Mo usichanganye Simba na CCM wala Magufuli

Sijijui

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
7,877
Reaction score
8,804
Wanajamvi

Hivi hakuna mtu anayeweza kumsaidia Mo kuelewa kuwa Kuna tofauti ya Simba na CCM, Je Mo anadhani yeye kuwa mwanaccm ndo wanasimba wote tumekuwa wanaccm na washabiki wa Magufuli?

Kwamba Mo hana uwezo wa kutofautisha tamasha la Simba na tamasha la CCM? Mwambieni anaboa kutuletea uccm wake kwenye burudani zetu.
 
Hakika tamasha limependeza saana. Doa pekee ni pale mdosi (MO ambaye ndiye Muwekezaji mkuu wa Club ya Simba) kama kawaida yao (wadosi) na heshima ya unafiki na uwoga alipotaka kuleta siasa wakati akimtambulisha mgeni rasmi Mh. Zungu (aliyekuwa Mbunge wa Ilala CCM) kwa kumfanyia kampeni na kama haitoshi akaendelea kwa kumfanyia pia kampeni Rais Magufuli.

Lakini kwa kuwa washabiki wengi wa Simba ni watu makini na wasioendekeza upuuzi wa ugabochori wakampa za uso kwa kumchunia pale aliposema Magufuri oyeeee.

Kama ana akili atakuwa amenyooka kwani inaoneka baada ya kupigwa "spana" katika hizi siku mbili zilizopita kuhusu wapi zilipo 20bil alizotakiwa kulipa kabla kuinunua Simba na sio baada ya kuanza kunufaika na Simba inaonekana amekuwa akitafuta kila aina ya "Platform" ya kumuunga mkono hasa mamlaka za juu kwa kujipendekeza ili kuweka mambo yake sawa
 
Unataka kuwa na Sauti na hauna pesa?
Ndo ashafanya ukitaka kufa, au lia.
Nyie wabongo kila kitu mnalalamika, kama wewe moyoni mwako una chama chako, mtu akikitaja chama kingine wewe inakubadilisha nini?
Utabaki kuwa vile vile tu hata akitaje Mara mia.
 
Kiukweli sasa hivi bila kutaja maneno hayo ni kama kula bila kumuomba Mungu, tunakoelekea hata wenzi wetu wataambiwa waseme no kama hujataja maneno hayo.
Hii imekua too much,nidhamu ya uoga imezidi
 
MO ndio aache ujinga, Pale Uwanjani wanaingia Mashabiki wa Vyama mbalimbali ambao pia ni Simba. Ajue tu kua Simba sio ya CCM. Tena kwa wengine tulioko Simba tunaichuklia Yanga kama CCM sababu ya mfanano wa Jezi. Asituchanganyie habari
Yanga ni timu ya wananchi na siyo ya CCM kwa nini uichukie wakati zile ni rangi tu .
 
Mo Aache ujinga wake kabisa.

Ndio maana tuliamua kukaa kimya bila kupunga mikono.


Nadhan na Gambe alilopiga limechangia sana.


Simba sio CCM .
 
Nyie watu wa dizaini yenu mko tayari kuuza hata utu wenu almradi tu mmeona pesa Haya kufa wewe utaletewa pesa huko makao mapya.
 
Mo sio mjinga anajua ili afanye biashara zake vizuri lazima awe karibu na serikali, wakina Rostam na Lowassa wamesalimu amri ili kulinda maslahi yao
 
Simba wote wameelekezwa na Mo wawe wanachama wa CCM.

Kama mtu hataki ahamie Lipuli.
Kama CCM wanataka waanzishe timu yao na dini yao siyo kutuletea siasa kwenye mpira , tunapokuwa kwenye mpira tusichanganyiwe na ulevi wa siasa , mpira ni ulevi tosha halafu mtu mwingine alete siasa zake , aangalie majukwaa ya siasa ndiyo mahali pake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…