Model gani ya noah ni imara na madhubuti kwa rough road

ATA

Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
84
Reaction score
22
wakuu, habari zenu!
Naomba kufahamishwa ni model gani ya gari aina ya Noah imara na madhubuti kwa 'rough road'. maana niko kwenye mchakato wa kununua.
Michango yenu ni muhimu sana kwangu kufanya maamuzi sahihi.
Natanguliza shukrani.
 
Ni Townace Noah au Liteace Noah. Mie ninayo Liteace Noah na ninafanya nayo root za off road na haina shida.
 
nunua kitu road tourer unesenese

Nijuavyo "mimi" ni kwamba hakuna aina ya noah inayoitwa Road tourer au field tourer. Ila hayo majina yapo tu kwenye sticker kwa zilezile townace noah, liteace noah na noah yenyewe. Kwa hiyo kwa mujibu wa swali la mwana jamvi kuwa ni "model" gani imara na madhubuti, nadhani jibu lingetoka kwenye moja kati ya hizi:
1. Noah
2. Townace Noah
3. Liteace Noah
 
Ahsante mkuu kwa ufafanuzi wako. Wakuu ushauri wenu ni muhimu sana kwangu, naomba muendelee kunipa maarifa zaidi kwa ajili ya uchaguzi sahihi.
 
Townace Noah.......ndo yenyewe ile ujue ni plastic tu ukikutana na kitu SCANIA ujue utachanwa mpaka utumbo
 
mkuu karibu uniuwe kwa kucheka...SCANIA hata kama una land rover 109 lazima ufanywe nyama ya kusaga...
 
Ahsante mkuu, kwa mwaka 1996 ni mbali kidogo

Ngoja nikupe siri! Ni bora ukanunua Townace/Liteace noah ya 1996 kuliko noah mayai ya 2007. Hizo gari ni imara usipime, chunguza hata zinazotumika kwa biashara ya abiria utakuta ndo zenyewe tupu na hii ni kwa sababu zinastahimili. Yangu mimi ni 1998.
 
Nafunga mjadala sasa ni wewe kufanya maamuzi.
Townace/Liteace noah hizi ndio gari za kazi
Ukitaka za kuchukulia madem na wake za watu nunua hizo Mayai za kuanzia mwaka 2000.
 
Mleta mada, ushauri aliokupa Konzogwe ndio ambao ningekupa. Noah za 1996-1999/2000 ndio zifaazo kwa rough road. Za kuanzia 2002 ndio hizi mayai. Ziache
 
Last edited by a moderator:
Nunua Noah ya 1996-2000 ingine 3s,zipo za diesel ingine 3c kama una fundi mzuri hazichanganyi haraka,Ukipata Noah yenye chata Super Extra Limo very powerful na mafuta inatumia nzuri.
 
Nafunga mjadala sasa ni wewe kufanya maamuzi.
Townace/Liteace noah hizi ndio gari za kazi
Ukitaka za kuchukulia madem na wake za watu nunua hizo Mayai za kuanzia mwaka 2000.

Mkuu Zanzibar Spices, ahsante kwa ushauri wako, nami pia sasa nakaribia kufanya maamuzi, lakini niulize tena kidogo kati ya hizo mbili yaani Townace na Liteace ipi ni bora na imara kwa barabara za vumbi.
 
Zote ziko sawa kabisa hamna tofauti labda majina yake tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…