Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Maisha ya hapa duniani ni kupambana ili kuweza kumudu mahitaji yako ya kila siku. Na ili ufanikiwe inabidi kuweka aibu chini na kupambana kwa juhudi na maarifa ili kuweza kutimiza ndoto zako. Kuna hii biashara ya nyama choma, ambayo ukiifanya vizuri inaweza ikakutoa sehemu moja kwenda nyingine. Unaweza ukaanza hivi:-
Ainisha maeneo yote ya kufanyia hii biashara
Inaweza kuwa maeneo ya msongamano wa watu au sehemu ya vituo ambapo abiria wanasubiri usafiri;njia panda, Sehemu ya kona ya barabara, minadani, sokoni, vituo vya daladala, maeneo ya ujenzi n.k
Jiko
Tengeneza toroli la matairi linaloweza kufunguka kama jiko
Mwamvuli
Tafuta mwamvuli mkubwa kwa ajili ya kuzuia jua,unaweza kuwaomba mafundi wa maturubali wakutengeneze.
Nyama na viungo
Nunua nyama nzuri na viungo vya kumshawishi mteja,ili ule moshi utakapomfikia mtu yeyote aanze kujisachi mfukoni kama kuna fedha ya ziada aweze kula bidhaa yako.
Vaa mavazi ya kuvutia na safi
Unaweza kuvaa pensi, suruali ya jinsi au kadeti,tisheti safi,kofia,na viatu vya wazi ili kuwaaminisha walaji wako unajali afya zao.
Vifungashio
Tafuta vifungashio kwa ajili ya wateja, inaweza kuwa foili, mfuko wa karatasi, au aina yoyote utakayobuni na kumshawishi mteja.
Anza kazi
Anza kazi kwa ujasiri, na uanze kupiga hela; mafanikio yakianza kupatikana fungua matawi mengi hata yafike 500 kama utaweza.
Hitimisho
Biashara hii anaweza kufanya mtu yeyote haijalishi una kiwango gani cha elimu
Nb: Maisha ni pesa