Mohamed Dewji kuinunua Simba

Mohamed Dewji kuinunua Simba

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohammed Dewji ameweka wazi mpango wake wa kuinunua klabu ya Simba inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara.

Akizungumza na kipindi cha Mkasi TV kinachoruka kupitia EATV, Dewji alisema tayari wapo kwenye mazungumzo na rais wa klabu hiyo ili kukamilisha mpango huo.

"Unajua kila mtu ana interest, hakuna interest ya klabu, mimi nimeona sitaki nijihusishe na klabu ambayo haitafanikiwa, ndio maana mimi nilikuwa nasema Azam itakuja kufanya vizuri zaidi kuliko Simba na Yanga na wameanza," alisema.

"Nimeongea na rais wa Simba na ameniambia nimwandikie paper. Unajua mimi nimemwambia ‘wewe unafikiria mimi nikinunua hisa 51% ya Simba, maana yake nitaipeleka wapi? Mimi ni mtu wa hapa hapa na naipenda Simba. Leo mashabiki wa Manchester United, Arsenal they don't care klabu ya nani, wanachohitaji ni mafanikio.

Mimi nimewaambia nipo tayari niwekeze bilioni 20. Leo Katumbi wa TP Mazembe ni timu yake na inafanya vizuri. Mimi nimewaambia hata nikiwekeza bilioni 20 sitaona hela, mimi na biashara mia nyingine ninapata hela.

Kwenye mpira ni mapenzi na timu basi. Tunataka kuendeleza mpira tuendeleze Simba yetu, tupate raha Simba ikishinda. Tayari nimeshamwandikia paper sasa tunakamilisha tutapeleka kama tutafanikiwa, kama ilishindika nitaanza na Mo Football Club," aliongeza Mo.

Aliongeza, "Tuliwafunga Zamalek, watu laki mbili walikuja kutupokea na bahati mbaya watu walikufa siku hiyo, sasa baada ya kushinda mimi niliitisha mkutano, nikasema jamani tumebahatika tumeshinda lakini hebu tujilinganishe na klabu ya Zamalek. Leo bajeti yetu ni shilingi ngapi na bajeti ya Zamalek ni shilingi ngapi? Leo Simba bajeti yake ni bilioni moja kwa mwaka it's a joke!

Mimi nimekuja na fikra nimesema kwamba jamani kwanini kuna watu wamesema wamejenga Simba? Tunawapa hisa bure za milioni 10 kila mmoja, tumefanya projection tunaweza kuraise zaidi ya bilioni 30 mpaka bilioni 40. Ukishapata bilioni 40 leo, ukienda kununua treasure bond unapata asilimia kumi tano."

"Sasa ukiwa na 40 bilioni , 10% ya 40 bilioni ni 4 na 5% ni 2 bilioni maana yake 6 bilioni. Unatoka kwenye 1 billion ya leo unaingia kwenye 6 bilioni, maana yake nini?

Unaweza kumwajiri kocha mzuri, unaweza kuwa na gym pamoja na viwanja, unaweza kununua wachezaji ukashindana na Zamalek na hatimaye baada ya miaka mitano unaweza kushinda African Champions League," alisisitiza.

Chanzo: Bongo5
 
Kwani haiwezekani kufuata nyayo za Azam akaanzisha klabu yake mwenyewe kuliko kusubiri kuzozana na akina sembo kila uchao?

Akiinunua Simba wanachama wanapoteza haki yao ya umiliki na haki ya kufanya maamuzi
 
Last edited by a moderator:
Mi naona ifike wakati hizi timu Simba na Yanga zimilikiwe na mtu binafsi ili maamuzi ya haraka yafanyike...
Mambo ya kusikiliza kila tawi yashapita
 
African lyon ilimshinda akaiuza,ngoja niendele kudunduliza kisent ili ifike mo aniuzie mikia fc,hlf niifutilie kwa mbali kwenye ramani ya mpira wa bongo,timu gani linaroga na kununua mechi km nn cjui!
 
Simba wakiipoteza hiyo ofa ya MO watajuta,mpira wa sasa unahitaji fedha nyingi na mikakati mikubwa ya kupata fedha Yanga na Azam zinasajili wachezaji wazuri kwa sababu ya fedha ingawa Yanga nao siku akiondoka Manji nao watarudi kule kule kwa Simba.

Sumba sasa haina fedha wala hakuna kiongozi mwenye mipango ya kuleta fedha Simba huo ndio ukweli nilimsikia aliyekuwa katibu wa Simba Ezekiel Kamwaga kwenye kipindi cha michezo cha cloud tv kwamba walikuwa wanakosa fedha za kulipa mishahara watendaji wa club.

ni aibu kubwa kama kweli tunaipenda hii timu ni lazima mashabiki na wanachama wakubali kuiuza imilikiwe na mtu mmoja au watu wachache,haiwezekani leo MO aje adhamini Simba achangie Simba halafu nguvu /sauti yake kwenye Simba ilingane na mwanachama anayechangia 10,000 kwa mwaka.
 
Kwanza nimpongeze Mo kwa uzalendo na mapenzi makubwa kwa simba na kwa taifa lake.
Pili nitamshangaa mtu yeyote mpenda soka; ambae hata ona fursa ya maendeleo mpira wa miguu itakayopatikana kwa Simba kupata mmiriki mwenye uwezo wa kuindesha klabu hiyo kongwe nchini.
Kutokana na mashaka ya baadhi ya watu hebu tujiulize maswali machache ya msingi,
Nani na ananufaika na nini simba ikiwa katika mikono ya wanachama?
Nani na atakosa nini Simba ikimilikiwa na Dewji?
Je upi mkakati wa wamiliki wa simba wa sasa wa kuifanya simba iwe timu yenye mafanikio katika soka la afrika na ulimwenguni kwa ujumla ili wawe na sababu ya kuing'ang'ania klabu?
Mimi kama mpenzi wa soka la kisasa napendekeza kwenu wadau tukubali kuwakaribisha watu wetu wenye uwezo wawekeze kwenye soka kwa maslahi mapana ya soka letu.

Nasema tena hongera sana Mheshimiwa Dewji kwani mimi naunga mkono hoja yako kwa mikono miwili. 😁😂😂😂
 
Mo Dewji ni mfanyabiashara kama wafanyabiashara wengine.. Japo ni mnazi mkubwa wa Mnyama, ila yeye si mjinga kutaka ku take risk kwa kuwekeza 20B katika timu.. lazima kuna kitu anakitafuta.
Narudia tena, tunatakiwa tuwe makini katika hili.
 
ingependeza sana kama angeanzisha MO FOOTBALL CLUB. halafu ikawa na ubora kama azam, yanga na simba.
 
Nilimsikia ktk kipindi cha mkasi, huyu jamaa ni mfanyabiashara mkubwa sana na anajua jinsi ya kusaka doo na kukuza himaya, alivyoongea aliongea points sana, kama atapewa nafasi hiyo ataifanya simba iwe na uwezo mkubwa sana kifedha.

Tatizo ni wanachama wenye njaa waliogeuza simba kama sehemu ya kipato.
 
Mo Dewji ni mfanyabiashara kama wafanyabiashara wengine.. Japo ni mnazi mkubwa wa Mnyama, ila yeye si mjinga kutaka ku take risk kwa kuwekeza 20B katika timu.. lazima kuna kitu anakitafuta.
Narudia tena, tunatakiwa tuwe makini katika hili.

washabiki wenyewe ndio kuwaza hivi kila siku bora niendelee kuishabikia arsenal yangu tu
timu haiwezi kupangwa na wanywa kahawa na kucheza bao siku nzima halafu ikapata kombe la afrika

Mpira wa bongo umenishinda
 
ingependeza sana kama angeanzisha MO FOOTBALL CLUB. halafu ikawa na ubora kama azam, yanga na simba.

Kupata fanbase hapa bongo ni tatizo. Azam yenyewe Chamazi hawajazi. Watu tumeshachomelewa simba ma yanga, hii itaathiri hata vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom