Mo na GSM mnazijua hesabu za mlinganyo?

Mo na GSM mnazijua hesabu za mlinganyo?

Naona msimu huu kulingana na Yanga ilivyo chukua makombe na kujiongezea thamani, Yanga hawakutaka kukubali kuendelea na mkataba ule wa mwaka jana. Wame force mpaka wameongezewa dau kutoka 1300 ambayo walikuwa wanachukua mwaka jana mpaka 1350
Hiyo ndio thamani halisi ya Club kubwa
Sasa sh. 50/= kwa kila jezi ni ongezeko gani hapo? Tatizo anayedhamini klabu ndiye anayeiongoza
 
Mbumbumbu haya mambo ni mazito kwao anajua kwa kuwa mbet kaweka 26 basi mo ilitakiwa aweke 26*3 (kila tangazo alipie 26)
Eewaaa!! Kwani wenye Simba hawana uwezo wa ku negotiate na wafanyabiasha? Mbona mo na GSM wanapata mikataba minono kwa wafanyabiasha wenzao? Wenye Mali tunakwama wapi?
 
Zitangazwe kama vile m bet, sportpesa, Azam na NBC walivyotangaza na kutangazwa mbele ya camera. Kwanini unataka twende TUka Google kujua wanalipa bei gani? mbona wanasema wanapata hasara tyuuu?
pamoja na kupewa angalizo lakini bado unapuyanga tu. Unataka wakutangazie wewe au umma. Maana kama umma ulishatangaziwa,kama hukusikia wakusaidieje?
 
Sio kila hoja inajadiliwa kishabiki Gsm anawalipa yanga 1350 Kwa kila jezi anayouza mo hataki mikataba ya Bei ndogo sio kosa kuhoji yeye analipia shilingi ngapi?
Anataka hela nyingi kutoka kwa wadhamini wengine lakini yeye katoa hela mbuzi kwa Simba. Huu ni uzembe wa wamiliki wa timu hizi kubwa mbili. Uwezo wa ku bargain hatuna.
 
Huyo ni mtopolo wa kutupwa. Ndo ujue sasa kwamba Mashabiki wa utopolo wengi wao ni hamnazo

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Yani kukwambia Simba inaibiwa na manyang'au ni uhamnazo? yaani yeye anavuta hela kibao kutoka m-bet, NBC, Azam, TBC kwa matangazo lakini yeye anatangaza bidhaa zake bure chee.
 
Mikataba ya kinyonyaji uzuzu kabisa hii. Tena mtu analalama eti anapata hasara wakati amejaza matangazo yake kwenye jezi, anauza wachezaji, anapata get collection na anauza jezi, wakati sportpesa/m-bet, NBC, Azam wanaishia matangazo TU baaasi na wameridhika na faida wanapata
YAANI MWANANGU ACHA TU
 
pamoja na kupewa angalizo lakini bado unapuyanga tu. Unataka wakutangazie wewe au umma. Maana kama umma ulishatangaziwa,kama hukusikia wakusaidieje?
Kama ni tangazo basi lilikuwa ni tangazo la kifo Cha club. Maana nimesikia mtu mmoja alitangaza kuimiliki 49% ya timu milele kwa 20b TU, ambazo hata hivyo hazijulikani ziko bank ipi, wakati m-bet hata bila kumiliki hata 1% tu ya timu katoa 26b (kama ni kweli).

Yuko jamaa mmoja aliomba kuikodisha timu kwa miaka 10 tu basi na kuirudisha. Jamani watanzania amkeni amkeni bwanaa!!
 
Back
Top Bottom