MO Dewji: Nataka kuwekeza bilioni 20 Simba

Apewe tu ila sijaelewa mahesabu ya kukopesha serikali na kupata dollar 7.5million kama faida,na iyo faida wakishaikopesha serikali watapata faida kwa muda gani?
 
Mo ! Hii si mara ya kwanza kuonesha dhamira hii.Bahati mbaya itamchukua muda sana wenye klabu kulielewa hili somo. Pia ningemshauri anunue klabu nyingine awekeze ,ikifanya vizuri washabiki tutakuja tu.Hata mwenye Azam nadhani aliwahi waza kama yeye ikambidi aanze kivyake! Asisahau wale makomandoo wataishije?!
 
Mo Dewji nia yako ni njema lakini kuna mahafidhina hapo Simba hawataki kusikia hizo habari zako.Hao ni wale ambao wanataka mambo yawe kama yalivyo ili waendelee kuchuma kwa mgongo wa Simba.Hao hawaamini timu kuandaliwa kisayansi bali 'kamati ya ufundi' chini ya wazee.
Evans Aveva na sekretarieti yako wapeni elimu wanasimba.Waambieni nyakati zimebadilika.
 
aje tumpe coastal union kwani lazima abembelezane na hao mikia?
 
Mbona mabilionea uko ulaya wananunua timu? ? Si mnaiona Chelsea inafanya vizuri chini ya bilionea wa kirusi abramovic. ..
 
Jamani kwanini hapewi huyu mtu simbayetu!!
naamini atatusaidia sana
Why Simba? Huyu jamaa si alikuwa na club yake - sijui iliitwa "leon"? Ilimshinda? Why asianze kama Bakhresa na Azam? Ameona nini?
 
Lengo haliwezi kufikiwa katika mfumo we sasa. Lazima katiba ya club ibadilike Kwanza. Toka club ya wanachama iwe kampuni ili watu wamiliki hisa.
Mo anaitaka Simba kama bidhaa nyingine yoyote!
 
Hapo chacha Mkuu! Ajabu hilo!
Ametoa utetezi kua, Aliachana na African Lyon, sababu alienda uwanjani akakuta Timu haina mashabiki, mbona AZAM imeweza, imepata wapi mashabiki.. Anatikiwa kujichunguza zaid
 
Mi siku hizi nimeacha kufuatilia soka la bongo kutokana na simba kufungwafungwa tu. Hao viongozi wakikataa hilo pendekezo wajue kuwa na kipato chao kitazidi kushuka kwa sababu mashabiki tumeshaacha kwenda viwanjani kuishuhudia hiyo club. Mpeni MO hiyo timu.
 
Mpeni timu Mo,tumechoka kuwaona ka kakundi flani hivi ka ushangiliaji ambako hakana timu maalum ya kushangilia,tunakoenda mtashindwa tena kushangilia maana Mwigulu atawaparula
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…