Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wakuu, habari zenu!
Naomba kufahamishwa ni model gani ya gari aina ya Noah imara na madhubuti kwa 'rough road'. maana niko kwenye mchakato wa kununua.
Michango yenu ni muhimu sana kwangu kufanya maamuzi sahihi.
Natanguliza shukrani.
ni townace noah au liteace noah. Mie ninayo liteace noah na ninafanya nayo root za off road na haina shida.
nunua kitu road tourer unesenese
nunua kitu road tourer unesenese
Nijuavyo "mimi" ni kwamba hakuna aina ya noah inayoitwa Road tourer au field tourer. Ila hayo majina yapo tu kwenye sticker kwa zilezile townace noah, liteace noah na noah yenyewe. Kwa hiyo kwa mujibu wa swali la mwana jamvi kuwa ni "model" gani imara na madhubuti, nadhani jibu lingetoka kwenye moja kati ya hizi:
1. Noah
2. Townace Noah
3. Liteace Noah
Townace Noah.......ndo yenyewe ile ujue ni plastic tu ukikutana na kitu SCANIA ujue utachanwa mpaka utumbo
mimi ninayo mkuu ya 1996 ni roho ya paka kwa kweli....
mkuu karibu uniuwe kwa kucheka...SCANIA hata kama una land rover 109 lazima ufanywe nyama ya kusaga...
Ahsante mkuu, kwa mwaka 1996 ni mbali kidogo
Nafunga mjadala sasa ni wewe kufanya maamuzi.
Townace/Liteace noah hizi ndio gari za kazi
Ukitaka za kuchukulia madem na wake za watu nunua hizo Mayai za kuanzia mwaka 2000.
Mkuu Zanzibar Spices, ahsante kwa ushauri wako, nami pia sasa nakaribia kufanya maamuzi, lakini niulize tena kidogo kati ya hizo mbili yaani Townace na Liteace ipi ni bora na imara kwa barabara za vumbi.
mimi ninayo mkuu ya 1996 ni roho ya paka kwa kweli....