Kwamba yupo tayari kufilisika kisa Simba
Si ndo hapo??
Hii ni trick ya kishamba sana,, kwamba kila simba inapata kitu flani (kizuri au kibaya), ye anajitokeza na kutangaza pesa alizowekeza. Anafanya hivi kwa maelngo mawili tu kwa maoni yangu.
1. Lengo la kwanza ni kutafuta kutukuzwa aonekane amejitolea sana na anastahili pongezi na si lawama.
Mifano ni mingi hapa nitatoa michache, mwaka 2020, Simba ilipofungwa na Mtibwa kwenye fainali ya mapinduzi cup, aliingia twitter akatangaza pesa alizotumia kusajili na kulipa mishahara kisha akajiuzulu then kesho yake wakamlamba miguu akaahirisha kujiuzulu, huku akiwa na uhakika kwamba hatopata lawama kwa ie failure ya mapinduzi.
Mwanzoni mwa msimu huu. ilivyoonekana kwamba Simba imesajili wachezaji wengi wabovu yeye alitokea tena kwenye mtandao wa X (twitter) akasema mara hii ametoa B 3 so mtu asiseme Mo hajatoa hela. Lengo ni kujiweka pembeni kutokana na lawama za kusajili wachezaji magalasa wa bei chee.
2. Lengo la pili ni anatengeneza mazingira asiulizwe faida anayoipata kwa uwekezaji wake hapo Simba. Ndo maana mara zote amekua hodari wa kutangaza hasara anayoipata ili ionekane hafaidiki. Lakini swali la kujiuliza ni inakuaje mfanyabiashara aliyefanikiwa kama yeye aendelee kuikumbatia biashara inayompa hasara kama aliyoitangaza kwa miaka 5 mfululizo bila kuiacha? Hadi hapo alipo, ameziacha biashara ngapi ambazo aliona zinampa hasara? Kwanini Simba impe hasara na aendelee kuing'ang'ania?
Pia kama anakubali hasara labda kutokana na mapenzi yake kwa simba, kwanini haishi kulalamika kwenye media kuhusu hasara anayopata. Si apate hasara kimyakimya tu coz anatimiza mapenzi yake kwa klabu anayoipenda?
Mbona tangu alipoiacha mwaka 2003 hadi mabadiliko yalipofanyika 2017 timu ilikua inaendeshwa kwa pesa za HansPope na mzee Hanspope hakuwahi kwenda kulalamika hasara kwenye media yoyote nchini?
Huyu jamaa anatuchukuliaje sisi watz?