Mohamed Dewji kuinunua Simba

Mohamed Dewji kuinunua Simba

Ni wazo zuri..kinachohitajika ni elimu kwa members na mashabiki..wakielomika watakubali na wataenfelea kuipenda Simba kama vile ManU etc
 
Aanzishe timu yake au akanunue timu nyingine ndogo abadirishe jina aendeleze soka nchini.

Timu sio simba na yanga tu. Aongeze ushindani, bilioni 20 inatosha kuanzia.

Mambo ya kuanza kusumbuana na wanachama ambao kitu muhimu kwao ni kuifunga Yanga tu hatutaendelea.
 
JBinafsi napenda simba iuzwe,huu mfumo wa timu kuwa ya wanachama unadumaza maendeleo ya soka tz haufai kabisa..simba na yanga waking"ang"ania huu mtindo watasherekea miaka mia wakiwa hawana hata uwanja wa mazoezi...tukiachana na hayo sasa hivi simba imeshika mwelekeo wa kuwa timu ndogo kama ilivyo liverpool uingeleza ,simba haimo kwenye ushindani wa ubingwa na haitotokea hata siku moja,mimi kama shabiki wa yanga siihofii simba hata chembe na uzingatie timu zenye pesa zinaongezeka wachangamkie hiyo opportunity....najua simba ikiuzwa na mashabiki wa yanga watapata akili ,nao watamkabizi manji timu yao
 
Ningekua mimi ningempatia hiyo timu bure Ila kwa sharti lakutobadilisha jina la timu.Mi shabiki wa Simba ila sioni mipango endelevu tena pale.Ila najua kuna watu maisha yao wanaendesha kupitia Simba hivyo sidhani kama watakubali imilikiwe na mtu mmoja.
 
ningekua mimi ningempatia hiyo timu bure ila kwa sharti lakutobadilisha jina la timu.mi shabiki wa simba ila sioni mipango endelevu tena pale.ila najua kuna watu maisha yao wanaendesha kupitia simba hivyo sidhani kama watakubali imilikiwe na mtu mmoja.
miaka 75 timu haina hata uwanja wa maonyesho?
 
Kuepuka figisufigisu za mashabiki maandazi aanzishe yake hizi timu mbili zina mtaji mkubwa wa wanachama na mashabiki ila dira ndo hakuna mfano uhamasishe wanachama na mashabiki wanunue gazeti la yanga imara au ngurumo za simba kwa wiki wangekuwa wanaingiza kipato kikubwa na shabiki anajua hanunui khabari tu ila anakuwa kaichangia timu ila ndo hivyo tena
 
Sio lazima mtu mmoja amiliki 51%. Kwani timu za Kijerumani na Kispanyiola zinamilikiwa na akina nani? Fanya timu iwe kampuni, halafu tangaza bei ya hisa na sharti mwanahisa asiruhusiwe kumiliki zaidi ya 10% ya hisa. Na wenye hisa zaidi ya tano waingie kwenye bodi ya timu na wenye hisa chache wawe wanachagua wawakilishi kwenye bodi. Tutasonga tu.
 
Timu ya simba inawenyewe na ningumu sana kufanya kazi kwenye timu kama ile ni bora angeanzisha timu yake mwenyewe toka mwanzo ili awe na uwezo wa kuindesha jinsi anavyotaka . Pia asiangalie kupata faida kwa siku za mwanzo maana naona amekaa kibiashara zaidi.
 
ile timu yake ya singida ilimshinda nini??
Ile timu haikuwahi kuwa yake, alikuwa mfadhili na kutokana na viongozi vilaza kuona anafaidi akawaachia timu yao ikawashinda ikafia mbali.......
 
Wale wazee wanaovaa kofia watakataa,na watasikilizwa.
Ndo wanaodidimiza soka kwa njaa zao.... ila akitaka awaweke kwenye mipango yake kama Manji alivyowakamata akina Akilimali..
 
Back
Top Bottom