Mo dewji: Nimepoteza billion 41 ndani ya Simba

Mo dewji: Nimepoteza billion 41 ndani ya Simba

Kugharamia Timu sio hela ndogo na ukichanganya na wapigaji wanaoongeza sifuri kwa bei za Wachezaji ndio kabisaa itafika 100 B katibuni tu..
 
Mim ni simba ,,ila ndio umfananishe gsm na hii takataka? Lugha ya kusema nimeppoteza mana yake ni wewe ni kama unalazimishwa kua simba na zaidi haujatoa fedha kwa mapenz yako, umetoa ukiwa na kinyongo, au kama sabab sio hii bas ni njia ya danganya toto kwa wanasimba na viongozi ili waone umetumia hela nyingi ili uendelee kuwa simba na kujinufaisha bila kua na mapenz yoyote na klabu kuiona inakua klab bora afrika..
Ni kweli alilazimishwa na Makonda kipindi kile Simba imepoteza kwenye FAINALI ya Mapinduzi.
Aliambiwa mara ile tumekuvalisha kanga safari hii tunakuvisha bikini na picha juu.

Kama ingekuwa ni wewe si ingekubidi uwe mpole tu?
 
Ni kweli alilazimishwa na Makonda kipindi kile Simba imepoteza kwenye FAINALI ya Mapinduzi.
Aliambiwa mara ile tumekuvalisha kanga safari hii tunakuvisha bikini na picha juu.

Kama ingekuwa ni wewe si ingekubidi uwe mpole tu?
Makonda ana dhambi nyingi sana
 
“Nadhani kitu ghali zaidi nilichowahi kununua ni klabu ya mpira inaitwa Simba ina mashabiki milioni 35, niliinunua hii klabu miaka mitano iliyopita, nimepoteza takribani Dola za marekani milioni 4 (Tsh bilioni 10.2) kwa mwaka mmoja na kwa miaka yote mitano nimepoteza Dola za Marekani milioni 20 (Tsh bilioni 51)"

Rais wa Heshima na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji akizungumza kwenye Podcast ya Ahmed Mahmood.

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
Ufala mkubwa, hawa umbwa wana washabiki 35m yaani zaidi ya asilimia 60 ya watz ni ujinga mkubwa.
 
Si ndo hapo??
Hii ni trick ya kishamba sana,, kwamba kila simba inapata kitu flani (kizuri au kibaya), ye anajitokeza na kutangaza pesa alizowekeza. Anafanya hivi kwa maelngo mawili tu kwa maoni yangu.

1. Lengo la kwanza ni kutafuta kutukuzwa aonekane amejitolea sana na anastahili pongezi na si lawama.

Mifano ni mingi hapa nitatoa michache, mwaka 2020, Simba ilipofungwa na Mtibwa kwenye fainali ya mapinduzi cup, aliingia twitter akatangaza pesa alizotumia kusajili na kulipa mishahara kisha akajiuzulu then kesho yake wakamlamba miguu akaahirisha kujiuzulu, huku akiwa na uhakika kwamba hatopata lawama kwa ie failure ya mapinduzi.

Mwanzoni mwa msimu huu. ilivyoonekana kwamba Simba imesajili wachezaji wengi wabovu yeye alitokea tena kwenye mtandao wa X (twitter) akasema mara hii ametoa B 3 so mtu asiseme Mo hajatoa hela. Lengo ni kujiweka pembeni kutokana na lawama za kusajili wachezaji magalasa wa bei chee.

2. Lengo la pili ni anatengeneza mazingira asiulizwe faida anayoipata kwa uwekezaji wake hapo Simba. Ndo maana mara zote amekua hodari wa kutangaza hasara anayoipata ili ionekane hafaidiki. Lakini swali la kujiuliza ni inakuaje mfanyabiashara aliyefanikiwa kama yeye aendelee kuikumbatia biashara inayompa hasara kama aliyoitangaza kwa miaka 5 mfululizo bila kuiacha? Hadi hapo alipo, ameziacha biashara ngapi ambazo aliona zinampa hasara? Kwanini Simba impe hasara na aendelee kuing'ang'ania?
Pia kama anakubali hasara labda kutokana na mapenzi yake kwa simba, kwanini haishi kulalamika kwenye media kuhusu hasara anayopata. Si apate hasara kimyakimya tu coz anatimiza mapenzi yake kwa klabu anayoipenda?
Mbona tangu alipoiacha mwaka 2003 hadi mabadiliko yalipofanyika 2017 timu ilikua inaendeshwa kwa pesa za HansPope na mzee Hanspope hakuwahi kwenda kulalamika hasara kwenye media yoyote nchini?
Huyu jamaa anatuchukuliaje sisi watz?

Na la 3. Ili aendelee kutangaza biashara zake zinazompa faida kupitia platform za Simba. Kumbuka alishasema biashara inayompa faida sana kwa sasa ni mo energy. Sasa bila ya kina boko kubeba chupa na kuzitangaza atamuuzia nani? Maana anajua fika kwamba Azam amewekeza sana kwenye biashara ya TV. Ukienda kenya karibia yote, Uganda, Msumbuji Rwanda etc Azam TV yupo huko na vinjwaji hvyo vinauzika sana. Sasa anajificha kwenye kichaka cha hasara ili asipate kubughidhiwa.
 
Ufala mkubwa, hawa umbwa wana washabiki 35m yaani zaidi ya asilimia 60 ya watz ni ujinga mkubwa.
Tumia akili mashabiki wa simba wengine wako diaspora .wengine sio watanzania
Screenshot_20240229-204028_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom