Mo dewji: Nimepoteza billion 41 ndani ya Simba

BILIONEA Mohamed Dewji Mo amethibitisha rasmi kuwa Klabu ya Simba aliinunua miaka 5 iliyopita na ndio kitu cha gharama kwake kukinunua[emoji3578]

#KitengeSports

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
""Inachanganya hii, kitu ukishakinunua si ni chako, sasa utakiachiaje bure bure, aidha aseme amemuuzia nani sasa maana ni mali yake hii simba ""
 
Mim ni simba ,,ila ndio umfananishe gsm na hii takataka? Lugha ya kusema nimeppoteza mana yake ni wewe ni kama unalazimishwa kua simba na zaidi haujatoa fedha kwa mapenz yako, umetoa ukiwa na kinyongo, au kama sabab sio hii bas ni njia ya danganya toto kwa wanasimba na viongozi ili waone umetumia hela nyingi ili uendelee kuwa simba na kujinufaisha bila kua na mapenz yoyote na klabu kuiona inakua klab bora afrika..
 
Simba ndiyo kitu pekee cha gharama alichowahi kukinunua tajiri Mohammed Dewji.. Najivunia kuwa mshabiki wa Yanga isiyonunuliwa. Pole nyingi ziwaendee wanaume wanaonunuliwa kirahisi rahisi na mwanaume.
 
Mo anazingua na ni mmoja wa watu wanaofanya wanasimba kuishi kinyonge pamoja na mafanikio ya timu inayoyapata.

Klabu imepoteza mwelekeo wa kiutawala na kiuongozi na ndiyo msingi wa matatizo mengi ya timu.
 
Basi nitakua sijaelewa..nilikua nimeelewa kuwa wewe haupo ktk group la kupigania ile 51% uko ktk wale wa simba inashinda mie poa tu
Hapana. Mgawanyo wa umiliki wa timu ni suala nyeti sana, siwezi kuwa wale wa "timu inashinda poa tu" kama vibaraka wa GSM.

Nilichotaka kusema ni kama nilivyoandika, kuwa ana mchango fulani katika kuleta mafanikio ambayo Simba imeyapata kwa kipindi hivi kifupi kwa hiyo siyo mtu wa kumbeza.

Kuhusu ishu ya umiliki hadi matangazo yake hayo ni mambo mengine. Nina mengi ya kusema kuhusu hayo ila sidhani kama muda ni muafaka kuyasema ila yeye kila wakati Simba ikiwa inakaribia hatua fulani kuja na hivi viinterview vyake vya "kupoteza pesa" inaleta picha mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…