo IPO ndio issued kwa MO kwa hizo bilioni 20 zake halafu ile 49 stake inabaki kwa wanachama. Vinginevyo katiba ya SSC ibadilishwe kutoka club iwe kampuni, na hizo shares ziwe floated kwa public MO azinunue kama deserving na sio kuuziwa kwa preferential.
pasco
 
Kweli kila mtu na fani yake.
Yaani umeandika kwa kiswahili lakini bado nimetoka kapa!.
 
Eti ni "kama chapati mpaka uigeuze upande wa pili ndo iwe tayari kuliwa"[emoji23] [emoji23] [emoji23] yaani watu mna maneno nyie. Mimi imenibidi nihame hilo chama kangu sasa ivi ni mshabiki wa Panone fc[emoji5] [emoji5]
Soka si kama mpz? Kwamba akikuchosha mnaachana, ni mapz, ndyo maan mo anahagaika na kupatia mafanikio, yule wa azam yy hakiwa hvyo alianzia chini, manji si mwana michezo ila kapewa kiki na ugomvi wake na manji...

Na ki ukwel amefanikiwa
 
P
Hlo jambo haliwezi kuwa, may b wanachama wote wa simba wabadili iq zao, maana kuna watu hapo wanaitumia club kuendesha familia.. Unafikr hlo jambo litawezekana?
 
Soka si kama mpz? Kwamba akikuchosha mnaachana, ni mapz, ndyo maan mo anahagaika na kupatia mafanikio, yule wa azam yy hakiwa hvyo alianzia chini, manji si mwana michezo ila kapewa kiki na ugomvi wake na manji...

Na ki ukwel amefanikiwa
Na ni kweli mkuu wakifanya kununua hisa hivyo itahamasisha hata matajiri wengine wawaze nao kuwekeza kwenye soka katika vilabu vinginevyo vya mikoani. Hiyo inaweza leta ushindani mkubwa wa kiteam na kufanya mpira wa tz kupiga hatua tofauti na ilivyo sasa leage imekuwa kama leage ya mkoa wa dar. Itafanya kuwa na hela sasa na team nyingine kujua zaidi ya pale zilipodumalia, maana toka nimepata akili sasa team nyingine zilichukua makombe ni chache sana. Mara nyingi ni Simba ama Yanga, Wazee wa team nao wanaharibu mpira nahisi nacho hicho kitu kitaondoka sasa.
 
asilimia 51? kwani simba ni kampuni? nani anamiliki leo na ni kwa asilimia ngapi?

sielewi hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…